Nyumbani » 28/02/2013 Entries posted on “Febuari, 2013”

Juhudi zaidi zahitajika kutimiza malengo ya Milenia

MDGS

Imeelezwa kwamba mipango ya maendeleo ya sasa duniani lazima ijikite katika njia bora zenye uwiano wa kutimiza malengo ya Millenia yanayofikia kikomo mwaka 2015. Akitoa hutuba ya ufunguzi wakati wa kongamano lililopewa jina Tendea kazi malengo ya Milenia,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo UNDP amesema changamoto za uchumi kama vila upatikanaji [...]

28/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Global Fund yazindua utaratibu mpya wa kutoa ufadhili

Global Fund

Mfuko wa Kimataifa wa Kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria, Global Fund, umezindua utaratibu mpya wa kufadhili mapambano hayo, ambao utawahusisha wadau wote kikamilifu. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko huo, utaratibu huo mpya wa kutoa ufadhili utasaidia taasisi anayoiongoza kuwafikia walengwa ambao ni watu walioathirika na Ukimwi, Kifua kikuu na malaria. Kiasi [...]

28/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wataalamu wa UM wataka uchunguzi kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu Korea Kaskazini

Bendera ya Korea Kaskazini

Kundi la wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu limesema kuwa, kuna haja ya kutambua na kuweka msukumo juu ya utekelezwaji wa mapendekezo ya kuendesha uchunguzi, ili kubaini tuhuma za ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Korea ya Kaskazini. Kundi hilo limesisitiza haja ya kuendesha uchunguzi huo ili kubainisha ukweli wa mambo, [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatari ya saratani ipo juu tu kwenye maeneo yaloathiriwa na ajali ya nyuklia Fukushima: WHO

kiwanda cha Fukushima

Uchunguzi wa kina uliofanywa na wataalam wa kimataifa kuhusu hatari za kiafya kutokana na ajali ya kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Fukushima Daiichi nchini Janapan, umebaini kuwa hatari zilizotarajiwa kwa ujumla ndani na nje ya Japan zipo chini, na kwamba hakuna dalili zozote za kuongezeka viwango vya hatari hizo kuzidi viwango vya kawaida. Hata [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wananchi katika jimbo la Jonglei Sudan Kusini wanaishi katika uoga: OCHA

Toby Lanzer

Mratibu wa masuala ya kibinadamu katika Sudan Kusini, Toby Lanzer, ametoa wito kwa serikali ya Sudan Kusini kuongeza nguvu juhudi zake za kuimarisha utiivu wa sheria na utaratibu, na kuwafikisha mbele ya sheria wale wote wanaotenda uhalifu na kuweka maisha ya watu hatarini. Ametoa wito kwa makundi yote yenye silaha kuhakikisha ya kwamba raia hawalengwi [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kumaliza ugonjwa wa ukimwi ni suala la haki za binadamu:UNAIDS

nemba ya UNAIDS

Mkurugernzi mkuu wa programu ya pamoja ya Umoja wa Mataifa ya kupambana na virusi vya HIV na ugonjwa wa ukimwi UNAIDS, Michel Sidibe, amesema kuwa kumaliza tatizo la ugonjwa wa ukimwi ni haki ya binadamu kwa wote. Akihutubia baraza la haki za binadamu la  Umoja wa Mataifa juu ya suala la kutokuwepo usawa katika jitihada [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ukabila na udini tishio kwa amani duniani: Dieng

Adama Dieng

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa limehadharishwa kwamba  ongezekeo la uhasama wa vikundi vya kidini na kikabila katika nchi kadhaa linaweza kuchochea ghasia katika nchi hizo. Akihutubia baraza hilo katika mkutano wa 22 unaoendelea, Mshauri maalum wa Katibu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mauaji ya kimbari Adam Dieng amesema nchi zinazokabiliwa na [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mataifa yaanza kupiga hatua kukabiliana na uvuvi haramu

fisheries1

Hatimaye mataifa mbalimbali duniani yameanza kupiga kahatua kuridhia mpango wenye shabaha ya kukabiliana na wimbi la uvuvi haramu ambao unafanywa bila kuzingatia vigezo vya kimataifa na hatua hiyo inafuatia majadiliano yaliyofanywa kwa miaka kadhaa. Vitendo vya uvuvi haramu ambavyo vimekithiri katika maeneo mbalimbali vinatajwa kusababisha uharibifu wa viumbe hai pamoja na uoto wake wa asili. [...]

28/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNICEF yakomboa shule ziliizoteketezwa na kimbunga Madagascar

Watoto wa shule Madagascar

MADAGASCAR! Kisiwa ndani ya bahari ya HINDI kilichoko Kusini Mashariki mwa Afrika chenye idadi ya watu  zaidi ya milioni 22. Kisiwa hiki kimekuwa kikikumbwa na vimbunga mara kadhaa! Vimbunga hivi vimekuwa vikiathiri sekta  mbalimbali za kiuchumi na kijamii. Leo katika makala tunamulika namna ambavyo vimbunga hivi vimeathiri sekta ya kilimo chini Madgascar na mchango wa [...]

27/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNRWA yalaani mauaji ya watoto wa Kipalestina nchini Syria

kambi ya yarmouk mjini Damascus

Shirika la Umoja wa Mataifa linalowasaidia Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limelaaani shambulizi lililofanywa nchini Syria likiwalenga watoto wa Kipalestina ambao ni wanafunzi katika shule mbalimabli. Kwa mujibu wa Shirika hilo mashambulizi hayo mfululizo yaliyowalenga wakimbizi wa Kpalestina waishio Syria yamesababisha vifo vya watu wanne akiwamo  mototo mwenye umri wa miaka 14 aliyepata jeraha kichwani huku [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mamilioni ya watu kwa sasa wanakabiliwa na matizo ya kusikia duniani :WHO

Mtu mwenye tatizo la kusikia

Zaidi ya watu milioni 360 duniani wanakabiliwa na tatizo la kupoteza uwezo wa kusikia kwa mujibu wa makadirio yaliyotolewa na Shirika la afya duniani WHO kabla ya maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kulea sikio ambayo itadhimishwa tarehe tatu mwezi ujao wa Machi. Huku watu wakiendelea kupatwa na uzee duniani visa vya wao kukabiliwa na [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kuendelea kwa mapigano Syria ni baa la kibinadmu la nyakati za sasa

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremić.

Naye Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Vuk Jeremic, amesema ufanisi wa mazungumzo kuhusu ustaarabu utatokana na jinsi masuala mawili sugu Mashariki ya Kati yanatatuliwa, ambayo ni janga la umwagaji damu Syria na hatma ya watu wa Palestina. Akiongea kwenye kongamano hilo la nchi zinazoendeleza ustaarabu, Bwana Jeremic amesema, inasikitisha kuwa kwa takriban [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban ahimiza ustahmilivu na heshima kupunguza migawanyo na migogoro

ban kwenye kongamano la Alliance of Civilzations, Vienna, Austria

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema viongozi kote duniani, wawe wa kimataifa au kimataifa, wanafaa kuongea lugha ya kustahmiliana na heshima, na kujitenga na migawanyo na kuharibiana sifa. Akiongea kwenye kongamano la muungano wa nchi zinazoendeleza ustaarabu linalofanyika mjini Vienna, Austria, Bwana Ban amesema masuluhu ya kudumu kwa migawanyiko yanaweza tu kutokana [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Zaidi ya watu bilioni 1 wanaishi katika nchi zenye migogoro duniani: ESCAP

Noeleen Heyzer

Wakati malengo ya Millenia yakikaribia kufikia kikomo chake mwaka 2015,zaidi ya watu bilioni moja na nusu wanaishi katika mizozo mbalimbali nchini mwao. Akifungua konagamano katika mji mkuu wa Timor kuhusu maendeleo ya kimataifa Kwa mujibuwa Msaidizi wa Katibu Mkuu wa umoja wa Mataifa aliye pia Katibu  wa Tume ya maswala ya Uchumi na Kijamii kwenye [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa Shirika la Uhamiaji (IOM) wakamilika nchini Tanzania

iom logo

Shirika la Kimataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limehitimisha mkutano wake wa siku tatu nchini Tanzania uliowajumuisha maofisa wa uhamiaji kutoka baadhi ya nchi wanachama wa jumuiya ya maendeleo kusini mwa Afrika SADC, na kuanisha vipaumbele vinavyopaswa kuzingatiwa ili kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu. George Njogopa na taarifa zaidi. Maafisa hao uhamiaji wamejadilia haja ya [...]

27/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuendeleza mazingira safi hakupotezi nafasi za ajira: ILO

peter poschin

Mratibu wa progamu ya ajira ya shirika la kazi duniani ILO Peter Poschen ameonya juu ya uwezekano wan chi zilizoendelea kukubwa na tatizo la tabia nchi kama zitaendelea kupuuza kuchukua hatua kuunga mkono kampeni ya inayohimiza uchumi unaojali mazingira. Mtaalamu huyo amesema iwapo dunia itazingatia na kuweka sera sahihi na kuzitekeleza kwa vitendo, kunaweza kushuhudia [...]

27/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNAIDS na UNDP zaunga mkono pendekezo la kusaidia nchi maskini kuendeleza na kuongeza ugawaji wa dawa muhimu

unaids

Shirika linalohusika na masuala ya HIV na UKIMWI, UNAIDS na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa, UNDP, leo yamezindua chapisho jipya linaosema kwamba kushindwa kupanua kipindi cha mpito kwa nchi maskini ili ziweze kuhitimu matakwa ya mkataba kuhusu masuala ya kibiashara yanayohusiana na haki miliki (TRIPS), huenda kukazuia uwezo wa watu kupata [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

UNICEF na washirika wakomboa watoto kutoka ajira migodini huko DRC

Watoto wakitafuta madini huko DRC

Ajira kwa watoto watoto ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazokabili nchi zinazoendelea. Katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC hali ni mbaya zaidi. Nchini humo sio ajabu kuwaona  watoto wenye umri wa kwenda shule wakifanya kazi za kujipatia kipato ambazo hata hivyo huwaingizia kipato kidogo  ikilinganishwa na kazi wanazofanya. Mwenzangu JOSEPH MSAMI anamulika [...]

26/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaelezea kushtushwa na mauaji ya watoto 70 kwa makombora Aleppo

maria calivis unicef

Shirika la Kuhudumia Watoto katika Umoja wa Mataifa, UNICEF, limeelezea kushtushwa na ripoti za mauaji ya watoto 70 katika shambulizi la makombora katika maeneo ya makazi mjini Aleppo, Syria, mnamo tarehe 18 na 22 Februari. Katika taairfa yake, Mkurugenzi wa UNICEF katika katika kanda ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika, Maria Calivis, amesema [...]

26/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mzozo wa Mali umesambaratisha elimu na riziki za watu: OCHA

John Ging

Mkuu wa operesheni za Afisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) Bwana John Ging, amesema kuwa madhara ya mzozo wa Mali ni makubwa mno, mzozo huo ukiwa umeathiri shughuli zote za maisha.  . Bwana Ging amewaambia waandishi wa habari mjini New York kuwa katika ziara yake nchini Mali, watu wengi wamesema [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lakutana kujadili hali Mashariki ya Kati

Jeffrey Feltman, akitoa taarifa mbele ya Baraza la Usalama la UM

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limekutana kujadili hali katika Mashariki ya Kati, likiwemo suala la Palestina. Akilihutubia baraza hilo, Naibu Katibu Mkuu anayehusika na masuala ya kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman amesema kuwa shambulizi la kombora dhidi ya Isarel kutoka Gaza linaonyesha hali kuwa tete kati ya Isarel na Palestina.  [...]

