UM walaani mashambulio ya kigaidi ya karibuni Somalia

Kusikiliza /

Balozi Augustine Mahiga, Mkuu wa UNPOS

Ofisi ya masuala ya kisiasa kuhusu Somalia katika Umoja wa Mataifa (UNPOS), imelaani mashambulizi ya kigaidi ambayo yametekelezwa nchini Somalia katika kipindi cha wiki mbili za kwanza mwezi Februari mwaka 2013, pamoja na kuuawa kwa msomi maarufu wa Kiislamu, Sheikh Abdiqadir “Ga’amey” Nur Farah, kule Garowe.

 

Mauaji ya Dkt. Nur Farah yametendeka baada ya shambulio la kujitoa mhanga katika mji wa Galkayo, kati mwa Somalia, na ambalo liliwalenga maafisa wakuu wa polisi katika jimbo la Puntland, na mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mengine likiwemo lile la bomu la gari kwenye mkahawa wa Lido mjini Mogadishu, ambalo lilimuuwa mkuu wa idara ya ujasusi katika wilaya ya Shibis.

 

Mwakilishi Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Somalia, Augustine Mahiga, ametoa wito kwa watu wa Somalia kuimarisha nguvu zao za kupinga ugaidi kwa kushirikiana na vyombo vya utawala ili kuwafikisha wahusika mbele ya sheria

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930