Nyumbani » 15/02/2013
Entries posted on “Febuari 15th, 2013”
Kusikiliza /

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo kuhusu Yemen ambayo pamoja na kupongeza tangazo la kuwepo kwa mjadala wa kitaifa nchini humo baadaye mwezi huu inaonya wale wote wanaokwamisha mchakato wa mpito nchini humo akiwemo Rais wa zamani Ali Abdullah Salehe. Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan Kusini, UNMISS Hilde Johnson amesema mwaka mmoja na nusu wa taifa la nchi hiyo umekumbwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu. Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa, Bi. Johnson ambaye pia ni [...]
15/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa Februari dunia iliadhimisha siku ya Radio duniani. Siku hii hutoa fursa kwa radio za kimataifa, kitaifa na za kijamii kutathmini shughuli zao za kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Mathalani mchango wa Radio katika ukombozi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii na hata usalama wa waandishi wa habari. Radio imebuniwa zaidi [...]
15/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameonyesha wasiwasi juu ya hali ya kisiasa huko Maldives na hatma ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ambaye kwa sasa ameomba hifadhi kwenye ubalozi wa India nchini humo. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akipendekeza pande zote zinazovutana zijizuie kufanya vurugu na badala yake [...]
15/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Utafiti uliofanywa na Shirika la Uhamiaji Duniani (IOM) unaonyesha kuwa asilimia 93 ya jamii zilizotimuliwa kutoka maeneo ya kaskazini mwa Mali na ambazo sasa zinaishi katika mji mkuu Bamako na mji jirani Koulikoro zinataka kurejea nyumbani mara tu hali ya usalama na ya kiuchumi itapoimarika. Utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu mapema mwezi huu [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Huku hali ya usalama nchini Mali ikibaki kuwa tete, Ofisi ya Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imesema inawatuma wataalamu wa haki za binadamu kuchunguza hali ilivyo nchini humo. Wataalamu watatu ambao tayari wamewasili mjini Bamako watachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, yakiwemo madai ya ulipizaji kisasi. Cécile Pouilly [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Tathmini iliyofanywa na Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu usalama wa chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), imeonyesha kuwa mizozo ya kisiasa na kijeshi kati ya mwezi Disemba mwaka 2012 na mwezi Januari mwaka huu, huenda ikatumbukiza nchi hiyo kwenye baa la ukosefu wa chakula. Maeneo mengi yaliyoshikiliwa na muungano [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema msimu wa upanzi unakaribia huko Mali lakini kuna wasiwasi kutokana na jinsi ya kurejesha wakulima kwenye maeneo yao baada ya kukimbia mapigano yaliyoanzia kaskazini mwa nchi hiyo. Hali hiyo ndiyo ilimsukuma Mkurugenzi wa Shirika la mpango wa chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva kuwa na [...]
15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya dharura kwa mamia ya watu waliokumbwa na mafuriko katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na maeneo mengine ya jirani na kusababisha kiasi cha watu 98,000 kupoteza makazi yao na wengine 560,000 kuwa katika hali ya shida na taabu. IOM kwa [...]
15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Marekani iendelee kuongoza katika kukabiliana na changamoto nyingi za kikanda na za kimataifa, wito ambao ametoa wakati wa ziara yake mjini Washington, ambako amekutana na kufanya mashauriano na Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry. Viongozi hao wawili wamejadili [...]
15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Viongozi wa takwimu za masuala ya afya waliokutana mjini Geneva, Uswisi kujadili ushirikiano wa siku za usoni katika kuboresha mbinu za makadirio ya takwimu kuhusu masuala ya afya wamehitimisha mkutano kwa kukubaliana uwekezaji zaidi katika sekta hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na shirika la afya duniani, WHO ambapo mathalani washiriki wamesema zaidi ya nchi 100 hazina [...]
15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesafirisha kwa ndege vyakula kwa ajili ya maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kwenye mji wa Punia ulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC. WFP imesema usambazaji wa biskuti zenye lishe bora unatarajiwa kung'oa nanga hapo kesho. Shirika hilo limesema mvua kubwa zinazonyesha zimelazimu watumie [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »
Kusikiliza /

Shirika la kudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi huko Sudan Kusini waliokufa kutokana na ugonjwa wa ini aina ya E, au Hepatitis E imeongezeka na kufikia zaidi ya 111 tangu mwezi Julai mwaka jana. UNHCR imesema idadi ya walioambukizwa nayo imefikia zaidi ya Elfu sita na takwimu hizo zilikusanywa na shirika la afya [...]
15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »