Mamia washiriki mbio za UNEP na mazingira Nairobi

Kusikiliza /

Wanariadhi wanaochipukia walioshiriki mbio hizo

Takribani wanariadha Elfu Mbili wakiwemo waliobobea na wanaochipukia, wanafunzi, wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa waliingia kwenye barabara za mji mkuu wa Kenya Nairobi kwenye awamu ya pili ya mbio za Nusu marathoni zilizoandaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Mbio hizo zilikuwa ni za kusherehekea kutangazwa kwa mji  wa Nairobi kuwa mji mkuu wa mazingira duniani kufuatia tangazo lilitolewa na baraza kuu la Umoja wa Mataifa mwezi Disemba mwaka uliopita. Akizungumza muda mfupi baada ya kukamilika kwa mbio hizo Mkurugenzi Mkuu wa UNEP Achim Steiner amesema kuwa uungwaji mkono ulioshuhudiwa kwenye mbio hizo ni ishara ya uhusiano mzuri uliopo kati ya taifa la Kenya na UNEP. Amesema kwa zaidi ya miaka 40 UNEP imepata uungwaji mkono kwenye masuala ya mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930