Ugonjwa wa ngozi uenezwao kwa uchafu walipuka Syria

Kusikiliza /

Watoto Syria

Ugonjwa wa ngozi uenezwao kutokana mazingira machafu, Leishmaniasis umeripotiwa kulipuka nchini Syria, ikiwa ni miezi kadha tangu kutolewa kwa onyo juu ya uwezekano wa kulipuka kwa ugonjwa huo.

Visa 955 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwenye maeneo ya Hamah, Hassaka, Damascus na Homs nchini Syria.

Shirika la afya duniani WHO limetoa huduma zikiwemo madawa na mahitaji mengine muhimu kwa vituo vya afya ili kuviwezesha kuwahudumia karibu wagonjwa 165,000.

Idadi ya wakimbizi wa Syria wanaowasili nchini Jordan imezidi wakimbizi 3000 kwa siku na kuwa mzigo wa WHO na washirika wengine.

Inakisiwa kuwa hali hii itakuwa yenye changamoto bila kuwepo msaada kutoka kwa WHO.

Shirika la WHO nchini Lebanon limeendesha chanjo maeneo ya kaskazini likiwalenga watoto 8000. Saudi Arabia nayo imetoa msaada wa dola milioni 2.1 kwa msaada wa dawa na chanjo kwa wananchi wa Syria.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031