Nyumbani » 14/02/2013 Entries posted on “Febuari 14th, 2013”

Burundi yapaza sauti kutetea wanawake

Kusikiliza / Wanawake Burundi

Burundi nayo imejumuika na mataifa mengine katika kampeni hiyo ambapo SERUKA ambacho ni kituo pekee cha kupokea wanawake waathirika wa vitendo vya ukatili ikiwemo wa kingono na majumbani kilikuwa mstari wa mbele. Mmoja wa washiriki ni Yvone kutoka eneo la Songa mjini Bujumbura. (SAUTI YVONE) Kwa upande wake Lysie ambaye naye alikuwepo kwenye kituo hicho [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na waziri mpya wa mambo ya nje Marekani, John Kerry

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry. Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Marekani, Bwana Ban amempongeza Bwana Kerry kwa uteuzi wake katika wadhfa huo, na kumsifu kwa ushirikiano wake kuhusu masuala mengi, yakiwemo ya kisiasa, usalama [...]

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hafla ya madhehebu ya dini kuungana kwa ajili ya amani yafanyika kwenye UM

Kusikiliza / Vuk Jeremic

Hafla maalum imefanyika leo kwenye makao makuu ya UM mjini New York, kuadhimisha kuanza kwa wiki moja ya Ushirikiano wa dini mbalimbali duniani, kama ilivyotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika azimio namba 65/5. Hafla hiyo yenye kauli mbiu, "Kuungana kwa ajili ya desturi ya amani kupitia ushirikiano wa dini" imeandaliwa na afisi [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wa vijana wakamilika Nairobi

Kusikiliza / Amina Mohammed, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP akizungumza na vijana kwenye mkutano wa TUNZA

Mkutano wa kimataifa wa vijana ambao umedumu kwa muda wa juma moja umekamilika kwenye makao  ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi nchini Kenya. Washiriki walijadili masuala ya chakula na mazingira ikiwemo utupaji wa chakula wakati watu wengi wana uhaba wa chakula. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (SAUTI JASON)

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Makao Makuu ya UNPOS sasa kuhamia Mogadishu ili kuimarisha usaidizi wake

Kusikiliza / Tayé-Brook Zerihoun, Naibu mkuu wa Ofisi ya masuala ya siasa ya UM akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Somalia

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepokea na kuridhia ripoti ya Katibu Mkuu  Ban Ki-Moon kuhusu hali ilivyo nchini Somalia ambayo pamoja na mambo mengine imependekeza kuhamisha ofisi ya Umoja huo kuhusu Somalia, UNPOS kutoka Nairobi, Kenya kwenda Mogadishu. Ripoti hiyo iliwasilishwa na Tayé-Brook Zerihoun ambaye alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa [...]

14/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu hazitambui mpaka: Pillay

Kusikiliza / Navi Pillay

  Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navi Pillay, amesisitiza haja ya kuingilia kati kutafutia ufumbuzi mambo yanayohusu haki za za binadamu kwenye eneo la Trinistran huko barani Ulaya, kufuatia ripoti moja iliyochapishwa leo kuhusu haki za binadamu kwenye eneo hilo. Akisisitiza juu ya hilo, Pillay amesema kuwa suala la haki [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu waendelea kulazimika kuhama licha ya waasi wa FARC Colombia kusitisha mapigano: OCHA

Kusikiliza / colombia_farc

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, imesema kuwa licha ya idadi ya mashambulizi kupungua, idadi ya watu wanaolazimika kuahama makwao nchini Colombia bado inaendelea kupanda kwa sababu makundi yenye silaha bado yanafanya mashambulizi. Mashambulizi ya kundi lenye silaha la FARC yalishuka kwa asilimia 73 katika kipindi cha miezi miwili ya [...]

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN-Habitat yazindua ripoti kuhusu ukuaji wa miji

Kusikiliza / unhabitat-1

Ripoti mpya ya Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, imesema kuwa watunga sera na wadau katika masuala ya maendeleo wanatakiwa kuzingatia ukuaji na maendeleo jumuishi zaidi. Ripoti hiyo iitwayo, “Hali ya miji ya dunia mwaka 2012/2013,” na ambayo inahusu ukuaji wa miji, inasema kuna haja ya kuzingatia ukuaji unaozidi ukuaji wa kiuchumi tu, [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Chanjo dhidi ya homa ya manjano kuanza Chad: WHO

Kusikiliza / homa ya manjano

Wizara ya Afya nchini Chad imepanga kuanza chanjo ya dharura ya jumla dhidi ya homa ya manjano, kufuatia kuthibitishwa kwa visa viwili vya maambukizi ya homa hiyo mnamo Disemba mwaka 2012. Kampeni hiyo ya chanjo itafanyika katika wilaya tatu zinazopakana na eneo la Darfur nchini Sudan, ambako visa vya homa ya manjano vilikuwa vimeripotiwa awali, [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi Mogadishu wahamishiwa makazi mapya: UM

Kusikiliza / Mtoto akiwa ndani ya moja ya kibanda ambacho ni makazi yao huko Somalia

Maisha duni ya wakimbizi wa ndani mjini Mogadishu Somalia yaliyodumu kwa takribani miongo miwili ya mzozo nchini humo sasa yameimarika kutokana na hatua zilizochukuliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Mashirika hayo 14 pamoja na mengine ya kiraia yalichukua hatua ya kuhamisha familia Elfu Tano za wakimbizi kwenda maeneo mapya mjini Mogadishu ambako makazi, malazi [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Paza sauti kutetea wanawake na watoto wa kike: Bachelet

Kusikiliza / Washiriki wa kampeni mjini Manilla, Ufilipino wakicheza muziki

Kataa ukatili wa majumbani, kataa ubakaji na uhalifu wa kingono. Huo ni ujumbe wa hii leo wa Mkuu wa shirika la masuala ya wanawake la Umoja wa Mataifa, UN-WOMEN  Michelle Bachelet inayofanyika duniani kote ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Kampeni hiyo ijulikanayo kama One billion rising inadhaminiwa na shirika la V-Day linaloongozwa [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031