Ban na Jim wajadili malengo ya maendeleo ya milenia

Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim ambapo wameangalia upya fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili hizo hususan kwenye maeneo ya nchi za Maziwa Makuu barani Afrika.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Bwana Ban na Bwana Jim wamejadili pia kuharakishwa utekelezwaji wa malengo ya maendeleo ya milenia yanayofikia ukomo mwaka 2015, sambamba na mchakato wa ajenda ya maendeleo baada ya mwaka 2015.

Viongozi hao wawili walijikita zaidi pia kweney suala la utoaji fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo na changamoto za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031