UNEP yawateua wanamuziki wawili wa Kenya kuwa mabalozi wema.

Kusikiliza /

UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limewateua wanamuziki wawili maarufu kuwa mabalozi wake wema nchini Kenya. Susan Owiyo na Erick Wainaina wote kutoka Kenya wametangazwa rasmi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya. Susan Owiyo ameshashiriki kwenye tamasha mbali mbali za kimataifa kwenye miji maarufu duniani likiwemo tamasha la rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela mwaka 2008 mjini London nchini Uingereza na pia kwenye tamasha kama hilo kwenye ukumbi wa City Hall mjini New York nchini Marekani mwaka 2009. Naye Erick Wainanaina ni mwanamuziki aliyetunukiwa tuzo kadhaa kwenye taaluma yake ya uimbaji zikiwemo za kimataifa. Mabalozi hao wawili wamelishukuru shirika la UNEP kwa kuwatambua na wakaahidi kutoa mchango kuwahamasisha watu kuhusu utunzi wa mazingira.

 

(SAUTI ZA SUSAN NA ERIC)

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Oktoba 2017
T N T K J M P
« sep    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031