Nyumbani » 01/02/2013 Entries posted on “Febuari 1st, 2013”

Waliotumia madawa ya kulevya na harakati za kujikomboa

Kusikiliza / UNODC_DRUGS

Madawa ya kulevya yameendelea kuwa tishio siyo tu kwa uchumi wa nchi kwa kuwa vijana wanatumbukia katika lindi hilo na kushindwa kufanya kazi, bali pia kijamii kwa kuwa waathirika wa madawa hayo wanashindwa kufanya kazi na hata kuleta mizozo ya kijamii ndani ya familia na jamii zao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kupambana [...]

01/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

Kusikiliza / radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

01/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mkakati mpana wahitajika kudhibiti kauli za chuki: Dieng

Kusikiliza / Adama Dieng, Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuzuia mauaji ya kimbari.

Harakati zozote za kudhibiti kauli chochezi na za chuki zinazoweza kusababisha migogoro zinahitaji mpango mpana unaojumuisha pande nyingi. Hiyo ni kauli ya Adama Dieng, Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuzuia mauaji ya kimbari, kauli ambayo ameitoa wakati wa mkutano wa kujadili suala hilo mjini New York, Marekani. Dieng amesema hilo ni [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kila 1 kati ya nchi 2 duniani hazipo tayari kuzuia na kutibu saratani: WHO

Kusikiliza / 2cancer_jpeg

Zaidi ya nusu ya nchi kote duniani hazina uwezo wa kuzuia na kutoa matibabu dhidi ya saratani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani, WHO. Shirika hilo limesema nyingi ya nchi hizi hazina mpango tekelezi wa kudhibiti kansa, ambao unajumuisha kuzuia, kugundua mapema, kutibu na huduma za uuguzi. WHO inasema kuna haja [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uendeshaji wa kesi ya ubakaji Somalia inatia wasiwasi: UNPOS

Kusikiliza / somalia-map1

Kuhusu maswala ya haki nchini Somalia, Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kisiasa nchini Somalia (UNPOS), imeelezea wasiwasi wake kuhusu jinsi kesi inayohusu madai ya ubakaji dhidi ya mwanamke mmoja wa Kisomali inavyoendeshwa. Watu watano wameshtakiwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa na polisi ikisema kuwa habari zilizochapishwa kuhusu madai ya ubakaji huo, zilikuwa za [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na UNDP washirikiana kuwasaidia wahamiaji wa Chad

Kusikiliza / Safari ya kutoka Ufaransa kurejea Chad

Shirika la wahamiaji duniani  IOM na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa wametia saini mkataba wa kutekeleza programu ya kusaidia wahamiaji wa Chad walio Ufaransa, na ambao wana kiasi kikubwa cha ujuzi na maarifa,  kurudi nyumbani ili kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amezungumza na Radio ya Umoja [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge la Urusi litupilie mbali muswada wa propaganda za ushoga.

Kusikiliza / homophobia1

Kundi la wataalamu huru wa masuala ya haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa bunge la Urusi kutupilia mswada  ambao utaidhinisha kutolewa kwa adabu kwa propaganda zozote zinazohusu ushoga kwa watoto. Wataalamu hao wanaonya kuwa mswada huo utakandamiza haki za binadamu nchini Urusi na kuwalenga zaidi walio mashoga , wasagaji na wale [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM yuko Burundi kwa ziara ya siku mbili

Kusikiliza / Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman  amewasili nchini Burundi kwa ziara ya siku mbili. Afisa huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na wawakilishi wa vyama vya kisiasa. Tayari Bwana Feltman amekuwa na mazungumzo hii  leo  na [...]

01/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto 210,000 mjini Homs wanahitaji msaada wa kibinadamu: UNICEF

Kusikiliza / Watoto wa Syria

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye mji wa Homs nchini Syria umegundua kuwa jumla ya watu 420,000 nusu yao wakiwa ni watoto wanahitaji msaada wa dharura. Shughuli hiyo ya mwezi mzima ambayo tayari imekamilika iligundua kuwa  karibu watu 700,000 kwenye mji huo waliathiriwa na mzozo ulishuhuhudiwa wakiwemo watu 635,000 waliolazimika kuhama makwao. Watoto ndio walioathirika [...]

01/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yahofia usalama wa wafilipino waliobakia Syria

Kusikiliza / Baadhi ya wafilipino waliorejea nyumbani kutoka Syria

Usalama wa raia wa Ufilipino ambao bado wamebakia Syria baada ya wenzao kuanza kurejea makwao unatia hofu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM. Mratibu wa IOM nchini Syria Othman Belbesi amesema kuwa idadi kubwa ya raia hao wameshindwa kuondoka kutokana  na kutojua namna watavyoondoka. Baadhi yao wanadaiwa kukwama katika maeneo ambayo siyo [...]

01/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu nchini Somalia yaimarika

Kusikiliza / Stefano Porretti

Kaimu mratibu wa Umoja wa Mataifa juu ya shughuli za misaada ya kibinadamu nchini Somalia Stefano Porretti, amepongeza maendeleo makubwa yaliyofikiwa nchini humo na kusifia kitendo cha kuwakwamua wananchi waliotumbukia kwenye mzozo ambao sasa wamepungua hadi kufikia milioni 1.05. Hata hivyo afisa huyo ameonya kuwa mafanikio hayo yanaweza kuporomoka kama kutakosekana mipango endelevu. Amesema tangazo la [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatimaye msafara wa UNHCR waingia kaskazini mwa Syria

Kusikiliza / Watoto wakipokea misaada eneo la Azza

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, kwa mara ya kwanza limefaulu kusambaza vifaa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya baridi kwa wakimbizi wa ndani wa Syria waliotawanyika katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo. Vifaa hivyo ni pamoja na mahema, mablanketi ambapo usambazaji wa huduma hizo ulifanyika kwa ufanisi mkubwa na [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro unaoendelea Syria waibua ugonjwa wa ngozi

Kusikiliza / Taka zikiwa zimesambaa eneo moja nchini Syria

Shirika la Afya duniani WHO limesema mzozo unaoendelea nchini Syria unaendelea kusababisha uhaba wa dawa muhimu kama vile vile nusu kaputi na dawa za kuondoa maambukizi mwilini pamoja na kuibuka kwa magonjwa ya ngozi. WHO inasema maduka ya dawa nchini Syria yanazidi kukosa uwezo wa kutoa dawa za msingi kama vile zile za kutuliza maumivu [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031