Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi ya UM huko Guinea Bissau

Kusikiliza /

Kikao cha baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2092 kwa Guinea Bissau ambalo pamoja na mambo mengine linaongeza kwa miezi mitatu zaidi muda wa ofisi ya umoja huo nchini humo, UNOGBIS. Ofisi hiyo ina jukumu la kusaidia kuimarisha mchakato wa ujenzi wa amani nchini humo na kiongozi wa ofisi hiyo ni Rais wa zamani wa Timor Letse Jose Ramos Horta. Azimio hilo liliwasilishwa na nchi tano ikiwemo Rwanda, Morocco na Uingereza. Katika hatua nyingine Baraza la Usalama wamejadili hali ya amani huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC ambapo wamepokea ripoti ya katibu Mkuu kuhusu ofisi ya kulinda amani nchini humo MONUSCO. Akiwasilisha ripoti  hiyo Mkuu wa MONUSCO Roger Meece amesema hali ya amani katika baadhi ya maeneo ya Mashariki mwa DRC inazorota na kukwamisha usambazaji wa misaada ya kibinadamu

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031