IOM yasambaza misaada kwa waathirika wa mafuriko Chad

Kusikiliza /

Wahanga wa mafuriko Chad

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya dharura kwa mamia ya watu waliokumbwa na mafuriko katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na maeneo mengine ya jirani na kusababisha kiasi cha watu 98,000 kupoteza makazi yao na wengine 560,000 kuwa katika hali ya shida na taabu.
IOM kwa kushirikiana na maafisa wa serikali inasambaza huduma muhimu katika maeneo ya  Bongor, Hadjer Lamis  na N'Djamena yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo.

Mataifa kadhaa ya Magharibi ikiwemo Ujerumani imeanza kuchangisha mafunga ya fedha kwa ajili ya kufanikisha shughuli za usambazaji wa huduma za usamaria mwema ikiwemo mahitaji ya chakula na mengine ya kawaida.
Shirika la Mpango wa chakula duniani WFP limepeleka msaada wa chakula kuzikirimu zaidi ya familia 15,000 ambazo zipo kwenye mkwamo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031