26/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Utulivu wa eneo la Afrika Magharibi watikiswa na wasafirishaji haramu: UM

Jalada la ripoti hiyo ya UNODC

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaonya kuwa usafirishaji wa madawa ya kulevya aina ya Cocaine, usafirishaji haramu wa binadamu na madawa bandia yanahatarisha utulivu wa nchi za Afrika Magharibi. Ripoti hiyo ya shirika la Umoja wa Mataifa linalodhibiti uhalifu na madawa ya kulevya, UNODC imesema kuwa mambo hayo yanayoendeshwa na magenge ya uhalifu ya [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kundi la wanawake 10 kupanda Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania:WFP

Kilele cha Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania

Kundi la wanawake saba raia wa Nepal ambalo lina sifa ya kuukwea mlima mrefu zaidi duniani  wa Everest na milima mingine barani Ulaya na nchini Australia sasa limeungana na wanawake wengine watatu wenye asili ya Afrika kuukwea mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Safari yao ya kuukwea mlima huo wenye urefu wa mita 5,895 itaanzia kwenye mji [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kenya fanyeni uchaguzi kwa amani epukeni ukimbizi wa ndani: UM

Bendera ya Kenya

Ikiwa imesalia siku Tano kabla ya uchaguzi mkuu nchini Kenya Umoja wa Mataifa umeitaka nchi hiyo kuchukua tahadhari juu ya uwezekano wa kutokea vurugu zinazoweza kusababisha wakimbizi wa ndani wakati wa mchakato mzima wa uchaguzi. Ujumbe huo umetolewa na Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu wakimbizi wa ndani Chaloka Beyani ambaye amesema historia ya [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Dola Milioni 45 zahitajika haraka kuokoa wanawake na watoto Mali: UNICEF

Wanawake nchini Mali wakiwa kwenye foleni wakisubiri watoto wao wapimwe afya

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetoa ombi la dharura la dola Milioni 45 kwa ajili ya kuwawezesha wanawake na watoto waliojikuta katikati ya mzozo nchini Mali kupata mahitaji ya kimsingi kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo.  UNICEF inasema kuwa athari za mzozo unaoendelea kwa watoto ni kubwa mno ikitaja suala la [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban atoa wito kwa vijana kuongoza katika kuendeleza amani na maendeleo

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema leo ya kwamba ulimwengu utategemea ujasiri na hatua mathubuti za vijana katika kutafuta amani na maendeleo endelevu. Bwana Ban amesema hayo mjini Vienna, Austria, akikutana na vijana wakati wa mkutano wa tano wa kimataifa wa nchi zinazotetea ustaarabu, yaani Alliance of Civilizations. Katibu Mkuu ametoa wito [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Tushirikiane kudhibiti usafirishaji haramu baharini: UNHCR

Kamishna Mkuu wa UNHCR, Antonio Guterres

Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa juu wa wakimbizi, Antonio Guterres,amerejelea wito wake akizitaka nchi zilizoko katika eneo la Asia Pacific kuanzisha mashirikiano ya pamoja ili kukabiliana na wimbi la watu wanaopoteza maisha wakati wakiwa kwenye misafara ya kimagendo katika bahari ya Hindi.  Ametoa wito huo wakati UNHCR ikiandaa mkutano utakaofanyika mwezi huu huko Indonesia [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wakulima Ethiopia wanufaika na mpango wa P4P: WFP

Moja ya mashine zinazotolewa na WFP kusaidia wakulima Ethiopia

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limetangaza mafanikio makubwa ya mpango wake wa ununuzi wa chakula kwa maendeleo, P4P nchini Ethiopia baada ya vyama vya ushirika kuliuzia shirika hilo kiasi kikubwa cha chakula kinachotosha kulisha watu Milioni Moja nukta nane nchini humo kwa mwezi mzima.  Taarifa zaidi na Assumpta Massoi. (Sauti [...]

26/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na washirika wasaidia raia waliokimbia ghasia Darfur

Wakimbizi wa ndani katika kambi ya muda ya El Sireaf  nchini Sudan

Umoja wa Mataifa na washirika wake huko Sudan umelazimika kutoa misaada ya dharura na hata kuwasafirisha kwa ndege wahanga wa ghasia mpya za  wiki iliyopita huko jimbo la Darfur Kaskazini nchini Sudan. Ujumbe wa pamoja wa Umoja huo na Umoja wa Afrika huko Darfur, UNAMID umeeleza kuwa mapigano hayo  yametokea wakati ambapo tayari Watu Elfu [...]

26/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Watoto, wazazi wajikita kwenye elimu huko Turkana

Watoto wa kiturkana wakipata elimu

Imezoeleka ya kwamba sehemu kubwa ya jamii ya wafugaji imekuwa nyuma kielimu husuani katika elimu ya msingi ambapo watoto wenye umri wa kwenda shule wamekuwa hawafanyi hivyo. Badala yake, watoto hawa hutumia muda mwingi kuchunga mifugo nakufanya kazi nyingine za nyumbani. Huko nchini Kenya katika eneo la Turkana kaskazini-magharibi mwa nchi hiyo, mambo yalikuwa hivyo  [...]

25/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Udhibiti wa mauaji ya kimbari bado safari ni ndefu: Dieng

Adama Dieng, Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa UM kuhusu masuala ya mauaji ya kimbari

Jumuiya ya kimataifa iongeze juhudi kuhakikisha mauaji ya kimbari kama yale yaliyotokea Rwanda na Bosnia-Herzegovina hayajirudii tena, na hiyo ni kauli ya Mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya mauaji ya kimbari, Adama Dieng. Bwana Dieng ametoa ushauri huo wakati wa mjadala wa wazi kwenye siku ya kwanza ya kikao [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na viongozi wa UAE Dubai na Abu Dhabi

494460-bansheikh

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mazungumzo na Sheikh Mohammad bin Rashed Al Maktoum, ambaye ni Waziri Mkuu wa ufalme wa United Arab Emirates, pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje, Dr. Mohammad Gargash. Katika mkutano huo, wamezungumza kuhusu maendeleo katika kanda nzima, yakiwemo masuala kuhusu Syria, Iran, Lebanon, [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bokova afanya ziara nchini Burkina Faso,akutana Rais Compaore.

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso

Mkurugenzi mkuu wa Shirika la elimu , sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova amethibitisha kujitolea kwa shirika hilo kwa mwaka wa kimataifa wa ushirikiano wa sekta ya maji ambao unaoongozwa na shirika hilo. Bokova ameyasema hayo katika mazungumzo na Rais Blaise Compaore wa Burkina Faso nchini humo wakati wa ziara rasmi [...]

25/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kikao cha 22 cha Baraza la Haki za Binadamu chaanza Geneva

Kikao cha Baraza la Haki za binadamu, Geneva, Uswisi

Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa, leo limefungua rasmi kikao chake cha 22, ambacho kitaendelea hadi tarehe 22 Machi, huku rasi wa Baraza hilo akieleza matarajio yake kuwa kikao hicho kitaendeleza heshima ya haki za binadamu, na hivyo kuendeleza pia usalama na maendeleo. Akiongea wakati wa kufungua kikao hicho cha 22, rais [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Uhuru na haki za binadamu ni muhimu kwa UM: Ban

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki- Moon amesema uhuru na haki za binadamu ni mambo muhimu ambayo yanasaidia kusongesha mbele shughuli za Umoja huo. Katika ujumbe wake aliotoa kwa njia ya video kwenye mkutano wa Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva, Uswisi, Bwana Ban amesema baada ya kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lataka utekelezwaji wa mkataba DRC.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Baraza la usalama la Umoja wa Mataiafa limepongeza hatua ya utiwaji saini wa makubaliano ya amani na usalama kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, DRC na ukanda wa nchi za maziwa makuu uliofanyika mwishoni mwa wiki mjini Addis Ababa Ethiopia. Makubaliano hayo yalitiwa saini chini ya udhamini wa Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, nchi [...]

25/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Mamia washiriki mbio za UNEP na mazingira Nairobi

Wanariadhi wanaochipukia walioshiriki mbio hizo

Takribani wanariadha Elfu Mbili wakiwemo waliobobea na wanaochipukia, wanafunzi, wafanyikazi wa Umoja wa Mataifa waliingia kwenye barabara za mji mkuu wa Kenya Nairobi kwenye awamu ya pili ya mbio za Nusu marathoni zilizoandaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Mbio hizo zilikuwa ni za kusherehekea kutangazwa kwa mji  wa Nairobi kuwa mji [...]

25/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ajira ya watoto kwenye sekta ya ufugaji imekithiri: FAO

Watoto wakichunga mifugo

Ajira za watoto katika sekta ya ufugaji ni kubwa na iliyopuuzwa na hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo duniani, FAP kwenye utafiti kuhusu masuala ya ajira za watoto katika sekta ya ufugaji.   Kulingana na FAO  sekta ya kilimo inachukua nafasi kubwa kwenye ajira za watoto duniani na kwamba kukabilina na suala [...]

25/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ITU yazungumzia elimu kwa njia ya mtandao

Elimu mtandao

Shirika la kimataifa la mawasiliano, ITU limesema kuwa mitandao ya intaneti yenye kasi kubwa zaidi yaweza kuimarisha mfumo wa elimu duniani na kusaidia kufikia lengo la maendeleo la milenia la elimu kwa wote. Taarifa ya ITU imekariri ripoti mpya ya tume ya maendeleo ya mitandao ya kasi na mfumo wa digitali inayoeleza kuwa mitandao hiyo [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mikakati yaanza kudhibiti wahamiaji haramu: IOM

Usafirishaji wa wahamiaji haramu

Shirika la kimataifa la kuhudumia wahamiaji IOM, linakutana nchini Tanzania na maafisa uhamiaji kutoka Msumbiji, Malawi na wenyeji wa Tanzania kwa lengo la kubainisha mbinu za kisasa za kukabiliana na wimbi la wahamihaji haramu. Mkutano huo wa siku tatu, unafanyika wakati ambapo kiwango cha wahamiaji haramu kutoka eneo la Pembe ya Afrika wanaomiminika nchini Tanzania [...]

25/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban asifu makubaliano ya utaratibu wa kutafuta amani na usalama DRC

Ban na viongozi wa Afrika Addis

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesifu hatua ya nchi kumi na moja za eneo la Maziwa Makuu kutia saini makubaliano ya utaratibu wa amani, usalama na ushirikiano kwa ajili ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na eneo zima. Akizungumza mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambako makubaliano hayo yamesainiwa, Bwana Ban amesema anatumai kuwa [...]

24/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UM na Polisi Tanzania waimarisha utetezi wa haki za watoto na wanawake

Adolfina Chiallo, Mkuu wa dawati la Jinsia, Jeshi la polisi Tanzania

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya wanawake, UN-WOMEN kwa kushirkiana na jeshi la polisi nchini Tanzania wamezindua dawati maalum la masuala ya jinsia na watoto ambalo litamulika na kufuatialia vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto. Adolfina Chialo ni Kamishna msaidizi wa polisi anayesimamia dawati hilo la jinsia. (SAUTI YA ADOLFINA)

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hospitali ya kutembea yaleta nafuu Somalia

Wahudumu wa kliniki wakitoa huduma kwa wagonjwa Somalia

Wakazi wa maeneo kadhaaa ya Somalia wananufaika na huduma ya hospitali inayotembea ambayo imeanzishwa  ikiwalenga wakimbizi waliolazimika kuhama makazi yao kutokana na  ukame na mapiganao yanayofanywa  na kundi la kigaidi la Al- Shabaab.  Hospitali hiyo inayohudumia takribani watu elfu tatu katika kambi ya KARIBU, na ambayo inamilikiwa na Jeshi la Somali na kudhaminiwa na Ujumbe [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatma ya amani DRC, macho na masikio yaelekezwa Addis Ababa

Walinzi wa amani wa kikosi cha MONUSCO wakiwa na raia huko DRC

Hali ya usalama Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC imeendelea kuwa gumzo kila uchwao kutokana na mazingira yasiyotabirika, ambayo hufanya wakazi wake kuendelea kuwa wakimbizi ndani ya nchi yao iliyosheheni rasilimali lukuki; chini ya ardhi na juu ya ardhi. Katika eneo hilo vikundi vya waasi kikiwemo kile cha M23 kimekuwa kikisababisha hofu miongoni [...]

