Nyumbani » 21/02/2013
Entries posted on “Febuari 21st, 2013”
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Mon amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki Dimitris Avramopoulos ambapo wamejadili hali ya kisiasa Mashariki mwa Mediteranian, na pia kuangazia matarajio ya kuanza tena mazungumzo ya kutafuta suluhu la kina huko Cyprus, pamoja na kutafuta suluhu kwa mgogoro kuhusu jina kati ya Ugiriki [...]
21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameiambia kamati maalum kuhusu kutokomeza ukoloni kwamba, sasa ndio wakati wa kuwa na ya aina mpya ya mazungumzo kuhusu ukoloni, na ambayo yanawajumuisha wote. Bwana Ban amesema kuwa jamii ya kimataifa sasa inashikilia hata zaidi dhana kuwa, ukoloni hauna nafasi katika ulimwengu wa sasa. Katibu Mkuu ameongeza [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Taarifa ya timu ya Umoja wa mataifa nchini Msumbiji inaonyesha Kwamba huenda mvua kubwa ikaendelea kunyesha na kusababaisha mafuriko makali zaidi katika ukanda wa kati na kaskazini mwa Msumbiji. Taarifa hii inakuja wakati huu ambapo kumekuwa na mlipuko wa kipindupindu katika jimbo la Cabo Delgado lililoko Kaskazini mwa Msumbiji ambapo watu 413 wameripotiwa kuugua huku [...]
21/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya juu ya kitisho cha ukosefu wa chakula inayoikabili Yemen ikisema kuwa hali ya ukosefu wa chakula huenda ikapindukia kuzidi ile ya mwaka uliopita 2012. WFP imesema kuwa, hali ya uzalishaji chakula imeporomoka kiasi cha kuzua kitisho ambacho kinaweza kuzorotesha ustawi wa kijamii. Imesema kuna wasiwasi wa familia [...]
21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mahakama Kuu ya Rufani nchini Haiti inatazamia kuendelea juma hili kuzikiliza kesi dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilivyofanyika wakati wa utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Jean-Claude Duvalier, Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navy Pillay ameitolea mwito serikali kutowakingia kifua wale waliohusika na vitendo [...]
21/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkutano uliozileta pamoja ujumbe wa pamoja wa Afrika na Umoja wa Maitafa huko Darfur, UNAMID na ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Sudan, UNCT umejadili kwa kina njia bora ya kuupa msukumo mpango wa amani katika jimbo la Darfu uliosaniwa Doha, baina ya serikali na kundi la waasi . Mkutano huo umeangazia njia zinazoweza kusaidia [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mashabiki wa mitindo ya mavazi na washiriki wa michezo ya bahati nasibu kwenye Intaneti wamebuni mchakato mpya wa kulisaidia Shirika la Mpango wa Chakula, (WFP) katika operesheni zake za dharura nchini Syria. Mchakato huo utaambatana na mchezo wa Stylista kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, ambao ulibuniwa na kampuni ya dijitali ya Sandbox Global, yenye [...]
21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kazi duniani, ILO nchini Kenya na taasisi ya kuwezesha wanawake nchini humo, Kenya Women Finance Trust wameibuka na mradi wa kusaidia kuhifadhi mazingira na wakati huo huo kuinua kipato cha wanawake. Mradi huo wa miaka miwili utakaoanza mwezi Aprili mwaka huu unalenga kuwapatia mikopo wanawake vijana ili waweze kununua taa aina ya kandili [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia kiongozi mshirika wa shirika la Maendeleo la Umoja huo UNDP Rebecca Grynspan ameanza ziara ya siku tatu nchini Burundi inayonuwia kuweka mikakati ya kuistaawisha nchi hiyo kimaendeleo baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Bi Grynspan mbali na kukutana na viongozi mbalimbali wa [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limewateua wanamuziki wawili maarufu kuwa mabalozi wake wema nchini Kenya. Susan Owiyo na Erick Wainaina wote kutoka Kenya wametangazwa rasmi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya. Susan Owiyo ameshashiriki kwenye tamasha mbali mbali za kimataifa kwenye miji maarufu duniani likiwemo tamasha [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Viongozi wa mataifa ya Afrika wametakiwa kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira katika kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazoshuhudiwa kwa sasa zikiwemo kuchafuka kwa hewa na athari za kemikali kwa afya na mazingira kwa mujibu wa ripoti ya mazingira iliyotolewa hii leo la Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano [...]
21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »