Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Mashariki ya Kati

Kusikiliza /

Jeffrey Feltman, akitoa taarifa mbele ya Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali katika Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina. Akilihutubia baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman amesema kuwa shambulizi la kombora dhidi ya Isarel kutoka Gaza linaonyesha hali kuwa tete kati ya Isarel na Palestina.  Amesema pia Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu sana suala la mahabusu wa Kipalestina wanaozuiliwa na Israel, akisema kwamba Umoja wa Mataifa unatoa unashikilia kuwa wale wanaozuiliwa washtakiwe au waachiliwe.
Kuhusu Syria, Bwana Feltman amesema machafuko yanaendelea kutia wasiwasi, huku nchi jirani zikiwa katika hatari ya kuingizwa kwenye mzozo huo. Amesema wanaoendeleza uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu watakabiliwa na mkono wa sheria.

(SAUTI YA FELTMAN)

Katika ripoti yake ya wiki ilopita, tume huru ya uchunguzi ya Baraza la Haki za Binadamu ilisema kuwa serikali na makundi ya upinzani yametekeleza ukatili na kutojali uhai wa mwanadamu. Wote wametenda maovu ambayo ni sawa na uhalifu wa kivita, ingawa viwango vya maovu yalotekelezwa na serikali vinazidi vile vya upinzani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930