22/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Njia mpya yapatikana kufika Mali Kaskazini: WFP

Watoto Mali

  Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, limeanzisha njia mpya kwa ajili ya kufanikisha safari za ardhini kuwasambaza huduma muhimu kwa maeneo yanahohitaji misaada ya dharura kaskazini mwa Mali. Hivi sasa misaada ya muhimu inasafirishwa kupitia njia inayoanzia mji mkuu wa Niger Niamey na kulekea moja kwa moja hadi kaskazini mwa Mali ambako kunashudia [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hali ya watu milioni 1.2 kaskazini mwa Mali inatia wasiwasi: OCHA

Wakimbizi wa Mali

Shirika la kuratibu masuala ya kibinadamu la Umoja wa Mataifa OCHA limeelezea wasi wasi wake kuhusiana na hatma ya watu zaidi ya milioni 1.2 kaskazini mwa Mali ambao wameathiriwa na oparesheni za kijeshi. Hata hivyo kumekuwa na dalili za kuyafikia maeneo ya kati mwa Mali na pia kwa kiwango cha kidogo maeneo ya Kaskazini kufuatia [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mongolia yatajwa kuwa mwandalizi wa siku ya mazingira mwaka huu

Kipaumbele kwa uchumi unaolinda mazingira

Taifa la Mongolia ambalo limelipa kipaumbele suala la uchumi usioathiri mazingira kwenye sekta zake za kiuchumi zikiwemo sekta za uchimbaji madini na kutoa hamasisho kwa vijana litakuwa mwandalizi wa siku ya mazingira duniani mwaka huu siku ambayo itadhimishwa tarehe tano mwezi Juni.  Kauli mbiu ya siku hiyo inajulikana kama Think.Eat.Save. Reduce Your Foodprint ikiwa inaipa [...]

22/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNHCR yataka hatua zichukuliwe kuzuia ajali za boti kwenye Bahari ya Hindi

Usafiri wa boti kwa wanaohama jimbo la Rakhine

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi katika Umoja wa Mataifa, UNHCR, limeelezea kusikitishwa na kuongezeka kwa idadi ya watu wanaokufa kwenye Bahari Hindi wakati wakikimbilia usalama wao na kutafuta maisha bora katika nchi za kigeni. Kwa mujibu wa UNHCR, wengi wao ni watu wa jamii ya Rohingya kutoka jimbo la Rakhine, Myanmar, na wengine wakitoka kutoka kwenye [...]

22/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laongeza muda wa ofisi ya UM huko Guinea Bissau

Kikao cha baraza la usalama

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hii leo limepitisha kwa kauli moja azimio namba 2092 kwa Guinea Bissau ambalo pamoja na mambo mengine linaongeza kwa miezi mitatu zaidi muda wa ofisi ya umoja huo nchini humo, UNOGBIS. Ofisi hiyo ina jukumu la kusaidia kuimarisha mchakato wa ujenzi wa amani nchini humo na kiongozi wa [...]

22/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hollywood yamulika mradi wa ILO, yenyewe yatoa angalizo

Washiriki wa tukio hilo la kuhamasisha ajira zinazohifadhi mazingira

Mamia ya watu mashuhuri katika fani ya uigizaji na utunzi wa filamu wameshiriki katika tukio maalum la kutia shime mradi wa shirika la kazi duniani, ILO unaohusu ajira zinazozingatia uhifadhi wa mazingira. Shughuli hiyo iliyofanyika huko Hollywood, iliratibiwa na mtunzi wa filamu Hans Zimmer na mwongozaji filamu Ron Howard ambapo waliangalia miradi kama ule wa [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wawasihi wakazi wa Jonglei kuacha mapigano

Hilde Johnson

Mkuu wa ofisi ya Umoja  wa Mataifa nchini Sudan Kusini Hilde Johnson, amehitimisha ziara yake ya siku mbili kwenye jimbo la Jonglei nchini humo na kutaka jamii ziache mwendelezo wao wa ghasia. Ziara hiyo ilifanyika baada ya tukio la hivi karibuni la wizi wa mifugo na mashambulizi kwa dhidi ya raia kwenye jimbo hilo ambapo [...]

22/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki

ban-dimitris

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Mon amefanya mazungumzo na Waziri wa mambo ya nje wa Ugiriki Dimitris Avramopoulos ambapo wamejadili hali ya kisiasa Mashariki mwa Mediteranian, na pia kuangazia matarajio ya kuanza tena mazungumzo ya kutafuta suluhu la kina huko Cyprus, pamoja na kutafuta suluhu kwa mgogoro kuhusu jina kati ya Ugiriki [...]

21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ukoloni hauna nafasi katika ulimwengu wa sasa: Ban

ban-ki1

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameiambia kamati maalum kuhusu kutokomeza ukoloni kwamba, sasa ndio wakati wa kuwa na ya aina mpya ya mazungumzo kuhusu ukoloni, na ambayo yanawajumuisha wote. Bwana Ban amesema kuwa jamii ya kimataifa sasa inashikilia hata zaidi dhana kuwa, ukoloni hauna nafasi katika ulimwengu wa sasa. Katibu Mkuu ameongeza [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watoa tahadhari ya baa la njaa kufuatia mafuriko Musumbiji

Eneo la Xai Xai kwenye mto Limpopo nchini Msumbiji, moja maeneo yaliyoharibiwa na mafuriko  ya mwaka huu

Taarifa ya timu ya Umoja wa mataifa nchini Msumbiji inaonyesha  Kwamba huenda mvua kubwa ikaendelea kunyesha na kusababaisha mafuriko makali zaidi katika ukanda wa kati na kaskazini mwa Msumbiji.  Taarifa hii inakuja wakati huu ambapo kumekuwa na mlipuko wa kipindupindu katika jimbo la Cabo Delgado lililoko Kaskazini mwa Msumbiji ambapo watu 413 wameripotiwa kuugua huku [...]

21/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

WFP yaonya juu ya tatizo la chakula Yemen

Familia ikiwa na msaada wa chakula

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeonya juu ya kitisho cha ukosefu wa chakula inayoikabili Yemen ikisema kuwa hali ya ukosefu wa chakula huenda ikapindukia kuzidi ile ya mwaka uliopita 2012. WFP imesema kuwa, hali ya uzalishaji chakula imeporomoka kiasi cha kuzua kitisho ambacho kinaweza kuzorotesha ustawi wa kijamii. Imesema kuna wasiwasi wa familia [...]

21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay ataka wavunjifu wa haki za binadamu Haiti kutokingiwa kifua

Navi Pillay

Mahakama Kuu ya Rufani nchini Haiti inatazamia kuendelea juma hili kuzikiliza kesi dhidi ya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu vilivyofanyika wakati wa utawala wa rais wa zamani wa nchi hiyo Jean-Claude Duvalier, Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navy Pillay ameitolea mwito serikali kutowakingia kifua wale waliohusika na vitendo [...]

21/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Makubaliano ya Doha kuhusu Darfur yapewa msukumo

Kikao cha pamoja cha UNAMID na UNCT

Mkutano uliozileta pamoja ujumbe wa pamoja wa Afrika na Umoja wa Maitafa huko Darfur, UNAMID na ofisi ya Umoja wa Mataifa huko Sudan, UNCT umejadili kwa kina njia bora ya kuupa msukumo mpango wa amani katika jimbo la Darfu uliosaniwa Doha, baina ya serikali na kundi la waasi . Mkutano huo umeangazia njia zinazoweza kusaidia [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaungana na Sandbox Global kupiga vita njaa Syria

Ushirikiano wa WFP na Stylista

Mashabiki wa mitindo ya mavazi na washiriki wa michezo ya bahati nasibu kwenye Intaneti wamebuni mchakato mpya wa kulisaidia Shirika la Mpango wa Chakula, (WFP) katika operesheni zake za dharura nchini Syria. Mchakato huo utaambatana na mchezo wa Stylista kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, ambao ulibuniwa na kampuni ya dijitali ya Sandbox Global, yenye [...]

21/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

ILO yasaidia harakati za uhifadhi wa mazingira Kenya

Taa aina ya kandili inayotumia nishati ya jua

Shirika la kazi duniani, ILO nchini Kenya na taasisi ya kuwezesha wanawake nchini humo, Kenya Women Finance Trust wameibuka na mradi wa kusaidia kuhifadhi mazingira na wakati huo huo kuinua kipato cha wanawake. Mradi huo wa miaka miwili utakaoanza mwezi Aprili mwaka huu unalenga kuwapatia mikopo wanawake vijana ili waweze kununua taa aina ya kandili [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Harakati za maendeleo Burundi zazidi kupatiwa shime

Rebecca Grynspan

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye pia kiongozi mshirika wa shirika la Maendeleo la Umoja huo UNDP Rebecca Grynspan ameanza ziara  ya siku tatu nchini Burundi inayonuwia kuweka mikakati ya kuistaawisha  nchi hiyo kimaendeleo baada ya kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Bi Grynspan mbali na kukutana na viongozi mbalimbali  wa [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP yawateua wanamuziki wawili wa Kenya kuwa mabalozi wema.

UNEP

Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP limewateua wanamuziki wawili maarufu kuwa mabalozi wake wema nchini Kenya. Susan Owiyo na Erick Wainaina wote kutoka Kenya wametangazwa rasmi hii leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi Kenya. Susan Owiyo ameshashiriki kwenye tamasha mbali mbali za kimataifa kwenye miji maarufu duniani likiwemo tamasha [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Viongozi wa Afrika watakiwa kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira

Makao Makuu ya UNEP, Nairobi Kenya

Viongozi wa mataifa ya Afrika wametakiwa kuyapa kipaumbele masuala ya mazingira katika kukabiliana na changamoto za kimazingira zinazoshuhudiwa kwa sasa zikiwemo kuchafuka kwa hewa na athari za kemikali kwa afya na mazingira kwa mujibu wa ripoti ya mazingira iliyotolewa hii leo la Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa UNEP. Ripoti hiyo iliyotolewa kwenye mkutano [...]

21/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Quinoa zao la kumkomboa mkulima, lastahimili ardhi kame!

Quinoa

Hatimaye mwaka wa kimataifa wa zao la Quinoa umezinduliwa rasmi kwenye kikao maalum cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani. Shughuli hiyo imeshudiwa na viongozi na wawakilishi wa mataifa na mashirika mbali mbali akiwemo Rais wa Bolivia, Evo Morales ambaye nchi yake ndiyo inaongoza duniani kwa kuuza zao hilo nje ya [...]

20/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Myanmar imeendelea kupiga hatua kutekeleza mageuzi- Mtaalamu UM

Tomás Ojea Quintana

Mtaalamu wa masuala ya haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Myanmar amesema nchi hiyo imeanza kupiga hatua kwa kuchomoza mifumo inayozingatia misingi ya haki za binadamu lakini ameonya kuwa safari bado ni ndefu. Toma's Ojea amesema kuwa taifa hilo linapiga hatua kusonga mbele na kukaribisha matumaini ambayo amesema kuwa yanafungua ukusara mpya na [...]

20/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Maandalizi ni muhimu kabla ya kupeleka vikosi vya kulinda amani: Ladsous

Herve-Ladsous

Umoja wa Mataifa umetakiwa kujenga kile kinachoitwa maandalizi ya awali wakati wa kuelekea kwenye operesheni za amani katika nchi za Mali, Syria na eneo la Pembe ya Afrika. Mkuu wa masuala ya ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataiaf Hervé Ladsous, amesema hayo wakati akizungumza na kamati maalumu inayohusika na ulinzi wa amani inayofahamika [...]

