Baraza la Usalama laonya wanaoingilia mchakato wa mpito Yemen

Kusikiliza /

Baraza la Usalama la UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo kuhusu Yemen ambayo pamoja na kupongeza tangazo la kuwepo kwa mjadala wa kitaifa nchini humo baadaye mwezi huu inaonya wale wote wanaokwamisha mchakato wa mpito nchini humo akiwemo Rais wa zamani Ali Abdullah Salehe.

Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, Mwakilishi wa kudumu wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Mark Lyall Grant amesema baraza limeonyesha matumaini kuwa mjadala huo wa kitaifa utawezesha kufanyika kwa kura ya maoni juu ya katiba na hatimaye uchaguzi mwezi Februari mwakani.

Amesema Baraza la usalama limeonya kuwa iwapo vitendo vya kuingilia mchakato wa mpito Yemen utaendelea, Baraza litachukua hatua kwa mujibu wa ibara ya 14 ya katiba iliyoanzisha Umoja wa Mataifa.  Halikadhalika Balozi Grant amesema tarehe Saba mwezi ujao, Uingereza itakuwa mwenyeji wa mkutano wa marafiki wa Yemeni utakaofanyika mjini London.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031