Hatua mathubuti zahitajika kukabili ukatili wa kingono Afrika Kusini: Pillay

Kusikiliza /

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea kushtushwa na kuhuzunishwa na kitendo cha ubakaji na mauaji ya kikatili ya msichana mmoja raia wa Afrika Kusini, na kutaka mkakati wa kina uwekwe ili kukabiliana na suala la ukatili wa kingono, ambalo amelitaja kuwa jinamizi linalowakumba maelfu ya wanawake nchini Afrika Kusini.

Msichana Anene Booysen mwenye miaka kumi na saba, anadaiwa kubakwa na wanaume kadhaa, kabla ya kukatwakatwa na kuawa mnamo tarehe 2 Februari, katika mji wa Bredasdorp, takriban maili themaini kutoka mji wa Cape Town.

Bi Pillay amekaribisha mwitikio wa Rais Jacob Zuma na wengine kwa tukio hilo, ingawa amesema jamii nzima ya Afrika Kusini haikutakiwa kusubiri tukio hili la kushangaza ndipo ichukuwe hatua kukabiliana na tatizo la ubakaji ambalo limeenea nchini humo. Amesema kuna haja ya kutoa ujumbe mkali kwamba ukatili wa kingono kamwe haukubaliki, na kwamba wahalifu watakabiliwa ipasavyo kwa ajili ya vitendo vyao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031