20/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia ukosefu wa haki ina usawa duniani

socialjustice

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema kutokuwepo kwa usawa na haki miongoni mwa jamii kunazorotesha juhudi za jumuiya za kimataifa katika kuwakwamua mamilioni ya raia katika umaskini. Taarifa zaidi na Alice Kariuki. (SAUTI YA ALICE KARIUKI)     Taarifa zaidi na ALICE KARIUKI ………… Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hiyo ya [...]

20/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wahisani watathmini usaidizi wa kibinadamu huko ukanda wa Sahel

Ukame ukanda wa Sahel

Mwaka mmoja tangu jumuiya ya kimataifa izindue kampeni mahsusi ya kushughulikia matatizo ya kibinadamu huko Ukanda wa Sahel, hii leo wahisani wamekutana huko Geneva, Uswisi na kutathmini usaidizi huo ambapo wamesema umekuwa wa manufaa lakini bado msaada zaidi wahitajika. Wakuu wa mashirika ya kimataifa ikiwemo ya Umoja wa Mataifa walitathmini na kusema kuwa usaidizi mkubwa [...]

20/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Netanyahu wazungumzia hali ya Mashariki ya Kati

KM Ban na Waziri Mkuu Netanyahu

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin Moon amempongeza Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kufuatia ushindi alioupata katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini humo. Katika mazungumzo yao yaliyofanyika kwa njia ya simu viongozi hao pia wamejadili umuhimu wa kufufua mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina na hali ya amani katika [...]

20/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mwaka wa kimataifa wa zao la Quinoa wazinduliwa, Ban atoa angalizo

Mkulima wa Quinoa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumza katika shughuli maalum ya uzinduzi wa mwaka wa kimataifa wa zao la Quinoa [Keen-wa] na kusema kuwa kutambulika kwa zao hilo kutasaidia kuharakisha utimizaji wa malengo ya maendeleo ya Milenia ikiwemo lile la kupunguza njaa kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2015. Katika hotuba yake Bwana Ban [...]

20/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WIPO yapanua kumbukumbu zake za nembo za biashara na Hakimiliki

WIPO

Shirika la kimataifa linalohusika na kulinda nembo za biashara na hakimiliki, WIPO limetangaza kupanuka kwa kumbukumbu zake za nembo na majina ya biashara. Shirika hilo limejumuisha kwenye kumbukumbu zake sehemu zingine sita ikiwemo ofisi ya majina na nembo za bishara nchini Marekani  na kuongeza kumbukumbu zake kutoka milioni 2.2 hadi milioni 10.9 na kulifanya kuwa [...]

20/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kudumisha amani wafanyika Pwani ya Kenya

Adama Dieng

Mkutano wa kutafuta njia za kuzuia mizozo na machafuko wakati wa uchaguzi unafanyika mjini Mombasa, Kenya. Mkutano huo umeandaliwa na kamati ya kuzuia mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Kenya, ambayo inafadhiliwa na Afisi ya Mshauri Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari. Mkutano huo ambao pia umehudhuriwa na [...]

20/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aelezea kusikitishwa na hatma ya wafungwa wa Kipalestina

Katibu Mkuu Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, ban Ki-Moon, ameelezea kusikitishwa na hali inayoendelea kuzorota ya wafungwa wa Kipalestina wanaozuiliwa na mamlaka ya Israel, na ambao sasa wanafanya mgomo wa kutokula chakula. Taarifa ya msemaji wake imesema Bwana Ban, ambaye amesikitishwa zaidi na hali ya mfungwa Samer Issawi, amepokea barua kutoka kwa Rais Mohammud Abbas, na [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Syria haitaki misaada iingie kupitia mpaka wake na Uturuki: Amos

Mkuu wa OCHA, Bi. Valerie Amos

Umoja wa Mataifa umesema mgao wa hivi karibuni wa misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa ndani nchini Syria haukuweza kuwafikia wale wote wanaohitaji kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo. Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linaloratibu misaada ya kibinadamu, OCHA, Bi. Valeri Amos ametoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari baada ya mkutano [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Liberia yahitaji dola Milioni 37 kukidhi mahitaji ya kibinadamu 2013

Wakimbizi nchini Liberia

Serikali ya Liberia na Umoja wa Mataifa hii leo wametangaza ombi la dola Milioni 37 zitakazotumika kukidhi mahitaji ya binadamu nchini humo kwa mwaka huu wa 2013 kutokana na hali ngumu inayoendelea kukabili wananchi. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Martin Nersiky amewaambia waandishi wa habari kuwa Liberia inaendelea kukabiliwa na changamoto kubwa za kibinadamu ambapo [...]

19/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Idadi ya raia waliouawa katika mzozo wa Afghanistan ilipungua 2012: UNAMA

Wananchi wa Afghanistan

Ripoti mpya ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA) imeonyesha kushuka kwa idadi ya raia walouawa katika mapigano kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka sita. Ripoti hiyo kuhusu ulinzi wa raia katika mizozo ya silaha, na ambayo imeandaliwa na UNAMA kwa ushirikiano na Ofisi ya Haki za Binadamu katika Umoja wa [...]

19/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Si sahihi mahakama ya kijeshi kutumika kuhukumu raia: Pillay

Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya UM, Navi Pillay

Ofisi ya Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu imesema imesikitishwa na kitendo cha Sahara Magharibi kutumia mahakama za kijeshi kuendesha kesi zinazowahusu raia ikisema kuwa hatua hiyo uvunjifu wa haki za binadamu. Mamlaka katika eneo la Sahara Magharibi imeripotiwa, kuwatia hatiani raia 25 kwa kutumia mahakama za kijeshi. Mahakama hiyo ya kijeshi ambayo [...]

19/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ripoti ya UM yaweka bayana athari za mazingira kwa mfumo wa endokrini

UNEP

Ripoti ya shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP imesema kuwa matumizi ya kemikali ambazo hazifanyiwa uchunguzi  zinaweza kuleta hitalafu katika mwili wa binadamu ikiwemo kuvuruga mfumo wa homoni. Ripoti hiyo ambayo pia imeandaliwa kwa pamoja pia na shirika la afya ulimwenguni WHO imekariri mfumo wa kisanyansi unaojulikana Endokrine ambayo ni mahsusi kwa [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wakosoa muswada unaobinya uhuru wa kuandamana Misri

Waandamanaji nchini Misri

Kamishna wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay amekosoa hatua ya upitishwaji wa muswada wa sheria inayobinya uhuru wa watu kufanya maandamano iliyoungwa mkono na baraza la mawaziri wa  nchi hiyo. Pillay amesema kitendo hicho hakifungamani na misingi inayolinda na kutetea haki za binadamu. Amesema kuwa pamoja na ukweli kwamba uhuru wa [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani mashambulio ya kigaidi ya karibuni Somalia

Balozi Augustine Mahiga, Mkuu wa UNPOS

Ofisi ya masuala ya kisiasa kuhusu Somalia katika Umoja wa Mataifa (UNPOS), imelaani mashambulizi ya kigaidi ambayo yametekelezwa nchini Somalia katika kipindi cha wiki mbili za kwanza mwezi Februari mwaka 2013, pamoja na kuuawa kwa msomi maarufu wa Kiislamu, Sheikh Abdiqadir “Ga’amey” Nur Farah, kule Garowe.   Mauaji ya Dkt. Nur Farah yametendeka baada ya [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa kuhusu mazingira na chakula waendelea Nairobi

Chakula kilichotupwa

Suala la utupaji wa chakula ni moja ya ajenda kuu zinazozungumziwa mwenye mkutano wa kimataifa unaowaleta pamoja mawaziri wa mazingira kutoka pembe zote za ulimwengu ambao kwa sasa umeingia siku yake ya pili mjini Nairobi nchi Kenya. Inakadiriwa kuwa kiasi cha tani Bilioni 1.3 za chakula hutupwa kila mwaka duniani ambapo asilimia kubwa hupotea wakati [...]

19/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Japan kutekeleza mfumo wa breki za gari wa kuzuia ajali barabarani

Usalama barabarani

Taifa la Japan mwezi huu litaanza kutekeleza hatua ya kuhakikisha usalama kwenye malori na mabasi kuambatana na kanuni nambari 13 ya tume ya uchumi ya Umoja wa Mataifa barani Ulaya UNECE kuhusu mfumo maalum wa breki za magari ikiwa ndiyo nchi ya 43 kutekeleza kanuni hiyo. Tume hiyo inasema kuwa kuanza kutumika kwa kanuni hiyo [...]

19/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Hali yausalama bado kikwazo katika usambazaji misaada Syria:WFP

Mgao wa wa chakula kwa wakimbizi

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema licha ya kwamba limeshiriki kwenye operesheni ya pamoja ya mashirika Umoja huo ya kusambaza misaada kwa wakimbizi walioko kambi ya Karameh nchini Syria, bado hali ya usalama si nzuri. WFP imesema operesheni hiyo ya tarehe 16 mwezi huu katika mkoa wa Idleb kaskazini Magharibi [...]

19/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ulimwengu waungana kupinga dhuluma dhidi ya wanawake katika kampeni ya "One Billion Rising"

Wanawake kwenye kampeni ya 1 Billion Rising

Kote duniani, watu wa tabaka mbalimbali walicheza muziki mnamo siku ya Alhamis, Februari kumi na nne, ambayo ni maarufu kama siku ya wapendanao, Wengi wao walikuwa wakijiunga kwenye kampeni ya kimataifa ijulikanayo kama "One Billion Rising", ya kupinga dhuluma dhidi ya wanawake. Kauli mbiu ya kampeni hiyo katika Umoja wa Mataifa ilikuwa "Kataa ukatili wa [...]

18/02/2013 | Jamii: Jarida, Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Kituo cha Seruka huko Burundi chapaza sauti kulinda haki za wanawake na watoto

Wanawake nchini Burundi

Utekelezaji wa vitendo dhalili dhidi ya wanawake na watoto wa kike unaendelea kupigiwa kelele kila uchwao na kwa kutumia mbinu mbali mbali kwa kuwa jamii zinazotekeleza vitendo hivyo nazo huibuka na mbinu mpya kila wakati ili kuweza kuendelea kukiuka haki za binadamu za wanawake na watoto wa kike. Nchini Burundi, ambako nako kuna vitendo vya [...]

16/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama laonya wanaoingilia mchakato wa mpito Yemen

Baraza la Usalama la UM

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeridhia taarifa ya Rais wa baraza hilo kuhusu Yemen ambayo pamoja na kupongeza tangazo la kuwepo kwa mjadala wa kitaifa nchini humo baadaye mwezi huu inaonya wale wote wanaokwamisha mchakato wa mpito nchini humo akiwemo Rais wa zamani Ali Abdullah Salehe. Akisoma taarifa hiyo kwa waandishi wa habari, [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Usalama na haki za binadamu bado changamoto Sudan Kusini: UM

Hilde Johnson, Msaidizi wa Katibu Mkuu wa UM na Mkuu wa UNMISS

Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani huko Sudan Kusini, UNMISS Hilde Johnson amesema mwaka mmoja na nusu wa taifa la nchi hiyo umekumbwa na changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa usalama na ukiukwaji wa haki za binadamu. Katika mahojiano maalum na radio ya Umoja wa Mataifa, Bi. Johnson ambaye pia ni [...]

15/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ujuzi wa waandishi ni muhimu katika matangazo ya radio

radioday11

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa Februari dunia iliadhimisha siku ya Radio duniani. Siku hii hutoa fursa kwa radio za kimataifa, kitaifa na za kijamii kutathmini shughuli zao za kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Mathalani mchango wa Radio katika ukombozi wa kisiasa, kiuchumi na kijamii na hata usalama wa waandishi wa habari. Radio imebuniwa zaidi [...]

