Ban amteua Tamrat Samuel kama Mwakilishi wake Maalum Liberia

Kusikiliza /

UNMIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametangaza uteuzi wa Bwana Tamrat Samuel kama naibu mwakilishi wake maalum wa masuala ya uongozi wa kisheria katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL).

Bwana Samuel atamrithi Bwana Louis M. Aucoin kutoka Marekani, ambaye amehitimisha majukumu uake mnamo Disemba 2012. Bwana Ban ameelezea kufurahishwa kwake na Bwana Aucoin kwa kujitolea kwake kutenda kazi wakati wa muhula wa mwaka mmoja na UNMIL.

Bwana Samuel ana uzoefu wa takriban miaka 30 ya kufanya kazi na Umoja wa Mataifa., huduma yake katika idara ya masuala ya kisiasa ikizingatia zaidi masuala ya kisiasa katika maeneo ya Asia na Pasifiki.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930