Thuluthi mbili za visa vya saratani vyaweza kuepukika: WHO

Kusikiliza /

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema zaidi ya asilimia sabini ya visa vya ugonjwa wa saratani vinaweza kuzuiliwa. Kwenye ujumbe wake wa siku ya saratani duniani ambayo ni leo tarehe nne Februari, WHO imesema hili linawezekana ikiwa nchi zitaongeza uwezo wao wa kudhibiti saratani.

Shirika hilo limesema na kwamba nusu ya nchi kote duniani hazina uwezo kama huo, na wala hazina mpango tekelezi wa kuudhibiti ugonjwa huo, ambao unajumuisha kuzuia, kugundua mapema, kutibu na huduma za uuguzi.

Kwa mujibu wa WHO, watu milioni 7.6 wanafariki dunia kila mwaka kutokana na saratani, huku takriban watu milioni 13 wakiwa wanapatikana na kansa kila mwaka. Joshua Mmali na ripoti kamili

RIPOTI YA JOSHUA

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930