Ban ahimiza ustahmilivu na heshima kupunguza migawanyo na migogoro

Kusikiliza /

ban kwenye kongamano la Alliance of Civilzations, Vienna, Austria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema viongozi kote duniani, wawe wa kimataifa au kimataifa, wanafaa kuongea lugha ya kustahmiliana na heshima, na kujitenga na migawanyo na kuharibiana sifa. Akiongea kwenye kongamano la muungano wa nchi zinazoendeleza ustaarabu linalofanyika mjini Vienna, Austria, Bwana Ban amesema masuluhu ya kudumu kwa migawanyiko yanaweza tu kutokana na uelewa unaovuka mipaka ya kidini, kitaifa, kitamaduni na kikabila.

Ameongeza kuwa uelewa kama huo unatokana na uongozi wa kuwajibika, ambayo ndiyo kauli mbiu ya kongamano hilo la Vienna.

Bwana Ban amesema wakati huu ambao hali ya hatari imetanda, muungano huo wa ustaarabu unahitajika zaidi kufaulu, akitoa mifano ya maeneo ambako umesaidia kupunguza hatari za machafuko na vifo, kama vile Pakistan, Mindanao na Kenya, ambako uchaguzi unafanyika wiki ijayo

(SAUTI YA BAN)

Bwana Ban amesema muungano huo unaweza kusaidia katika kukabiliana na mizozo ya Mali na Syria, na hali ya mkwamo wa juhudi za amani kati ya Waisraeli na Wapalestina

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031