Nyumbani » 07/02/2013 Entries posted on “Febuari 7th, 2013”

Radio ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule!

Kusikiliza / Wanawake Tanzania wafundishwa kutumia radio

Kuingia kwa zama za Televisheni kwa baadhi ya watu kulionekana kuwa mwanzo wa kuporomoka kwa usilizaji wa Radio. Lakini fikra hizo zimeonekana kuwa potofu kwa kuwa bado Radio inasikilizwa na watu wengi zaidi kuliko televisheni. Radio bado ina umuhimu wake na ndio maana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 13 Februari ya kila [...]

07/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Radio ya Umoja wa Mataifa enzi hizo

microphone

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa February, mamilioni ya watu duniani kote wanasherehekea siku ya Radio duniani. Tukio hili linalenga kuonyesha nguvu ya radio na umuhimu wa matangazo yake yanayofikia mamilioni ya watu kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Maadhimisho haya yanarejelea mwaka 1946 ambapo Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha radio yake yenyewe. [...]

07/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ijue Radio ya Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / un-radio-micro-historico

Radio ya Umoja wa Mataifa imetoka mbali, kuanzia mwaka 1946 ilipoanzishwa katika ofisi na studio za kuhama hama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Hapo ndio ilianza kurusha matangazo yake ya kwanza kabisa yakisema "Huu ni Umoja wa Mataifa ikiwaita wakazi wote wa dunia." Vipindi kama vile taarifa za habari na [...]

07/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Tamrat Samuel kama Mwakilishi wake Maalum Liberia

Kusikiliza / UNMIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametangaza uteuzi wa Bwana Tamrat Samuel kama naibu mwakilishi wake maalum wa masuala ya uongozi wa kisheria katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL). Bwana Samuel atamrithi Bwana Louis M. Aucoin kutoka Marekani, ambaye amehitimisha majukumu uake mnamo Disemba 2012. Bwana Ban ameelezea kufurahishwa [...]

07/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka haki itendeke Bangladesh kwa watuhumiwa wa uhalifu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Christof Heyns

Wataalamu huru wawili wa Umoja wa Mataifa wameonyesha wasiwasi wao vile ambavyo Bangladesh inasikiliza na kuhukumu watuhumiwa wa vitendo vya zamani vya uhalifu na wametaka haki itendeke. Wataalamu hao wa haki za binadamu Christof Heyns, na Gabriela Knaul wameonyesha wasiwasi wao kufuatia mwenendo wa mashauri yaliyotangulia ambapo watuhumiwa Abdul Kalam Azad alihukumiwa adhabu ya kifo [...]

07/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima Misri watarajia mabadiliko katika kilimo: ILO

Kusikiliza / Kilimo Misri

  Wakati msismko wa mapinduzi ya mwaka 2011 bado unahisiwa nchini Misri, wakulima wengi nchini humo wanatarajia kwamba sekta ya kilimo nayo itafikiwa na mabadiliko mazuri. Wakulima hao wanatarajia mabadiliko katika sheria, wakisaidiwa na Shirika la Ajira Duniani, ILO, ili biashara zao za kilimo ziwe na faida zaidi. Inatarajiwa kuwa hali hiyo itachangia kwa kiasi [...]

07/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha mazungumzo ya Kachin

Kusikiliza / KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha na kupongeza hatua ya kuwepo kwa mazungumzo yenye shabaha ya kutanzua mkwamo wa eneo la Kachin la China na Mynmar. Pande zote mbili zimetoa taarifa ya pamoja iliyoelezea namna zilivyodhamiria kuanzisha majadiliano ili kuepusha uwekekano wa kuzidisha machafuko katika jimbo la Kachin linalowaniwa na pande zote [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kusambaza ATM kwa wakimbizi wa Syria

Kusikiliza / Wakimbizi wa Syria

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limepanga kupanua huduma yake ya usambazaji wa misaada ya fedha kwa njia ya mashine zinazojiendesha yaani ATM kwa mamia ya wakimbizi wa Syria walioweka kambi kaskazini mwa Lebanon. UNHCR imesema kuwa hadi kufikia Marchi mwaka huu inaamini itakuwa imesambaza kadi za atm kwa zaidi ya [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi kwake

Mahamaka ya ICJ

Majaji wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, imeamuru kuwa serikali ya Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi katika serikali ya Muammar Gaddafi, Abdullah al-Senussi kwa mahakama hiyo mara moja. Serikali ya Libya bado inamshikilia pia mwanae Gaddafi, Seif al-Islam, na imekuwa ikisisitiza kwamba inapanga yenyewe kumshtaki na kumhukumu Bwana Senussi. Mapema wakati [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rushwa yagharimu Afghanistan dola Bilioni 3.9: UM

Huduma ya usafiri nchini Afghanistan

Afghanistan imetajwa kupiga hatua juu ya kukabiliana na vitendo vya rushwa katika ofisi za umma, lakini hata hivyo mafanikio hayo bado ni ya kiwango cha chini. Uchunguzi uliofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa umebaini kuwa pamoja na kuwepo kwa idadi  ndogo ya watu wanajihusisha na vitendo vya rushwa, lakini fedha zilizotokana na mwenendo huo [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemevu yabadilisha maisha: UNICEF

Utekelezaji wa mpango wa elimu jumuishi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema sera endelevu kuhusu elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu imekuwa na mafanikio makubwa katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki pamoja na Asia ya Kati. Hayo yamebainika katika kikao cha bodi ya utendaji ya UNICEF mjini New York, Marekani kilichojikita kwenye masuala ya watoto [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wafafanua matumizi ya vyombo visivyo na rubani huko DRC

Kusikiliza / Mkuu wa operesheni za Ulinzi wa amani za UM Hervé Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous ametolea ufafanuzi matumizi ya vyombo vya anga visivyo na rubani ambavyo umoja huo umependekeza vitumike kwenye maeneo hatari huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Bwana Ladsous amesema kuwa vyombo hivyo kimsingi ni sawa na kusema ni kamera zinazoruka angani ambazo [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031