Nyumbani » 22/02/2013 Entries posted on “Febuari 22nd, 2013”

UM na Polisi Tanzania waimarisha utetezi wa haki za watoto na wanawake

Kusikiliza / Adolfina Chiallo, Mkuu wa dawati la Jinsia, Jeshi la polisi Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN kwa kushirkiana na jeshi la polisi nchini Tanzania wamezindua dawati maalum la masuala ya jinsia na watoto ambalo litamulika na kufuatialia vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto. Adolfina Chialo ni Kamishna msaidizi wa polisi anayesimamia dawati hilo la jinsia. (SAUTI YA ADOLFINA)

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hospitali ya kutembea yaleta nafuu Somalia

Kusikiliza / Wahudumu wa kliniki wakitoa huduma kwa wagonjwa Somalia

Wakazi wa maeneo kadhaaa ya Somalia wananufaika na huduma ya hospitali inayotembea ambayo imeanzishwa  ikiwalenga wakimbizi waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na  ukame na mapiganao yanayofanywa  na kundi la kigaidi la Al- Shabaab.  Hospitali hiyo inayohudumia takribani watu elfu tatu katika kambi ya KARIBU, na ambayo inamilikiwa na Jeshi la Somali na kudhaminiwa na Ujumbe [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya amani DRC, macho na masikio yaelekezwa Addis Ababa

Kusikiliza / Walinzi wa amani wa kikosi cha MONUSCO wakiwa na raia huko DRC

Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC imeendelea kuwa gumzo kila uchwao kutokana na mazingira yasiyotabirika, ambayo hufanya wakazi wake kuendelea kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao iliyosheheni rasilimali lukuki; chini ya ardhi na juu ya ardhi. Katika eneo hilo vikundi vya waasi kikiwemo kile cha M23 kimekuwa kikisababisha hofu miongoni [...]

22/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Njia mpya yapatikana kufika Mali Kaskazini: WFP

Kusikiliza / Watoto Mali

  Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, limeanzisha njia mpya kwa ajili ya kufanikisha safari za ardhini kuwasambaza huduma muhimu kwa maeneo yanahohitaji misaada ya dharura kaskazini mwa Mali. Hivi sasa misaada ya muhimu inasafirishwa kupitia njia inayoanzia mji mkuu wa Niger Niamey na kulekea moja kwa moja hadi kaskazini mwa Mali ambako kunashudia [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya watu milioni 1.2 kaskazini mwa Mali inatia wasiwasi: OCHA

Kusikiliza / Wakimbizi wa Mali

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limeelezea wasi wasi wake kuhusiana na hatma ya watu zaidi ya milioni 1.2 kaskazini mwa Mali ambao wameathiriwa na oparesheni za kijeshi. Hata hivyo kumekuwa na dalili za kuyafikia maeneo ya kati mwa Mali na pia kwa kiwango cha kidogo maeneo ya Kaskazini kufuatia [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mongolia yatajwa kuwa mwandalizi wa siku ya mazingira mwaka huu

Kipaumbele kwa uchumi unaolinda mazingira

Taifa la Mongolia ambalo limelipa kipaumbele suala la uchumi usioathiri mazingira kwenye sekta zake za kiuchumi zikiwemo sekta za uchimbaji madini na kutoa hamasisho kwa vijana litakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani mwaka huu siku ambayo itadhimishwa tarehe tano mwezi Juni.  Kauli mbiu ya siku hiyo inajulikana kama Think.Eat.Save. Reduce Your Foodprint ikiwa inaipa [...]

22/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka hatua zichukuliwe kuzuia ajali za boti kwenye Bahari ya Hindi

Kusikiliza / Usafiri wa boti kwa wanaohama jimbo la Rakhine

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeelezea kusikitishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokufa kwenye Bahari Hindi wakati wakikimbilia usalama wao na kutafuta maisha bora katika nchi za kigeni. Kwa mujibu wa UNHCR, wengi wao ni watu wa jamii ya Rohingya kutoka jimbo la Rakhine, Myanmar, na wengine wakitoka kutoka kwenye [...]

22/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi ya UM huko Guinea Bissau

Kusikiliza / Kikao cha baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2092 kwa Guinea Bissau ambalo pamoja na mambo mengine linaongeza kwa miezi mitatu zaidi muda wa ofisi ya umoja huo nchini humo, UNOGBIS. Ofisi hiyo ina jukumu la kusaidia kuimarisha mchakato wa ujenzi wa amani nchini humo na kiongozi wa [...]

22/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hollywood yamulika mradi wa ILO, yenyewe yatoa angalizo

Kusikiliza / Washiriki wa tukio hilo la kuhamasisha ajira zinazohifadhi mazingira

Mamia ya watu mashuhuri katika fani ya uigizaji na utunzi wa filamu wameshiriki katika tukio maalum la kutia shime mradi wa shirika la kazi duniani, ILO unaohusu ajira zinazozingatia uhifadhi wa mazingira. Shughuli hiyo iliyofanyika huko Hollywood, iliratibiwa na mtunzi wa filamu Hans Zimmer na mwongozaji filamu Ron Howard ambapo waliangalia miradi kama ule wa [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wawasihi wakazi wa Jonglei kuacha mapigano

Kusikiliza / Hilde Johnson

Mkuu wa ofisi ya Umoja  wa Mataifa nchini Sudan Kusini Hilde Johnson, amehitimisha ziara yake ya siku mbili kwenye jimbo la Jonglei nchini humo na kutaka jamii ziache mwendelezo wao wa ghasia. Ziara hiyo ilifanyika baada ya tukio la hivi karibuni la wizi wa mifugo na mashambulizi kwa dhidi ya raia kwenye jimbo hilo ambapo [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031