Nyumbani » 19/02/2013 Entries posted on “Febuari 19th, 2013”

Ban aelezea kusikitishwa na hatma ya wafungwa wa Kipalestina

Kusikiliza / Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na hali inayoendelea kuzorota ya wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa na mamlaka ya Israel, na ambao sasa wanafanya mgomo wa kutokula chakula. Taarifa ya msemaji wake imesema Bwana Ban, ambaye amesikitishwa zaidi na hali ya mfungwa Samer Issawi, amepokea barua kutoka kwa Rais Mohammud Abbas, na [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria haitaki misaada iingie kupitia mpaka wake na Uturuki: Amos

Kusikiliza / Mkuu wa OCHA, Bi. Valerie Amos

Umoja wa Mataifa umesema mgao wa hivi karibuni wa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani nchini Syria haukuweza kuwafikia wale wote wanaohitaji kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valeri Amos ametoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Liberia yahitaji dola Milioni 37 kukidhi mahitaji ya kibinadamu 2013

Kusikiliza / Wakimbizi nchini Liberia

Serikali ya Liberia na Umoja wa Mataifa hii leo wametangaza ombi la dola Milioni 37 zitakazotumika kukidhi mahitaji ya binadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2013 kutokana na hali ngumu inayoendelea kukabili wananchi. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari kuwa Liberia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu ambapo [...]

19/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia waliouawa katika mzozo wa Afghanistan ilipungua 2012: UNAMA

Kusikiliza / Wananchi wa Afghanistan

Ripoti mpya ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) imeonyesha kushuka kwa idadi ya raia walouawa katika mapigano kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita. Ripoti hiyo kuhusu ulinzi wa raia katika mizozo ya silaha, na ambayo imeandaliwa na UNAMA kwa ushirikiano na Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa [...]

19/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Si sahihi mahakama ya kijeshi kutumika kuhukumu raia: Pillay

Kusikiliza / Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya UM, Navi Pillay

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema imesikitishwa na kitendo cha Sahara Magharibi kutumia mahakama za kijeshi kuendesha kesi zinazowahusu raia ikisema kuwa hatua hiyo uvunjifu wa haki za binadamu. Mamlaka katika eneo la Sahara Magharibi imeripotiwa, kuwatia hatiani raia 25 kwa kutumia mahakama za kijeshi. Mahakama hiyo ya kijeshi ambayo [...]

19/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM yaweka bayana athari za mazingira kwa mfumo wa endokrini

Kusikiliza / UNEP

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa matumizi ya kemikali ambazo hazifanyiwa uchunguzi  zinaweza kuleta hitalafu katika mwili wa binadamu ikiwemo kuvuruga mfumo wa homoni. Ripoti hiyo ambayo pia imeandaliwa kwa pamoja pia na shirika la afya ulimwenguni WHO imekariri mfumo wa kisanyansi unaojulikana Endokrine ambayo ni mahsusi kwa [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakosoa muswada unaobinya uhuru wa kuandamana Misri

Kusikiliza / Waandamanaji nchini Misri

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekosoa hatua ya upitishwaji wa muswada wa sheria inayobinya uhuru wa watu kufanya maandamano iliyoungwa mkono na baraza la mawaziri wa  nchi hiyo. Pillay amesema kitendo hicho hakifungamani na misingi inayolinda na kutetea haki za binadamu. Amesema kuwa pamoja na ukweli kwamba uhuru wa [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani mashambulio ya kigaidi ya karibuni Somalia

Kusikiliza / Balozi Augustine Mahiga, Mkuu wa UNPOS

Ofisi ya masuala ya kisiasa kuhusu Somalia katika Umoja wa Mataifa (UNPOS), imelaani mashambulizi ya kigaidi ambayo yametekelezwa nchini Somalia katika kipindi cha wiki mbili za kwanza mwezi Februari mwaka 2013, pamoja na kuuawa kwa msomi maarufu wa Kiislamu, Sheikh Abdiqadir “Ga’amey” Nur Farah, kule Garowe.   Mauaji ya Dkt. Nur Farah yametendeka baada ya [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira na chakula waendelea Nairobi

Kusikiliza / Chakula kilichotupwa

Suala la utupaji wa chakula ni moja ya ajenda kuu zinazozungumziwa mwenye mkutano wa kimataifa unaowaleta pamoja mawaziri wa mazingira kutoka pembe zote za ulimwengu ambao kwa sasa umeingia siku yake ya pili mjini Nairobi nchi Kenya. Inakadiriwa kuwa kiasi cha tani Bilioni 1.3 za chakula hutupwa kila mwaka duniani ambapo asilimia kubwa hupotea wakati [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan kutekeleza mfumo wa breki za gari wa kuzuia ajali barabarani

Kusikiliza / Usalama barabarani

Taifa la Japan mwezi huu litaanza kutekeleza hatua ya kuhakikisha usalama kwenye malori na mabasi kuambatana na kanuni nambari 13 ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya UNECE kuhusu mfumo maalum wa breki za magari ikiwa ndiyo nchi ya 43 kutekeleza kanuni hiyo. Tume hiyo inasema kuwa kuanza kutumika kwa kanuni hiyo [...]

19/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali yausalama bado kikwazo katika usambazaji misaada Syria:WFP

Kusikiliza / Mgao wa wa chakula kwa wakimbizi

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema licha ya kwamba limeshiriki kwenye operesheni ya pamoja ya mashirika Umoja huo ya kusambaza misaada kwa wakimbizi walioko kambi ya Karameh nchini Syria, bado hali ya usalama si nzuri. WFP imesema operesheni hiyo ya tarehe 16 mwezi huu katika mkoa wa Idleb kaskazini Magharibi [...]

19/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031