Mgogoro unaoendelea Syria waibua ugonjwa wa ngozi

Kusikiliza /

Taka zikiwa zimesambaa eneo moja nchini Syria

Shirika la Afya duniani WHO limesema mzozo unaoendelea nchini Syria unaendelea kusababisha uhaba wa dawa muhimu kama vile vile nusu kaputi na dawa za kuondoa maambukizi mwilini pamoja na kuibuka kwa magonjwa ya ngozi.

WHO inasema maduka ya dawa nchini Syria yanazidi kukosa uwezo wa kutoa dawa za msingi kama vile zile za kutuliza maumivu kwa kuwa mamlaka za afya kwenye majimbo hazipokei mgao wa kutosha kutoka mamlaka kuu.

Glen Thomas ni afisa kutoka WHO.

(SAUTI YA GLEN)

Tumepokea taarifa za ongezeko la wagonjwa wa ugonjwa wa ngozi Laschminiasis kwenye maeneo ya Aleppo. Ugonjwa huu umesambaa na unatokana na mazingira machafu. Moja  ya chanzo cha ugonjwa huu ni menejimenti mbovu ya takataka na hata afya duni ya binadamu inayosababishwa na mgogoro unaoendelea."

Wakati huo huo shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokwenda HOMS umebaini ukwa watoto Laki Mbili na Elfu Kumi wanahitaji msaada wa dharura.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031