OCHA yaonya kuhusu kuendelea kwa mzozo wa Syria

Kusikiliza /

Wananchi wa Syria wakisubiri misaada

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limeonya kuwa kadri mzozo wa Syria unavyoendelea wakati huu ukiingia takribani mwaka wa pili mahitaji ya kibindamu yanaongezeka na hivyo ni vyema mgogoro huo ukapatiwa ufumbuzi.

OCHA imesema kwa sasa kuna zaidi ya watu Milioni Nne wanahitaji msaada wa dharura na wengine zaidi ya Milioni Mbili ambao wamejikuta wakimbizi ndani ya Syria.

Shirika hilo limesema wakati huu ambapo mashirika ya misaada yanahana kusambaza misaada ni vyema ahadi ya zaidi ya dola Bilioni Moja na Nusu iliyotolewa katika mkutano wa wahisani huko Kuwait wiki iliyopita ikatekelezwa fedha zipatikane kwa ajili ya misaada.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA.

 

(SAUTI YA JENS)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031