15/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban aonyesha wasiwasi juu ya hatma ya kisiasa Maldives

Mohamed Nasheed, Rais wa zamani wa Maldives

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ameonyesha wasiwasi juu ya hali ya kisiasa huko Maldives na hatma ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Nasheed ambaye kwa sasa ameomba hifadhi kwenye ubalozi wa India nchini humo. Bwana Ban amekaririwa na msemaji wake akipendekeza pande zote zinazovutana zijizuie kufanya vurugu na badala yake [...]

15/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Waliokimbia makazi yao Mali wataka kurejea nyumbani: IOM

Familia inayoishi ukimbizini mjini Bamako, Mali

Utafiti uliofanywa na  Shirika la Uhamiaji Duniani (IOM) unaonyesha kuwa asilimia 93 ya jamii zilizotimuliwa kutoka maeneo ya kaskazini mwa Mali na ambazo sasa zinaishi katika mji mkuu Bamako na mji jirani Koulikoro zinataka  kurejea nyumbani mara tu hali ya usalama na ya kiuchumi itapoimarika. Utafiti huo uliofanywa kwa njia ya simu mapema mwezi huu [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM watuma wataalam wa haki za binadamu nchini Mali.

Wananchi wa Mali

Huku hali ya usalama nchini Mali ikibaki kuwa tete, Ofisi ya Kamishina Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa imesema inawatuma wataalamu wa haki za binadamu kuchunguza hali ilivyo nchini humo. Wataalamu watatu ambao tayari wamewasili mjini Bamako watachunguza madai ya ukiukaji wa haki za binadamu, yakiwemo madai ya ulipizaji kisasi. Cécile Pouilly [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM, Mashirika ya kiraia yaonya kuhusu baa la njaa CAR

Wananchi wa CAR wakisubiri mgao wa chakula

Tathmini iliyofanywa na Umoja wa Mataifa na mashirika yasiyo ya kiserikali kuhusu usalama wa chakula katika Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), imeonyesha kuwa mizozo ya kisiasa na kijeshi kati ya mwezi Disemba mwaka 2012 na mwezi Januari mwaka huu, huenda ikatumbukiza nchi hiyo kwenye baa la ukosefu wa chakula. Maeneo mengi yaliyoshikiliwa na muungano [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Msimu wa upanzi Mali wakaribia wakulima hawapo: FAO

Mkulima wa Mahindi, Mali

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO limesema msimu wa upanzi unakaribia huko Mali lakini kuna wasiwasi kutokana na jinsi ya kurejesha wakulima kwenye maeneo yao baada ya kukimbia mapigano yaliyoanzia kaskazini mwa nchi hiyo. Hali hiyo ndiyo ilimsukuma Mkurugenzi wa Shirika la mpango wa chakula na kilimo FAO José Graziano da Silva kuwa na [...]

15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yasambaza misaada kwa waathirika wa mafuriko Chad

Wahanga wa mafuriko Chad

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM, limeanzisha juhudi za kusambaza misaada ya dharura kwa mamia ya watu waliokumbwa na mafuriko katika mji mkuu wa Chad N'Djamena na maeneo mengine ya jirani na kusababisha kiasi cha watu 98,000 kupoteza makazi yao na wengine 560,000 kuwa katika hali ya shida na taabu. IOM kwa [...]

15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Ban asihi uongozi imara wa Marekani katika kukabiliana na changamoto za kimataifa

Katibu Mkuu Ban Ki-Moon na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa wito kwa serikali ya Marekani iendelee kuongoza katika kukabiliana na changamoto nyingi za kikanda na za kimataifa, wito ambao ametoa wakati wa ziara yake mjini Washington, ambako amekutana na kufanya mashauriano na Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry. Viongozi hao wawili wamejadili [...]

15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tuwekeze katika ukusanyaji wa takwimu za afya: WHO

Shirika la afya duniani

Viongozi wa takwimu za masuala ya afya waliokutana mjini Geneva, Uswisi kujadili ushirikiano wa siku za usoni katika kuboresha mbinu za makadirio ya takwimu kuhusu masuala ya afya wamehitimisha mkutano kwa kukubaliana  uwekezaji zaidi katika sekta hiyo. Mkutano huo uliandaliwa na shirika la afya duniani, WHO ambapo mathalani washiriki wamesema zaidi ya nchi 100 hazina [...]

15/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

WFP yasafirisha misaada ya chakula kwenda Punia mashariki mwa DRC

Ndege ikiwa na shehena ya misaada

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesafirisha kwa ndege vyakula kwa ajili ya maelfu ya watu ambao wamelazimika kuhama makwao kwenye mji wa Punia ulio Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, DRC. WFP imesema usambazaji wa biskuti zenye lishe bora unatarajiwa kung'oa nanga hapo kesho. Shirika hilo limesema mvua kubwa zinazonyesha zimelazimu watumie [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Vifo vitokanavyo na Hepatitis E vyaongezeka Sudan Kusini:UNHCR

Wakimbizi Sudan Kusini wakisaka maji

Shirika la kudumia wakimbizi duniani, UNHCR limesema idadi ya wakimbizi huko Sudan Kusini waliokufa kutokana na ugonjwa wa ini aina ya E, au Hepatitis E imeongezeka na kufikia zaidi ya 111 tangu mwezi Julai mwaka jana. UNHCR imesema idadi ya walioambukizwa nayo imefikia zaidi ya Elfu sita na takwimu hizo zilikusanywa na shirika la afya [...]

15/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Burundi yapaza sauti kutetea wanawake

Wanawake Burundi

Burundi nayo imejumuika na mataifa mengine katika kampeni hiyo ambapo SERUKA ambacho ni kituo pekee cha kupokea wanawake waathirika wa vitendo vya ukatili ikiwemo wa kingono na majumbani kilikuwa mstari wa mbele. Mmoja wa washiriki ni Yvone kutoka eneo la Songa mjini Bujumbura. (SAUTI YVONE) Kwa upande wake Lysie ambaye naye alikuwepo kwenye kituo hicho [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban akutana na waziri mpya wa mambo ya nje Marekani, John Kerry

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Waziri Mpya wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo amekutana na kufanya mashauriano na Waziri mpya wa Mambo ya nje wa Marekani, John Kerry. Wakizungumza na waandishi wa habari mjini Washington, Marekani, Bwana Ban amempongeza Bwana Kerry kwa uteuzi wake katika wadhfa huo, na kumsifu kwa ushirikiano wake kuhusu masuala mengi, yakiwemo ya kisiasa, usalama [...]

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hafla ya madhehebu ya dini kuungana kwa ajili ya amani yafanyika kwenye UM

Vuk Jeremic

Hafla maalum imefanyika leo kwenye makao makuu ya UM mjini New York, kuadhimisha kuanza kwa wiki moja ya Ushirikiano wa dini mbalimbali duniani, kama ilivyotangazwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa katika azimio namba 65/5. Hafla hiyo yenye kauli mbiu, "Kuungana kwa ajili ya desturi ya amani kupitia ushirikiano wa dini" imeandaliwa na afisi [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa kimataifa wa vijana wakamilika Nairobi

Amina Mohammed, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa UNEP akizungumza na vijana kwenye mkutano wa TUNZA

Mkutano wa kimataifa wa vijana ambao umedumu kwa muda wa juma moja umekamilika kwenye makao  ya Umoja wa Mataifa mjini Nairobi nchini Kenya. Washiriki walijadili masuala ya chakula na mazingira ikiwemo utupaji wa chakula wakati watu wengi wana uhaba wa chakula. Taarifa zaidi na Jason Nyakundi. (SAUTI JASON)

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Makao Makuu ya UNPOS sasa kuhamia Mogadishu ili kuimarisha usaidizi wake

Tayé-Brook Zerihoun, Naibu mkuu wa Ofisi ya masuala ya siasa ya UM akiwasilisha ripoti ya Katibu Mkuu kuhusu Somalia

  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepokea na kuridhia ripoti ya Katibu Mkuu  Ban Ki-Moon kuhusu hali ilivyo nchini Somalia ambayo pamoja na mambo mengine imependekeza kuhamisha ofisi ya Umoja huo kuhusu Somalia, UNPOS kutoka Nairobi, Kenya kwenda Mogadishu. Ripoti hiyo iliwasilishwa na Tayé-Brook Zerihoun ambaye alisema kuwa hatua hiyo ni muhimu kwa [...]

14/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Haki za binadamu hazitambui mpaka: Pillay

Navi Pillay

  Kamishna wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za binadamu Navi Pillay, amesisitiza haja ya kuingilia kati kutafutia ufumbuzi mambo yanayohusu haki za za binadamu kwenye eneo la Trinistran huko barani Ulaya, kufuatia ripoti moja iliyochapishwa leo kuhusu haki za binadamu kwenye eneo hilo. Akisisitiza juu ya hilo, Pillay amesema kuwa suala la haki [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watu waendelea kulazimika kuhama licha ya waasi wa FARC Colombia kusitisha mapigano: OCHA

colombia_farc

Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, OCHA, imesema kuwa licha ya idadi ya mashambulizi kupungua, idadi ya watu wanaolazimika kuahama makwao nchini Colombia bado inaendelea kupanda kwa sababu makundi yenye silaha bado yanafanya mashambulizi. Mashambulizi ya kundi lenye silaha la FARC yalishuka kwa asilimia 73 katika kipindi cha miezi miwili ya [...]

14/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UN-Habitat yazindua ripoti kuhusu ukuaji wa miji

unhabitat-1

Ripoti mpya ya Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa, UN-Habitat, imesema kuwa watunga sera na wadau katika masuala ya maendeleo wanatakiwa kuzingatia ukuaji na maendeleo jumuishi zaidi. Ripoti hiyo iitwayo, “Hali ya miji ya dunia mwaka 2012/2013,” na ambayo inahusu ukuaji wa miji, inasema kuna haja ya kuzingatia ukuaji unaozidi ukuaji wa kiuchumi tu, [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Chanjo dhidi ya homa ya manjano kuanza Chad: WHO

homa ya manjano

Wizara ya Afya nchini Chad imepanga kuanza chanjo ya dharura ya jumla dhidi ya homa ya manjano, kufuatia kuthibitishwa kwa visa viwili vya maambukizi ya homa hiyo mnamo Disemba mwaka 2012. Kampeni hiyo ya chanjo itafanyika katika wilaya tatu zinazopakana na eneo la Darfur nchini Sudan, ambako visa vya homa ya manjano vilikuwa vimeripotiwa awali, [...]

14/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Wakimbizi Mogadishu wahamishiwa makazi mapya: UM

Mtoto akiwa ndani ya moja ya kibanda ambacho ni makazi yao huko Somalia

Maisha duni ya wakimbizi wa ndani mjini Mogadishu Somalia yaliyodumu kwa takribani miongo miwili ya mzozo nchini humo sasa yameimarika kutokana na hatua zilizochukuliwa na mashirika ya Umoja wa Mataifa. Mashirika hayo 14 pamoja na mengine ya kiraia yalichukua hatua ya kuhamisha familia Elfu Tano za wakimbizi kwenda maeneo mapya mjini Mogadishu ambako makazi, malazi [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Paza sauti kutetea wanawake na watoto wa kike: Bachelet

Washiriki wa kampeni mjini Manilla, Ufilipino wakicheza muziki

Kataa ukatili wa majumbani, kataa ubakaji na uhalifu wa kingono. Huo ni ujumbe wa hii leo wa Mkuu wa shirika la masuala ya wanawake la Umoja wa Mataifa, UN-WOMEN  Michelle Bachelet inayofanyika duniani kote ili kutokomeza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Kampeni hiyo ijulikanayo kama One billion rising inadhaminiwa na shirika la V-Day linaloongozwa [...]

14/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Amerika zishirikiane na UM kutatua matatizo ya dunia: Ban

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akizungumza kwenye mkutano wa OAS

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye yuko mjini Washington D.C kwa shughuli mbali mbali, siku ya Jumatano ametoa wito kwa nchi za Amerika kushirikiana na Umoja huo katika kutatua matatizo yanayokabili dunia hivi sasa. Bwana Ban katika hotuba yake kwa Baraza la Kudumu la Ushirikiano wa nchi za Amerika, OAS, amesema bara la hilo [...]

