Somalia bado yahitaji misaada ya kibinadamu : WFP

Kusikiliza /

Wanawake na watoto Somalia wakisubiri msaada

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema bado Somalia inahitaji misaada ya kibinadamu kwa kuwa mafanikio yaliyopatikana kwenye uhakika wa chakula na usalama bado si endelevu hususan maeneo ya Kusini ambako ni vigumu kuingia.

WFP imesema zaidi ya watu Milioni Moja Kusini mwa Somalia wanahitaji misaada huku ikitaja watoto zaidi ya Laki Mbili wenye umri wa chini ya miaka mitano wanaokabiliwa na unyafuzi ambapo asilimia 70 wanaishi kusini mwa Somalia.

Watoto hao ni miongoni mwa watu Milioni Moja nukta sita ambao watapatiwa msaada wa chakula na shirika hilo kwa mwaka huu wa 2013 wakati huu ambapo shirika hilo linasema linakabiliwa na pungufu ya dola Milioni 57 kwa ajili ya operesheni ya usambazaji wa chakula kwa miezi Sita ijayo.

Hata hivyo WFP imesema pamoja na kusambaza misaaada ya kibinadamu, programu zake sasa nchini Somalia zitajikita katika kujenga uwezo wa wasomalia kukabiliana na njaa na mafuriko.  Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP.

 (SAUTI YA BYRS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930