Familia 967 zahamishiwa kwenye kambi huko DRC: IOM

Kusikiliza /

Familia za wakimbizi katika moja ya shule huko Goma, DRC

Shirika la kimataifa la Uhamiaji, IOM pamoja na washirika wengine wamekamilisha mpango wa siku mbili wa kuhamisha familia 967 zilizokuwa zimepata hifadhi katika shule tatu na kuwapeleka kwenye kambi za wahamiaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC.

Kuondoshwa kwa familia hizi kutoka shule za Ushindi, Neema na Nazareen na kupelekwa kambi ya Mugunga 1, kutaziwezesha shule hizo kufunguliwa kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa mgogoro uliosababishwa na uvamizi wa waasi wa kikundi cha M23 kwenye mji wa Goma Mashariki mwa DRC mwezi Novemba mwaka jana. Jumbe Omari Jumbe ni msemaji wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930