13/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula na lishe vipewe kipaumbele katika malengo ya maendeleo: FAO

FAO LOGO

Mkutano wa wadau mbalimbali wanaojadili kuhusu ajenda ya maendeleo ya kimataifa baada ya mwaka 2015, umetoa wito wa kufanya usalama wa chakula na lishe kuwa nguzo ya juhudi za maendeleo ya siku zijazo. Mkutano huo umetaka dhamira mpya ziwekwe kwa ajili ya jamii nzima ya kimataifa. Mjadala huo wa siku mbili kuhusu njaa, usalama wa [...]

13/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Pillay aelezea hofu kuhusu afya ya mahabusu wa Kiapalestina

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea hofu yake kufuatia ripoti za kudhoofika kwa afya ya mahabusu watatu wa Kipalestina wanaozuiliwa na Israel, na ambao wanafanya mgomo wa kutokula chakula. Tarek Qa'adan na Jafar Azzidine wamekuwa kwenye mgomo huo kwa siku 78, ili kupinga kuzuiliwa kwao na Israel, huku [...]

13/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Pillay, Falk waelezea hofu kuhusu afya ya mahabusu wa Kiapalestina

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea hofu yake kufuatia ripoti za kudhoofika kwa afya ya mahabusu watatu wa Kipalestina wanaozuiliwa na Israel, na ambao wanafanya mgomo wa kutokula chakula. Tarek Qa'adan na Jafar Azzidine wamekuwa kwenye mgomo huo kwa siku 78, ili kupinga kuzuiliwa kwao na Israel, huku [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Radio kuendelea kuwepo leo, kesho na milele: Mbotela

Leonard Mambo Mbotela, mtangazaji mkongwe Afrika Mashariki

Katika ukanda wa Afrika Mashariki, jina Leonard Mambo Mbotela ni maarufu sana kutokana na vile ambavyo mtangazaji huyo mkongwe wa Radio wa nchini Kenya alivyoweza kumudu mikrofoni yake na kuwasiliana na msikilizaji kila uchwao. Miongoni mwa vipindi tulivyofanya katika kuadhimisha siku ya radio duniani ni mahojiano na mtangazaji huyo mkongwe kuhusu mambo mbali mbali ikiwemo [...]

13/02/2013 | Jamii: Mahojiano, Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Usalama wa chakula na lishe vipewe kipaumbele katika malengo ya maendeleo: FAO

fao-food-10

Mkutano wa wadau mbalimbali wanaojadili kuhusu ajenda ya maendeleo ya kimataifa baada ya mwaka 2015, umetoa wito wa kufanya usalama wa chakula na lishe kuwa nguzo ya juhudi za maendeleo ya siku zijazo. Mkutano huo umetaka dhamira mpya ziwekwe kwa ajili ya jamii nzima ya kimataifa. Mjadala huo wa siku mbili kuhusu njaa, usalama wa [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki, Malengo ya maendeleo ya milenia | Kusoma Zaidi »

Bara la Afrika laungana kudhibiti majanga ya asili

Africa map

Wawakilishi kutoka nchi 40 za Afrika wanakutana huko Arusha, Tanzania kujadili njia za kuzuia na kupunguza athari za za majanga wakati huu ambapo ulimwengu unaoendea kuathiriwa na mabadiliko ya tabianchi, ukame, mafuriko , kupanda kwa joto, moto wa misistuni na majanga mengine ya kiasili. Kulingana na makadirio kutoka kituo cha utafiti wa hali ya hewa [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lapokea ripoti kuhusu Burundi

Baraza la Usalama

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hii leo kwa kauli moja limepitisha azimio nambari 2090 kuhusu Burundi, ambalo, pamoja na mambo mengine, linataja utekelezaji wa mauaji unaodaiwa kufanywa na vyombo vya dola kinyume na sheria, mauaji ambayo yanadaiwa kuambatana na sababu za kisiasa, na limependekeza mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC kufanya uchunguzi zaidi. [...]

13/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Kujumuishwa kwa wanawake katika ajira India kumeshuka: ILO

women india

Ripoti mpya ya Shirika la Ajira Duniani, ILO, imesema kuwa idadi ya wanawake ambao hawana ajira, au hawatafuti ajira kusini mwa bara Asia ipo chini zaidi kuliko ile ya wanaume. ILO imesema, wakati asilimia 80 ya wanaume katika eneo hilo wana ajira au wanatafuta ajira, idadi ya wanawake ipo chini zaidi, ikiwa ni asilimia 32 [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP kuanza kutumia bandari ya DSM nchini Tanzania

Rais Kikwete na Ertharin Cousin

Shirika la mpango wa chakula duniani (WFP), limesema kuanzia sasa litaanza kutumia Bandari ya Dar es salaam nchini Tanzania kusafirishia misaada ikiwemo chakula katika nchi za Maziwa makuu pamoja na zile za Pembe ya Afrika. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa shirika hilo Bi Ertharin Cousin aliyekamilisha ziara ya siku mbili nchini Tanzania ambapo wakati wa [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Adhaniaye radio inakufa hajui asemalo: Mbotela

Leonard Mambo Mbotela

Nchini Kenya, akizungumzia siku ya Radio duniani, mmoja wa watangazaji wakongwe nchini humo Lenard Mambo Mbotela amesema adhaniaye radio inakufa hajui asemalo kwani hata sasa wanaotengeneza magari wanalazimika kuweka radio tena za kisasa ili waweze kupata wanunuzi. Kuhusu nafasi ya radio na siasa amesema kwa sasa Kenya inapojiandaa na uchaguzi mkuu mwezi ujao, radio inatumika [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Radio yaendeleza demokrasia na maendeleo endelevu: UM

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon

Ikiwa ni zaidi ya miaka mia moja tangu kuanzishwa kwake, Radio imeripotiwa kuendelea kuwa chombo muhimu katika maisha ya kila siku ya mwanadamu ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumzia nafasi ya chombo hicho katika kuunganisha watu bila kujali mipaka yao. Akitoa ujumbe wa siku hii, Bwana Ban amesema katika kipindi hicho [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Radio yaunganisha watu na maeneo mengine: Ban

Watoto wakiwa wanasikiliza radio kwa pamoja

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ametoa ujumbe wake wa siku ya Radio duniani hii leo na kusema ni fursa kwa kila mtu kusherehekea na kutambua uwezo wa redio wa kuunganisha watu wote hata wale walio masafa ya mbali. Bwana Ban amesema tangu kubuniwa kwake zaidi ya miaka 100 iliyopita, redio imekuwa chombo [...]

13/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yagawa misaada ya dharura kwa wahamiaji raia wa Chad

Nembo la IOM

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewapelekea chakula , maji na madawa kundi la wahamiaji 32 waliawasili kwenye ofisi za IOM kwenye mji wa Faya Largeau kaskazini mwa Chad juma lililopia baada ya kutimuliwa kutoka nchini Libya. Makundi matatatu ya raia wa Chad wametimuliwa kutoka Libya mwezi Julai mwaka uliopita. Kutimuliwa kwa wahamiaji kunajiri baada [...]

12/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Baraza la usalama lipaze sauti moja kulinda raia kwenye migogoro

Navi Pillay, Kamishna Mkuu wa Tume ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekumbushwa jukumu lake la kupaza sauti moja ili kulinda maisha ya raia wasio na hatia wanaojikuta katikati ya mizozo sehemu mbali mbali duniani. Hayo yameibuka wakati wa mjadala wa wazi kuhusu usalama wa raia kwenye maeneo ya migogoro ambapo Kamishna Mkuu wa tume ya haki za binadamu ya [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lashutumu jaribio la nyuklia la DPRK

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Korea, Kim Sung-Hwan

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limeshutumu vikali kitendo cha Jamhuri ya Kidemokrasia ya watu  wa Korea DPRK kufanya jaribio la nyuklia siku ya Jumanne. Kauli ya baraza hilo imetolewa muda mfupi baada ya mashauriano ya dharura yaliyofanywa na wajumbe, kufuatia taarifa hizo za jaribio ambapo, taarifa ilisomwa mbele ya waandishi wa habari na [...]

12/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Radio ya Umoja wa Mataifa enzi hizo

Audrey Hepburn

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa February, mamilioni ya watu duniani kote wanasherehekea siku ya Radio duniani. Tukio hili linalenga kuonyesha nguvu ya radio na umuhimu wa matangazo yake yanayofikia mamilioni ya watu kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Maadhimisho haya yanarejelea mwaka 1946 ambapo Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha radio yake yenyewe. [...]

12/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Mkurugenzi Mkuu wa WFP azuru Tanzania

Ertharin Cousin, Mkurugenzi Mkuu WFP

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ertharin Cousin, ameanza ziara ya siku mbili nchini Tanzania hii leo. Akiwa mjini Dar es Salaam, Bi Cousin anatarajiwa kuzuru eneo la bandari kunakofanyika operesheni za WFP, ili kukagua eneo hilo ambalo ni muhimu kwa kazi ya WFP barani Afrika. Bi Cousin pia anatarajiwa kukutana [...]

12/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Uingereza yathibitisha kisa kingine cha homa ya Novel Coronavirus: WHO

Shirika la afya duniani, WHO

Serikali ya Uingereza imeripoti kuthibitisha kisa cha maambukizi ya homa ya Novel Coronavirus, kufuatia mkazi wake mmoja kuonyesha dalili za maambukizi ya virusi hivyo kuanzia Janauri 26 mwaka huu. Vipimo vya maabara vimebainisha mgonjwa huyo akiwa na homa ya H1N1 pamoja na Novel Coronavirus, na hivi sasa amewekwa katika kituo cha kutibu wagonjwa maututi. Uchunguzi [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban alaani majaribio ya zana za nyuklia nchini Korea Kaskazini

nuclear-explosion1

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki moon amelaani hatua ya Korea Kaskani ya kufanya majaribio ya zana za kinyumlia hii leo .Ban amesema kuwa hatua hiyo ni ukiukaji mkubwa wa mkataba wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa. Ban mara kwa mara amekuwa akitoa wito kwa utawala mpya wa taifa la Korea [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM yagawa misaada ya dharura kwa wahamiaji raia wa Chad

Wahamiaji wawasili Chad kutoka Libya

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM limewapelekea chakula , maji na madawa kundi la wahamiaji 32 waliawasili kwenye ofisi za IOM kwenye mji wa Faya Largeau kaskazini mwa Chad juma lililopia baada ya kutimuliwa kutoka nchini Libya. Makundi matatu ya raia wa Chad wametimuliwa kutoka Libya mwezi Julai mwaka uliopita. Kutimuliwa kwa wahamiaji kunajiri baada [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IAEA kushirikiana na Tanzania kukabili tatizo la Kansa

Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Yukiya Amano akikagua moja ya mitambo nchini Tanzania

Shirika la Kimataifa la za nguvu za atomiki(IAEA) limesema litaendelea kuunga mkono juhudi za nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania katika kukabiliana na magonjwa ya kansa ambayo yanaripotiwa kukua kwa kasi katika nchi za dunia ya tatu. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa IAEA, Yukiya Amano ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili akikagua shughuli [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wananchi wakimbia vijiji, wajificha maporini huko Jamhuri ya Afrika ya Kati

Vijiji ambavyo wananchi wamevikimbia kaskazini mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Ujumbe wa pamoja wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR na lile la misaada la Mercy Corps uliokwenda huko Bambari na Kaga Bandoro Jamhuri ya Afrika ya Kati umebaini uporaji na kutelekezwa kwa vijiji kadhaa huku wananchi wakiwa wamejificha maporini wakielezea unyanyasaji waliofanyiwa na waasi hao. Imeelezwa kuwa hii ni mara ya [...]

