Nyumbani » 06/02/2013 Entries posted on “Febuari 6th, 2013”

Wadhaniao huduma za posta zinakufa wanaota ndoto ya mchana: UPU

Kusikiliza / Huduma za kusafirisha barua na vifurushi

Kadri maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yanavyozidi kuibuka, baadhi ya watu wamekuwa na hofu juu ya hatma ya huduma za posta, wakidhani kuwa matumizi ya barua pepe, simu za mkononi na hata utumaji wa pesa kwa mtandao ni hati ya kifo kwa huduma za posta. Mkurugenzi Mkuu wa muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU, [...]

06/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mawaziri kujadili masuala ya mazingira Nairobi: UNEP

Kusikiliza / UNEP_logo-298x300

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) wiki ijayo litakuwa na mjadala kuhusu masuala ya habari wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Uongozi la UNEP mjini Nairobi, Kenya. Zaidi ya mawaziri 200 wa mazingira, wajumbe wa ngazi za juu, wakiwemo wanasayansi, wachumi, watunga sera, mashirika ya kiraia na viongozi wa biashara wanatarajiwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoendelea zakumbwa na gharama kubwa zaidi katika biashara: ESCAP/Benki ya Dunia

Kusikiliza / Kilimo cha kutumia maksai nchini Ethiopia

Ingawa uchumi wa kimataifa umepata sura ya kujumuisha wote, takwimu mpya zilizoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya Asia na Pasifiki, (ESCAP) na Benki ya Dunia, zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea ndizo zinazobeba mzigo mkubwa zaidi wa gharama ya kufanya biashara. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa licha ya [...]

06/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Teknolojia ya mawasiliano yaimarisha huduma za posta: UPU

Kusikiliza / Vifurushi

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU Bishar Hussein amesema kadri teknolojia ya mawasiliano inavyoimarika ndivyo ilivyo kwa huduma za posta na hivyo changamoto ni kwa mashirika ya posta duniani kuwa na ubunifu zaidi ili yaweze kwenda na wakati. Bwana Hussein ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani mauaji ya mtetezi wa haki za binadamu nchini Tunisia

Kusikiliza / Navi Pillay

  Kamishina Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani mauaji ya Katibu Mkuu wa kikundi cha vuguvugu la wazalendo nchini Tunisia, DPM, Chakri Belaid. Pillay amesema amehuzunishwa na taarifa za kifo cha Belaid ambaye alikuwa mtetesi mkubwa wa haki za binadamu na akipinga vurugu za kisiasana kueleza kuwa kifo chake [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yataja changamoto za kukabiliana na ukeketaji wanawake na watoto wa kike

Kusikiliza / Kampeni ya kutokomeza ukeketaji wanawake na watoto kike nchini Uganda

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Idadi ya watu duniani, UNFPA, Dkt. Babatunde Osotimehin amesema licha ya mafanikio katika kupambana na ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, bado kuna changamoto kubwa kutokomeza kabisa tabia hiyo. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Babatunde ametaja changamoto hiyo kuwa ni ajira mbadala kwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatari ya watoto wa kike kukeketwa yapungua, Kenya yatajwa kuwa mfano: Ripoti UM

Kusikiliza / Watoto wa kike

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo, siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, imesema kuwa hatari ya watoto wa kike kukeketwa imepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa zamani. Ripoti hiyo ya mashirika ya Umoja wa mataifa ya UNICEF linalohusika na watoto na UNFPA la idadi watu, imesema katika nchi 29 [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zaongezeka kutokana na kuwepo usalama nchini Somalia

Kusikiliza / Somalia health

Baada ya kuimarika kwa usalama baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kuikimbia miji ya kusini na kati kati mwa Somalia mashirika ya kutoa misaada sasa yameongeza huduma za kiafya na huduma zingine za dharura katika maeneo ambayo awali ilikuwa vigumu kuyafikia. Mratibu wa masuala ya dharura kwenye shirika la afya duniani WHO nchini Somalia Omar Saleh [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Jim wajadili malengo ya maendeleo ya milenia

Kusikiliza / Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim ambapo wameangalia upya fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili hizo hususan kwenye maeneo ya nchi za Maziwa Makuu barani Afrika. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Bwana [...]

06/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ushirikishaji jamii dhidi ya ukeketaji ndio siri ya mafanikio: Babatounde

Kusikiliza / Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na mangariba wa jamii ya Bondo nchini Sierra Leone

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA, Dkt. Babatunde Osotimehin amesema siri ya mafanikio ya vita dhidi ya ukeketaji wanawake na watoto wa kike ni ushirikishaji wa dhati wa jamii husika. Dkt. Osotimehin ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031