Nyumbani » 11/02/2013 Entries posted on “Febuari 11th, 2013”

UM wasisitiza ushirikiano katika matumizi ya maji

Mwaka wa kimataifa wa ushirikiano wa matumizi ya maji

Umoja wa Mataifa umezindua rasmi mwaka wa kimataifa wa ushirikiano katika sekta ya maji, ikiwa ni fursa kwa nchi kushirikiana katika menejimenti ya rasilimali hiyo adhimu kwa amani na maendeleo ya wote. Katika ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema mwaka 2013 ni fursa kwa nchi zote kushirikiana kulinda na kutunza [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na Radio za kijamii

Wahariri wa habari wa Radio Kwizera wakiwa kazini

Siku ya Radio duniani tarehe 13 mwezi Februari hutoa fursa kwa mashirika ya utangazaji ya kimataifa na kitaifa pamoja na hata radio za kijamii kutathmini jukumu lao adhimu la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umekuwa ukifanya kazi kwa ushirikiano na radio hizo ambazo ziko karibu zaidi na jamii. Hutumia radio [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Ban azindua ziara rasmi za watoto ndani ya Makao Makuu ya UM

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiangalia kitabu na mmoja wa watoto walioshiriki ziara hiyo.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezindua rasmi ziara za watoto ndani ya Umoja huo mjini New York Marekani na kusema kuwa ziara za namna hiyo ni fursa ya kuelezea watoto jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi kuboresha maisha ya wakazi mbali mbali duniani na wao wataeneza taarifa hizo. Amewaeleza watoto hao [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Pope Benedict wa XVI

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Pope Benedict wa XVI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Benedict wa XVI tarehe 28 mwezi huu ambapo ametoa shukrani zake kutokana na mchango wa kiongozi huyo katika kuchagiza mashauriano baina ya waumini wa madhehebu mbali mbali duniani. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa [...]

11/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tega sikio kwa redio itangazayo amani, maendeleo na haki za binadamu: Ban

sg-withradio

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kila mmoja anafaa kuadhimisha Siku ya Redio Duniani kwa kusherehekea uwezo wa redio, na kushirikiana kuufanya ulimwengu uzingatie masafa yanayotangaza amani, maendeleo na haki za binadamu kwa wote. Katika ujumbe wake wa video, Bwana Ban amesema tangu kubuniwa kwake zaidi ya miaka 100 iliyopita, redio imekuwa [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

UNESCO yasaidia uandaaji wa mitaala ya uandishi wa habari Tanzania

Rose Haji, Mshauri na Mratibu wa Mafunzo kwa Radio Jamii, UNESCO, Tanzania katika moja ya mafunzo kwa waandishi wa habari

Moja ya sababu zinazowatia waandishi wa habari na watangazaji wa Radio hatarini wanapofanya kazi zao ni ukiukaji wa maadili. Waandishi wa habari na watangazaji baadhi yao kwa kukosa stadi sahihi hutangaza habari kupitia radio bila kuzifanyia utafiti au pengine za upande mmoja. Nchini Tanzania ukosefu wa maadili umeripotiwa kusababishwa pia na elimu isiyotosheleza inayotolewa na [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNDP ataka hatua za haraka dhidi ya magonjwa yaso ya kuambukiza

Jarida la Lancet Oncology

Msimamizi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, Helen Ckark, ametoa wito hatua thabiti na za haraka zichukuliwe ili kusitisha kuenea kwa magonjwa kama vile saratani na kisukari kote duniani, akisema kuwa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza daima yapo kwenye ajenda ya kimataifa maendeleo. Akizindua msururu wa machapisho katika jarida la masuala [...]

11/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO, IFAD zatiliana saini mpango wa kuwasaidia wakulima wadogowadogo

farming Africa

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametiliana saini ili kufanikisha mpango wa kuwapiga jeki wakulima wadogo wadogo na wale wanaoishi maeneo ya vijijini walioko katika nchi zinazoendelea. Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na lile la maendeleo ya kilimo, IFAD kwa pamoja yamekubaliana kutoa kiasi cha dola za Marekani 875,000 ili kuwaendeleza wakulima [...]

11/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa ngozi uenezwao kwa uchafu walipuka Syria

Watoto Syria

Ugonjwa wa ngozi uenezwao kutokana mazingira machafu, Leishmaniasis umeripotiwa kulipuka nchini Syria, ikiwa ni miezi kadha tangu kutolewa kwa onyo juu ya uwezekano wa kulipuka kwa ugonjwa huo. Visa 955 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwenye maeneo ya Hamah, Hassaka, Damascus na Homs nchini Syria. Shirika la afya duniani WHO limetoa huduma zikiwemo madawa na mahitaji [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

CERF yasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

Jennifer Topping (Picha-UM)

Mfuko mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, umetoa zaidi ya dola Milioni Tano kwa ajiliya wahanga wa mafuriko nchini Msumbiji. Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jennifer Topping amesema licha ya kwamba misaada ya awali ilikwishatolewa lakini bado kuna watu wenye mahitaji makubwa ya kibinadamu nchini Msumbiji. Amesema msaada [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake yaanza kikao Geneva

stopviolenceagainstwomen-300x294

Kamati inayohusiana na kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake imeanza kikao chake cha hamsini na nne leo mjini Geneva, Uswisi kwa kupokea ripoti za vikao vilivyotangulia na kuweka ajenda mpya. Kamati hiyo pia imemchagua Bi Nicole Amelie kutoka Ufaransa kama mwenyekiti wake mpya, huku wanawake wengine wawili, Violeta Neubauer kutoka mashariki mwa Ulaya na Pramila Patten [...]

11/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

SUDAN na kikundi cha JEM watiliana saini makubaliana ya kusitisha mapigano

darfur

Serikali ya Sudan na kikundi kikuu cha waasi huko Darfur, cha Justice and Equality Movement, JEM wametiliana saini mkataba wa kusitisha mapigano ambao tayari umeanza kutekelezwa. Utiaji saini huo uliofanyika Doha, umeshuhudiwa na Kaimu Mwakilishi wa kikundi cha pamoja na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMID Aichatou Mindaoudou na Naibu Waziri [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chad yaridhia mkataba unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia

vichwa vya nyuklia

Idadi ya nchi zilizoridhia mkataba wa kimataifa unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia imeongezeka na kufikia 159 baada ya Chad kuridhia mkataba huo. Katibu Mtendaji wa shirika la kuratibu usimamizi wa mkataba huo Tibor Tóth ameunga mkono hatua hiyo ambayo amesema inaimarisha msimamo wa Afrika wa kutokomeza majaribio ya nyuklia na hatimaye kufikia lengo la kuwa [...]

11/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira wang'oa nanga Nairobi

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira ukiendelea Nairobi, Kenya

Mkutano wa  kimataifa wa vijana wa juma moja kuhusu mazingira umeng'oa rasmi hii leo mjini Nairobi nchini Kenya mkutano ambao unawaleta pamoja zaidi ya vijana 800 kutoka pembe zote za dunia. Kongamano hilo lijukanalo kama TUNZA International Youth Conference on the Environment  linawaleta pamoja vijana kutoka karibu mataifa 100 kujadili hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031