Ban aelezea kusikitishwa na hatma ya wafungwa wa Kipalestina

Kusikiliza /

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na hali inayoendelea kuzorota ya wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa na mamlaka ya Israel, na ambao sasa wanafanya mgomo wa kutokula chakula.

Taarifa ya msemaji wake imesema Bwana Ban, ambaye amesikitishwa zaidi na hali ya mfungwa Samer Issawi, amepokea barua kutoka kwa Rais Mohammud Abbas, na kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu. Bwana Ban pia amemwelezea Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu hisia zake katika mazungumzo kwa njia ya simu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kinachomsikitisha Katibu Mkuu zaidi ni wafungwa ambao wanazuiliwa chini ya utawala wa Israel bila mashtaka. Amesema wale wanaozuiliwa wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria na kushtakiwa kulingana na viwango vya kimataifa, au waachiliwe huru mara moja.

Bwana Ban ametoa wito suluhu lipatikane bila kuchelewa ili kuhakikisha hatma ya wafungwa hao na kulinda utulivu.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2017
T N T K J M P
« apr    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031