Liberia yahitaji dola Milioni 37 kukidhi mahitaji ya kibinadamu 2013

Kusikiliza /

Wakimbizi nchini Liberia

Serikali ya Liberia na Umoja wa Mataifa hii leo wametangaza ombi la dola Milioni 37 zitakazotumika kukidhi mahitaji ya binadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2013 kutokana na hali ngumu inayoendelea kukabili wananchi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari kuwa Liberia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu ambapo takribani nusu ya wananchi ni mafukara wakitumia chini ya dola moja kwa siku kukidhi maisha yao huku kukiwa na jukumu la wakimbizi

(SAUTI YA Martin)

"Zaidi ya wakimbizi Elfu Sitini na Wanne wa Ivory Coast bado wanaishi Liberia tangu wakimbie vurugu zilizotoka na uchaguzi nchini mwao, na wakimbizi wa zamani Elfu Ishirini na watano wa Liberia waliorejea nchini mwao nao bado wanahitaji misaada muhimu ya kibinadamu."

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031