Global Fund yazindua utaratibu mpya wa kutoa ufadhili

Kusikiliza /

Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria, Global Fund, umezindua utaratibu mpya wa kufadhili mapambano hayo, ambao utawahusisha wadau wote kikamilifu.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, utaratibu huo mpya wa kutoa ufadhili utasaidia taasisi anayoiongoza kuwafikia walengwa ambao ni watu walioathirika na Ukimwi, Kifua kikuu na malaria.

Kiasi cha hadi dola bilioni 1.9 za kimarekani zipo kwa ajili ya ufadhili wa shughuli za 2013 na 2014. Global Fund imezitaka nchi mbalimbali duniani kutaja kwa njia ya uwazi kiwango cha fedha zinazohitaji ili kufanikisha kukinga watu wake na ukimwi, kifua kikuu na malaria.

Kutokana na fedha zilizopo, kila nchi nchi itapokea kiasi cha hadi dola bilioni 5 za kimarekani, fedha ambazo zinaweza kuongezeka kulingana na mahitaji

Utaratibu huu mpya wa kutoa ufadhili utachukuwa nafasi ya mbinu ya zamani ya ufadhili, na utatekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2014 hadi 2016.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930