12/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wasisitiza ushirikiano katika matumizi ya maji

Mwaka wa kimataifa wa ushirikiano wa matumizi ya maji

Umoja wa Mataifa umezindua rasmi mwaka wa kimataifa wa ushirikiano katika sekta ya maji, ikiwa ni fursa kwa nchi kushirikiana katika menejimenti ya rasilimali hiyo adhimu kwa amani na maendeleo ya wote. Katika ujumbe wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amesema mwaka 2013 ni fursa kwa nchi zote kushirikiana kulinda na kutunza [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Umoja wa Mataifa na Radio za kijamii

Wahariri wa habari wa Radio Kwizera wakiwa kazini

Siku ya Radio duniani tarehe 13 mwezi Februari hutoa fursa kwa mashirika ya utangazaji ya kimataifa na kitaifa pamoja na hata radio za kijamii kutathmini jukumu lao adhimu la kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Umoja wa Mataifa kupitia mashirika yake umekuwa ukifanya kazi kwa ushirikiano na radio hizo ambazo ziko karibu zaidi na jamii. Hutumia radio [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Ban azindua ziara rasmi za watoto ndani ya Makao Makuu ya UM

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon akiangalia kitabu na mmoja wa watoto walioshiriki ziara hiyo.

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezindua rasmi ziara za watoto ndani ya Umoja huo mjini New York Marekani na kusema kuwa ziara za namna hiyo ni fursa ya kuelezea watoto jinsi Umoja wa Mataifa unavyofanya kazi kuboresha maisha ya wakazi mbali mbali duniani na wao wataeneza taarifa hizo. Amewaeleza watoto hao [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban azungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Pope Benedict wa XVI

Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Pope Benedict wa XVI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezungumzia uamuzi wa kujiuzulu wa Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Pope Benedict wa XVI tarehe 28 mwezi huu ambapo ametoa shukrani zake kutokana na mchango wa kiongozi huyo katika kuchagiza mashauriano baina ya waumini wa madhehebu mbali mbali duniani. Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Umoja wa Mataifa [...]

11/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Tega sikio kwa redio itangazayo amani, maendeleo na haki za binadamu: Ban

sg-withradio

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kila mmoja anafaa kuadhimisha Siku ya Redio Duniani kwa kusherehekea uwezo wa redio, na kushirikiana kuufanya ulimwengu uzingatie masafa yanayotangaza amani, maendeleo na haki za binadamu kwa wote. Katika ujumbe wake wa video, Bwana Ban amesema tangu kubuniwa kwake zaidi ya miaka 100 iliyopita, redio imekuwa [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

UNESCO yasaidia uandaaji wa mitaala ya uandishi wa habari Tanzania

Rose Haji, Mshauri na Mratibu wa Mafunzo kwa Radio Jamii, UNESCO, Tanzania katika moja ya mafunzo kwa waandishi wa habari

Moja ya sababu zinazowatia waandishi wa habari na watangazaji wa Radio hatarini wanapofanya kazi zao ni ukiukaji wa maadili. Waandishi wa habari na watangazaji baadhi yao kwa kukosa stadi sahihi hutangaza habari kupitia radio bila kuzifanyia utafiti au pengine za upande mmoja. Nchini Tanzania ukosefu wa maadili umeripotiwa kusababishwa pia na elimu isiyotosheleza inayotolewa na [...]

11/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNDP ataka hatua za haraka dhidi ya magonjwa yaso ya kuambukiza

Jarida la Lancet Oncology

Msimamizi wa Shirika la Mpango wa Maendeleo katika Umoja wa Mataifa, Helen Ckark, ametoa wito hatua thabiti na za haraka zichukuliwe ili kusitisha kuenea kwa magonjwa kama vile saratani na kisukari kote duniani, akisema kuwa magonjwa haya yasiyo ya kuambukiza daima yapo kwenye ajenda ya kimataifa maendeleo. Akizindua msururu wa machapisho katika jarida la masuala [...]

11/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

FAO, IFAD zatiliana saini mpango wa kuwasaidia wakulima wadogowadogo

farming Africa

Mashirika mawili ya Umoja wa Mataifa yametiliana saini ili kufanikisha mpango wa kuwapiga jeki wakulima wadogo wadogo na wale wanaoishi maeneo ya vijijini walioko katika nchi zinazoendelea. Mashirika hayo lile la chakula na kilimo FAO na lile la maendeleo ya kilimo, IFAD kwa pamoja yamekubaliana kutoa kiasi cha dola za Marekani 875,000 ili kuwaendeleza wakulima [...]

11/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ugonjwa wa ngozi uenezwao kwa uchafu walipuka Syria

Watoto Syria

Ugonjwa wa ngozi uenezwao kutokana mazingira machafu, Leishmaniasis umeripotiwa kulipuka nchini Syria, ikiwa ni miezi kadha tangu kutolewa kwa onyo juu ya uwezekano wa kulipuka kwa ugonjwa huo. Visa 955 vya ugonjwa huo vimeripotiwa kwenye maeneo ya Hamah, Hassaka, Damascus na Homs nchini Syria. Shirika la afya duniani WHO limetoa huduma zikiwemo madawa na mahitaji [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

CERF yasaidia waathirika wa mafuriko Msumbiji

Jennifer Topping (Picha-UM)

Mfuko mkuu wa misaada ya dharura wa Umoja wa Mataifa CERF, umetoa zaidi ya dola Milioni Tano kwa ajiliya wahanga wa mafuriko nchini Msumbiji. Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Jennifer Topping amesema licha ya kwamba misaada ya awali ilikwishatolewa lakini bado kuna watu wenye mahitaji makubwa ya kibinadamu nchini Msumbiji. Amesema msaada [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kamati ya kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake yaanza kikao Geneva

stopviolenceagainstwomen-300x294

Kamati inayohusiana na kutokomeza ubaguzi dhidi ya wanawake imeanza kikao chake cha hamsini na nne leo mjini Geneva, Uswisi kwa kupokea ripoti za vikao vilivyotangulia na kuweka ajenda mpya. Kamati hiyo pia imemchagua Bi Nicole Amelie kutoka Ufaransa kama mwenyekiti wake mpya, huku wanawake wengine wawili, Violeta Neubauer kutoka mashariki mwa Ulaya na Pramila Patten [...]

11/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

SUDAN na kikundi cha JEM watiliana saini makubaliana ya kusitisha mapigano

darfur

Serikali ya Sudan na kikundi kikuu cha waasi huko Darfur, cha Justice and Equality Movement, JEM wametiliana saini mkataba wa kusitisha mapigano ambao tayari umeanza kutekelezwa. Utiaji saini huo uliofanyika Doha, umeshuhudiwa na Kaimu Mwakilishi wa kikundi cha pamoja na Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa huko Darfur, UNAMID Aichatou Mindaoudou na Naibu Waziri [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Chad yaridhia mkataba unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia

vichwa vya nyuklia

Idadi ya nchi zilizoridhia mkataba wa kimataifa unaopiga marufuku majaribio ya nyuklia imeongezeka na kufikia 159 baada ya Chad kuridhia mkataba huo. Katibu Mtendaji wa shirika la kuratibu usimamizi wa mkataba huo Tibor Tóth ameunga mkono hatua hiyo ambayo amesema inaimarisha msimamo wa Afrika wa kutokomeza majaribio ya nyuklia na hatimaye kufikia lengo la kuwa [...]

11/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira wang'oa nanga Nairobi

Mkutano wa vijana kuhusu mazingira ukiendelea Nairobi, Kenya

Mkutano wa  kimataifa wa vijana wa juma moja kuhusu mazingira umeng'oa rasmi hii leo mjini Nairobi nchini Kenya mkutano ambao unawaleta pamoja zaidi ya vijana 800 kutoka pembe zote za dunia. Kongamano hilo lijukanalo kama TUNZA International Youth Conference on the Environment  linawaleta pamoja vijana kutoka karibu mataifa 100 kujadili hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa ili [...]

11/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Feltman asisitizia uchaguzi wa amani na uwazi nchini Kenya baada ya ziara yake Afrika

Jeffrey Feltman

Mkuu wa masuala ya Kisiasa katika Umoja wa Mataifa, Jeffrey Feltman, leo ametoa wito kwa Kenya kufanya uchaguzi wa amani, uwazi na kwa njia ya kuaminika. Akikutana na waandishi habari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, Bwana Feltman amesema ziara yake nchini Kenya iliangazia uchaguzi huo wa tareje 4 Machi, na [...]

08/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Hatua mathubuti zahitajika kukabili ukatili wa kingono Afrika Kusini: Pillay

Navi Pillay

Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa, Navi Pillay, ameelezea kushtushwa na kuhuzunishwa na kitendo cha ubakaji na mauaji ya kikatili ya msichana mmoja raia wa Afrika Kusini, na kutaka mkakati wa kina uwekwe ili kukabiliana na suala la ukatili wa kingono, ambalo amelitaja kuwa jinamizi linalowakumba maelfu ya wanawake nchini Afrika [...]

08/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

UNICEF kueneza mafanikio zaidi ya elimu jumuishi

inclusive education

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limetaja mafanikio zaidi yatokanayo na elimu jumuishi baada ya sera endelevu kuhusu mpango huo kuonyesha mafanikio makubwa katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki pamoja na Asia ya Kati. Akizungumza na Radio ya UM mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Elimu Jumuishi, Paula [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM walaani mwanamke kuchomwa moto kwa tuhuma za uchawi

Wananchi wa Papua New Guinea

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Navi Pillay ameelezea masikitiko yake kufuatia ripoti kuwa mwanamke mmoja huko Papua New Guinea mwenye umri wa miaka 20 aliteswa na kuchomwa moto hadi kufa kwa tuhuma za uchawi siku ya Jumatano. Taarifa zinasema kuwa mwanamke huyo Kepari Leniata alichomwa moto akiwa hai na kundi [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mikopo kwa mangariba yaokoa afya ya wanawake na watoto wa kike

Kampeni ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike

Siku ya Jumatano ya tarehe Sita mwezi Februari mwaka huu wa 2013, dunia ilipata fursa ya kutathmini harakati za kutokomeza ukeketaji wa watoto wa kike na wanawake, FGM. Siku hiyo ilikuwa ni fursa maalum kwa kuwa ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wanawake na watoto kama ilivyopitishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa [...]

08/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Tetemeko la ardhi huko Solomon laacha watu 3500 bila makazi

Mkazi wa visiwa vya Solomon

Zaidi ya nyumba 430 zimeharibiwa kwenye mkoa wa Temotu na kuwaacha watu 3500 bila makazi kufuatia tetemeko la ardhi na mawimbi ya baharini, Tsunami vilivyokumba visiwa vya Solomon. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka lakini tayari watu sita wameripotiwa kufa huku wengine wanne wakiwa hawajulikani walipo akiwemo mtoto aliyesombwa na maji hadi baharini. Kituo cha kushughulikia masuala [...]

08/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hatua zichukuliwe kutokomeza kutumikishwa: ILO

Watoto wakiwa wanaomba mjini

Ripoti mpya kutoka kwa Shirika la kazi duniani ILO imeangazia hatua zinazostahili kuchukuliwa ili kumaliza ajira za lazima ambapo wanawake , wanaume na watoto milioni 21 kote duniani wanadhulimiwa na kusafirishwa kiharamu kwa biashara ya ngono na utumwa. Kulingana na ILO jitihada za kutambua na kuzuia visa vya ajira  za lazima mara nyingi zimeshindwa kuzaa [...]

