Ukabila na udini tishio kwa amani duniani: Dieng

Kusikiliza /

Adama Dieng

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limehadharishwa kwamba  ongezekeo la uhasama wa vikundi vya kidini na kikabila katika nchi kadhaa linaweza kuchochea ghasia katika nchi hizo.

Akihutubia baraza hilo katika mkutano wa 22 unaoendelea, Mshauri maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kimbari Adam Dieng amesema nchi zinazokabiliwa na tishio hilo ni Syria,Mali,Sudan,Pakistan,Kyrgstan pamoja na Iraq.

Bwana Dieng ametoa wito kwa Baraza la Haki za Binadamu kutafunjia za  kuzuia tishio hilo kwa sasa ili kuepuka madhara makubwa kwa siku zijazo huku akitolea mifano ya macahafuko yaliyosababishwa na vikundi vya udini na ukabilakatika nchi za  Holocaust, Cambodia, Rwanda, and Sebrenica na kusisitiza kuwa machafuko yaliyotokea katika nchi hizo yanaashiria kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kukomesha ghasia.

SAUTI YA ADAM DIENG

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031