UM wakosoa muswada unaobinya uhuru wa kuandamana Misri

Kusikiliza /

Waandamanaji nchini Misri

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekosoa hatua ya upitishwaji wa muswada wa sheria inayobinya uhuru wa watu kufanya maandamano iliyoungwa mkono na baraza la mawaziri wa  nchi hiyo. Pillay amesema kitendo hicho hakifungamani na misingi inayolinda na kutetea haki za binadamu.

Amesema kuwa pamoja na ukweli kwamba uhuru wa kukusanyika unapaswa kuwa na mipaka, lakini suala la uhuru wa binadamu ni jambo linalopaswa kuzingatiwa kwa mapana yake. Amefafanua kuwa uhuru wa kukusanyika ni moja  ya mihimili inayounda demokrasia ambayo pia inaelezwa kwenye tamko la pamoja la dunia kuhusu haki za binadamu na Misri imeridhia, hivyo kubinywa kwa njia yoyote hakuwezi kukubalika. Rupert Colville ni msemaji wa kamishna hiyo.

(SAUTI YA RUPERT)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031