Nyumbani » 26/02/2013 Entries posted on “Febuari 26th, 2013”

UNAIDS na UNDP zaunga mkono pendekezo la kusaidia nchi maskini kuendeleza na kuongeza ugawaji wa dawa muhimu

Kusikiliza / unaids

Shirika linalohusika na masuala ya HIV na UKIMWI, UNAIDS na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, leo yamezindua chapisho jipya linaosema kwamba kushindwa kupanua kipindi cha mpito kwa nchi maskini ili ziweze kuhitimu matakwa ya mkataba kuhusu masuala ya kibiashara yanayohusiana na haki miliki (TRIPS), huenda kukazuia uwezo wa watu kupata [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

UNICEF na washirika wakomboa watoto kutoka ajira migodini huko DRC

Kusikiliza / Watoto wakitafuta madini huko DRC

Ajira kwa watoto watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili nchi zinazoendelea. Katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC hali ni mbaya zaidi. Nchini humo sio ajabu kuwaona  watoto wenye umri wa kwenda shule wakifanya kazi za kujipatia kipato ambazo hata hivyo huwaingizia kipato kidogo  ikilinganishwa na kazi wanazofanya. Mwenzangu JOSEPH MSAMI anamulika [...]

26/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaelezea kushtushwa na mauaji ya watoto 70 kwa makombora Aleppo

Kusikiliza / maria calivis unicef

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watoto 70 katika shambulizi la makombora katika maeneo ya makazi mjini Aleppo, Syria, mnamo tarehe 18 na 22 Februari. Katika taairfa yake, Mkurugenzi wa UNICEF katika katika kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Maria Calivis, amesema [...]

26/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Mali umesambaratisha elimu na riziki za watu: OCHA

Kusikiliza / John Ging

Mkuu wa operesheni za Afisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) Bwana John Ging, amesema kuwa madhara ya mzozo wa Mali ni makubwa mno, mzozo huo ukiwa umeathiri shughuli zote za maisha.  . Bwana Ging amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa katika ziara yake nchini Mali, watu wengi wamesema [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Mashariki ya Kati

Kusikiliza / Jeffrey Feltman, akitoa taarifa mbele ya Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali katika Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina. Akilihutubia baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman amesema kuwa shambulizi la kombora dhidi ya Isarel kutoka Gaza linaonyesha hali kuwa tete kati ya Isarel na Palestina.  [...]

26/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utulivu wa eneo la Afrika Magharibi watikiswa na wasafirishaji haramu: UM

Jalada la ripoti hiyo ya UNODC

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa usafirishaji wa madawa ya kulevya aina ya Cocaine, usafirishaji haramu wa binadamu na madawa bandia yanahatarisha utulivu wa nchi za Afrika Magharibi. Ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa linalodhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC imesema kuwa mambo hayo yanayoendeshwa na magenge ya uhalifu ya [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kundi la wanawake 10 kupanda Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania:WFP

Kusikiliza / Kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Kundi la wanawake saba raia wa Nepal ambalo lina sifa ya kuukwea mlima mrefu zaidi duniani  wa Everest na milima mingine barani Ulaya na nchini Australia sasa limeungana na wanawake wengine watatu wenye asili ya Afrika kuukwea mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari yao ya kuukwea mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 itaanzia kwenye mji [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kenya fanyeni uchaguzi kwa amani epukeni ukimbizi wa ndani: UM

Kusikiliza / Bendera ya Kenya

Ikiwa imesalia siku Tano kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Umoja wa Mataifa umeitaka nchi hiyo kuchukua tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea vurugu zinazoweza kusababisha wakimbizi wa ndani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Ujumbe huo umetolewa na Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ambaye amesema historia ya [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 45 zahitajika haraka kuokoa wanawake na watoto Mali: UNICEF

Kusikiliza / Wanawake nchini Mali wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapimwe afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi la dharura la dola Milioni 45 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na watoto waliojikuta katikati ya mzozo nchini Mali kupata mahitaji ya kimsingi kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.  UNICEF inasema kuwa athari za mzozo unaoendelea kwa watoto ni kubwa mno ikitaja suala la [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito kwa vijana kuongoza katika kuendeleza amani na maendeleo

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo ya kwamba ulimwengu utategemea ujasiri na hatua mathubuti za vijana katika kutafuta amani na maendeleo endelevu. Bwana Ban amesema hayo mjini Vienna, Austria, akikutana na vijana wakati wa mkutano wa tano wa kimataifa wa nchi zinazotetea ustaarabu, yaani Alliance of Civilizations. Katibu Mkuu ametoa wito [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Tushirikiane kudhibiti usafirishaji haramu baharini: UNHCR

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu wa wakimbizi, Antonio Guterres,amerejelea wito wake akizitaka nchi zilizoko katika eneo la Asia Pacific kuanzisha mashirikiano ya pamoja ili kukabiliana na wimbi la watu wanaopoteza maisha wakati wakiwa kwenye misafara ya kimagendo katika bahari ya Hindi.  Ametoa wito huo wakati UNHCR ikiandaa mkutano utakaofanyika mwezi huu huko Indonesia [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima Ethiopia wanufaika na mpango wa P4P: WFP

Kusikiliza / Moja ya mashine zinazotolewa na WFP kusaidia wakulima Ethiopia

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limetangaza mafanikio makubwa ya mpango wake wa ununuzi wa chakula kwa maendeleo, P4P nchini Ethiopia baada ya vyama vya ushirika kuliuzia shirika hilo kiasi kikubwa cha chakula kinachotosha kulisha watu Milioni Moja nukta nane nchini humo kwa mwezi mzima.  Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Sauti [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na washirika wasaidia raia waliokimbia ghasia Darfur

Kusikiliza / Wakimbizi wa ndani katika kambi ya muda ya El Sireaf  nchini Sudan

Umoja wa Mataifa na washirika wake huko Sudan umelazimika kutoa misaada ya dharura na hata kuwasafirisha kwa ndege wahanga wa ghasia mpya za  wiki iliyopita huko jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan. Ujumbe wa pamoja wa Umoja huo na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID umeeleza kuwa mapigano hayo  yametokea wakati ambapo tayari Watu Elfu [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031