Nyumbani » 25/02/2013 Entries posted on “Febuari 25th, 2013”

Watoto, wazazi wajikita kwenye elimu huko Turkana

Kusikiliza / Watoto wa kiturkana wakipata elimu

Imezoeleka ya kwamba sehemu kubwa ya jamii ya wafugaji imekuwa nyuma kielimu husuani katika elimu ya msingi ambapo watoto wenye umri wa kwenda shule wamekuwa hawafanyi hivyo. Badala yake, watoto hawa hutumia muda mwingi kuchunga mifugo nakufanya kazi nyingine za nyumbani. Huko nchini Kenya katika eneo la Turkana kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, mambo yalikuwa hivyo  [...]

25/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Udhibiti wa mauaji ya kimbari bado safari ni ndefu: Dieng

Kusikiliza / Adama Dieng, Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa UM kuhusu masuala ya mauaji ya kimbari

Jumuiya ya kimataifa iongeze juhudi kuhakikisha mauaji ya kimbari kama yale yaliyotokea Rwanda na Bosnia-Herzegovina hayajirudii tena, na hiyo ni kauli ya Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya mauaji ya kimbari, Adama Dieng. Bwana Dieng ametoa ushauri huo wakati wa mjadala wa wazi kwenye siku ya kwanza ya kikao [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na viongozi wa UAE Dubai na Abu Dhabi

Kusikiliza / 494460-bansheikh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Mohammad bin Rashed Al Maktoum, ambaye ni Waziri Mkuu wa ufalme wa United Arab Emirates, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Mohammad Gargash. Katika mkutano huo, wamezungumza kuhusu maendeleo katika kanda nzima, yakiwemo masuala kuhusu Syria, Iran, Lebanon, [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova afanya ziara nchini Burkina Faso,akutana Rais Compaore.

Kusikiliza / Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amethibitisha kujitolea kwa shirika hilo kwa mwaka wa kimataifa wa ushirikiano wa sekta ya maji ambao unaoongozwa na shirika hilo. Bokova ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso nchini humo wakati wa ziara rasmi [...]

25/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 22 cha Baraza la Haki za Binadamu chaanza Geneva

Kusikiliza / Kikao cha Baraza la Haki za binadamu, Geneva, Uswisi

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo limefungua rasmi kikao chake cha 22, ambacho kitaendelea hadi tarehe 22 Machi, huku rasi wa Baraza hilo akieleza matarajio yake kuwa kikao hicho kitaendeleza heshima ya haki za binadamu, na hivyo kuendeleza pia usalama na maendeleo. Akiongea wakati wa kufungua kikao hicho cha 22, rais [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhuru na haki za binadamu ni muhimu kwa UM: Ban

Kusikiliza / Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amesema uhuru na haki za binadamu ni mambo muhimu ambayo yanasaidia kusongesha mbele shughuli za Umoja huo. Katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, Bwana Ban amesema baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka utekelezwaji wa mkataba DRC.

Kusikiliza / Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa limepongeza hatua ya utiwaji saini wa makubaliano ya amani na usalama kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na ukanda wa nchi za maziwa makuu uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Addis Ababa Ethiopia. Makubaliano hayo yalitiwa saini chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, nchi [...]

25/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamia washiriki mbio za UNEP na mazingira Nairobi

Kusikiliza / Wanariadhi wanaochipukia walioshiriki mbio hizo

Takribani wanariadha Elfu Mbili wakiwemo waliobobea na wanaochipukia, wanafunzi, wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa waliingia kwenye barabara za mji mkuu wa Kenya Nairobi kwenye awamu ya pili ya mbio za Nusu marathoni zilizoandaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Mbio hizo zilikuwa ni za kusherehekea kutangazwa kwa mji  wa Nairobi kuwa mji [...]

25/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ajira ya watoto kwenye sekta ya ufugaji imekithiri: FAO

Kusikiliza / Watoto wakichunga mifugo

Ajira za watoto katika sekta ya ufugaji ni kubwa na iliyopuuzwa na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAP kwenye utafiti kuhusu masuala ya ajira za watoto katika sekta ya ufugaji.   Kulingana na FAO  sekta ya kilimo inachukua nafasi kubwa kwenye ajira za watoto duniani na kwamba kukabilina na suala [...]

25/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU yazungumzia elimu kwa njia ya mtandao

Kusikiliza / Elimu mtandao

Shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU limesema kuwa mitandao ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi yaweza kuimarisha mfumo wa elimu duniani na kusaidia kufikia lengo la maendeleo la milenia la elimu kwa wote. Taarifa ya ITU imekariri ripoti mpya ya tume ya maendeleo ya mitandao ya kasi na mfumo wa digitali inayoeleza kuwa mitandao hiyo [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mikakati yaanza kudhibiti wahamiaji haramu: IOM

Kusikiliza / Usafirishaji wa wahamiaji haramu

Shirika la kimataifa la kuhudumia wahamiaji IOM, linakutana nchini Tanzania na maafisa uhamiaji kutoka Msumbiji, Malawi na wenyeji wa Tanzania kwa lengo la kubainisha mbinu za kisasa za kukabiliana na wimbi la wahamihaji haramu. Mkutano huo wa siku tatu, unafanyika wakati ambapo kiwango cha wahamiaji haramu kutoka eneo la Pembe ya Afrika wanaomiminika nchini Tanzania [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930