UN-Habitat yazindua ripoti kuhusu ukuaji wa miji

Kusikiliza /

Ripoti mpya ya Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, imesema kuwa watunga sera na wadau katika masuala ya maendeleo wanatakiwa kuzingatia ukuaji na maendeleo jumuishi zaidi.

Ripoti hiyo iitwayo, “Hali ya miji ya dunia mwaka 2012/2013,” na ambayo inahusu ukuaji wa miji, inasema kuna haja ya kuzingatia ukuaji unaozidi ukuaji wa kiuchumi tu, ambao umechangia sera dni kwa miongo mingi.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, sera zinazofaa kuangaziwa kwa sasa, ni zile zinazojumuisha masuala ya viwango vya ubora wa maisha, miundo mbinu tosha, usawa na mazingira endelevu. Akizindua ripoti hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa UN-Habitat, Dr Joan Clos, amesema UN-Habitat inapigia debe aina mpya ya miji, ambayo inaambatana na karne ya 21, na ambayo inaangazia zaidi watu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031