08/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wapongeza bunge la Ufilipino kwa kupitisha muswada wa kulinda wakimbizi wa ndani

Wakimbizi wa ndani huko Mindanao

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limepongeza hatua ya bunge la Ufilipino la kupitisha muswada wa sheria wa kulinda haki za wakimbizi wa ndani nchini humo. Muswada huo uliopitishwa wiki hii utakuwa sheria pindi utakapotiwa saini na Rais Benigno Aquino wa III, na hivyo kuifanya Ufilipino kuw anchi ya kwanza kwenye ukanda [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Familia 967 zahamishiwa kwenye kambi huko DRC: IOM

Familia za wakimbizi katika moja ya shule huko Goma, DRC

Shirika la kimataifa la Uhamiaji, IOM pamoja na washirika wengine wamekamilisha mpango wa siku mbili wa kuhamisha familia 967 zilizokuwa zimepata hifadhi katika shule tatu na kuwapeleka kwenye kambi za wahamiaji huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Kuondoshwa kwa familia hizi kutoka shule za Ushindi, Neema na Nazareen na kupelekwa kambi ya Mugunga 1, [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za maji na usafi zimeathiriwa na mzozo nchini Syria: UNICEF

Huduma ya maji

Watoto nchini Syria wamo katika hatari ya kuambukizwa magonjwa kwa sababu ya uharibifu mkubwa wa mifumo ya huduma za maji na usafi ulosababishwa na mzozo ambao sasa umedumu karibu miaka miwili. Haya ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto, UNICEF. Uchunguzi wa kitaifa uloongozwa na UNICEF, na ambao kwa mara [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Somalia bado yahitaji misaada ya kibinadamu : WFP

Wanawake na watoto Somalia wakisubiri msaada

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa, WFP limesema bado Somalia inahitaji misaada ya kibinadamu kwa kuwa mafanikio yaliyopatikana kwenye uhakika wa chakula na usalama bado si endelevu hususan maeneo ya Kusini ambako ni vigumu kuingia. WFP imesema zaidi ya watu Milioni Moja Kusini mwa Somalia wanahitaji misaada huku ikitaja watoto zaidi ya [...]

08/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM na wadau watangaza ombi la dola milioni 892.6 kuisaidia D.R.C

wakimbizi wa DRC

Mashirika ya Umoja wa Mataifa, wadau katika masuala ya kibinadamu pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), leo wametangaza ombi la dola milioni 892.6 kwa ajili ya kufadhili mpango wa kuchukua hatua za kibinadamu mwaka 2013, ili kusaidia mamilioni ya watu ambao wameathiriwa na uhaba wa chakula, migogoro na magonjwa. Akizungumza wakati [...]

08/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Radio ni muhimu sasa kuliko wakati wowote ule!

Wanawake Tanzania wafundishwa kutumia radio

Kuingia kwa zama za Televisheni kwa baadhi ya watu kulionekana kuwa mwanzo wa kuporomoka kwa usilizaji wa Radio. Lakini fikra hizo zimeonekana kuwa potofu kwa kuwa bado Radio inasikilizwa na watu wengi zaidi kuliko televisheni. Radio bado ina umuhimu wake na ndio maana Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilitangaza tarehe 13 Februari ya kila [...]

07/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Radio ya Umoja wa Mataifa enzi hizo

microphone

Jumatano ya tarehe 13 mwezi huu wa February, mamilioni ya watu duniani kote wanasherehekea siku ya Radio duniani. Tukio hili linalenga kuonyesha nguvu ya radio na umuhimu wa matangazo yake yanayofikia mamilioni ya watu kwa nia ya kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha. Maadhimisho haya yanarejelea mwaka 1946 ambapo Umoja wa Mataifa uliamua kuanzisha radio yake yenyewe. [...]

07/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ijue Radio ya Umoja wa Mataifa

un-radio-micro-historico

Radio ya Umoja wa Mataifa imetoka mbali, kuanzia mwaka 1946 ilipoanzishwa katika ofisi na studio za kuhama hama kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, New York, Marekani. Hapo ndio ilianza kurusha matangazo yake ya kwanza kabisa yakisema "Huu ni Umoja wa Mataifa ikiwaita wakazi wote wa dunia." Vipindi kama vile taarifa za habari na [...]

07/02/2013 | Jamii: Siku ya Radio Duniani | Kusoma Zaidi »

Ban amteua Tamrat Samuel kama Mwakilishi wake Maalum Liberia

UNMIL

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, leo ametangaza uteuzi wa Bwana Tamrat Samuel kama naibu mwakilishi wake maalum wa masuala ya uongozi wa kisheria katika ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Liberia (UNMIL). Bwana Samuel atamrithi Bwana Louis M. Aucoin kutoka Marekani, ambaye amehitimisha majukumu uake mnamo Disemba 2012. Bwana Ban ameelezea kufurahishwa [...]

07/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UM wataka haki itendeke Bangladesh kwa watuhumiwa wa uhalifu

Mtaalamu huru wa Umoja wa Mataifa Christof Heyns

Wataalamu huru wawili wa Umoja wa Mataifa wameonyesha wasiwasi wao vile ambavyo Bangladesh inasikiliza na kuhukumu watuhumiwa wa vitendo vya zamani vya uhalifu na wametaka haki itendeke. Wataalamu hao wa haki za binadamu Christof Heyns, na Gabriela Knaul wameonyesha wasiwasi wao kufuatia mwenendo wa mashauri yaliyotangulia ambapo watuhumiwa Abdul Kalam Azad alihukumiwa adhabu ya kifo [...]

07/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Wakulima Misri watarajia mabadiliko katika kilimo: ILO

Kilimo Misri

  Wakati msismko wa mapinduzi ya mwaka 2011 bado unahisiwa nchini Misri, wakulima wengi nchini humo wanatarajia kwamba sekta ya kilimo nayo itafikiwa na mabadiliko mazuri. Wakulima hao wanatarajia mabadiliko katika sheria, wakisaidiwa na Shirika la Ajira Duniani, ILO, ili biashara zao za kilimo ziwe na faida zaidi. Inatarajiwa kuwa hali hiyo itachangia kwa kiasi [...]

07/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Ban akaribisha mazungumzo ya Kachin

KM Ban Ki-moon

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amekaribisha na kupongeza hatua ya kuwepo kwa mazungumzo yenye shabaha ya kutanzua mkwamo wa eneo la Kachin la China na Mynmar. Pande zote mbili zimetoa taarifa ya pamoja iliyoelezea namna zilivyodhamiria kuanzisha majadiliano ili kuepusha uwekekano wa kuzidisha machafuko katika jimbo la Kachin linalowaniwa na pande zote [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNHCR kusambaza ATM kwa wakimbizi wa Syria

Wakimbizi wa Syria

  Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR limepanga kupanua huduma yake ya usambazaji wa misaada ya fedha kwa njia ya mashine zinazojiendesha yaani ATM kwa mamia ya wakimbizi wa Syria walioweka kambi kaskazini mwa Lebanon. UNHCR imesema kuwa hadi kufikia Marchi mwaka huu inaamini itakuwa imesambaza kadi za atm kwa zaidi ya [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

ICC yaitaka Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi kwake

Mahamaka ya ICJ

Majaji wa Mahakama ya kimataifa ya uhalifu, ICC, imeamuru kuwa serikali ya Libya imkabidhi aliyekuwa mkuu wa idara ya ujasusi katika serikali ya Muammar Gaddafi, Abdullah al-Senussi kwa mahakama hiyo mara moja. Serikali ya Libya bado inamshikilia pia mwanae Gaddafi, Seif al-Islam, na imekuwa ikisisitiza kwamba inapanga yenyewe kumshtaki na kumhukumu Bwana Senussi. Mapema wakati [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Rushwa yagharimu Afghanistan dola Bilioni 3.9: UM

Huduma ya usafiri nchini Afghanistan

Afghanistan imetajwa kupiga hatua juu ya kukabiliana na vitendo vya rushwa katika ofisi za umma, lakini hata hivyo mafanikio hayo bado ni ya kiwango cha chini. Uchunguzi uliofanywa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa umebaini kuwa pamoja na kuwepo kwa idadi  ndogo ya watu wanajihusisha na vitendo vya rushwa, lakini fedha zilizotokana na mwenendo huo [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemevu yabadilisha maisha: UNICEF

Utekelezaji wa mpango wa elimu jumuishi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF limesema sera endelevu kuhusu elimu jumuishi kwa watoto wenye ulemavu imekuwa na mafanikio makubwa katika nchi za Ulaya ya Kati na Mashariki pamoja na Asia ya Kati. Hayo yamebainika katika kikao cha bodi ya utendaji ya UNICEF mjini New York, Marekani kilichojikita kwenye masuala ya watoto [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UM wafafanua matumizi ya vyombo visivyo na rubani huko DRC

Mkuu wa operesheni za Ulinzi wa amani za UM Hervé Ladsous

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa amani ndani ya Umoja wa Mataifa Hervé Ladsous ametolea ufafanuzi matumizi ya vyombo vya anga visivyo na rubani ambavyo umoja huo umependekeza vitumike kwenye maeneo hatari huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC. Bwana Ladsous amesema kuwa vyombo hivyo kimsingi ni sawa na kusema ni kamera zinazoruka angani ambazo [...]

07/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Wadhaniao huduma za posta zinakufa wanaota ndoto ya mchana: UPU

Huduma za kusafirisha barua na vifurushi

Kadri maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano yanavyozidi kuibuka, baadhi ya watu wamekuwa na hofu juu ya hatma ya huduma za posta, wakidhani kuwa matumizi ya barua pepe, simu za mkononi na hata utumaji wa pesa kwa mtandao ni hati ya kifo kwa huduma za posta. Mkurugenzi Mkuu wa muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU, [...]

06/02/2013 | Jamii: Mahojiano | Kusoma Zaidi »

Mawaziri kujadili masuala ya mazingira Nairobi: UNEP

UNEP_logo-298x300

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) wiki ijayo litakuwa na mjadala kuhusu masuala ya habari wakati wa kikao cha kwanza cha Baraza la Uongozi la UNEP mjini Nairobi, Kenya. Zaidi ya mawaziri 200 wa mazingira, wajumbe wa ngazi za juu, wakiwemo wanasayansi, wachumi, watunga sera, mashirika ya kiraia na viongozi wa biashara wanatarajiwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi zinazoendelea zakumbwa na gharama kubwa zaidi katika biashara: ESCAP/Benki ya Dunia

Kilimo cha kutumia maksai nchini Ethiopia

Ingawa uchumi wa kimataifa umepata sura ya kujumuisha wote, takwimu mpya zilizoandaliwa na Tume ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kiuchumi na kijamii kwa maeneo ya Asia na Pasifiki, (ESCAP) na Benki ya Dunia, zinaonyesha kuwa nchi zinazoendelea ndizo zinazobeba mzigo mkubwa zaidi wa gharama ya kufanya biashara. Takwimu hizo zinaonyesha kuwa licha ya [...]

06/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Teknolojia ya mawasiliano yaimarisha huduma za posta: UPU

Vifurushi

Mkurugenzi Mkuu mpya wa Muungano wa mashirika ya posta duniani, UPU Bishar Hussein amesema kadri teknolojia ya mawasiliano inavyoimarika ndivyo ilivyo kwa huduma za posta na hivyo changamoto ni kwa mashirika ya posta duniani kuwa na ubunifu zaidi ili yaweze kwenda na wakati. Bwana Hussein ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Pillay alaani mauaji ya mtetezi wa haki za binadamu nchini Tunisia

Navi Pillay

  Kamishina Mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay amelaani mauaji ya Katibu Mkuu wa kikundi cha vuguvugu la wazalendo nchini Tunisia, DPM, Chakri Belaid. Pillay amesema amehuzunishwa na taarifa za kifo cha Belaid ambaye alikuwa mtetesi mkubwa wa haki za binadamu na akipinga vurugu za kisiasana kueleza kuwa kifo chake [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNFPA yataja changamoto za kukabiliana na ukeketaji wanawake na watoto wa kike

Kampeni ya kutokomeza ukeketaji wanawake na watoto kike nchini Uganda

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Idadi ya watu duniani, UNFPA, Dkt. Babatunde Osotimehin amesema licha ya mafanikio katika kupambana na ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, bado kuna changamoto kubwa kutokomeza kabisa tabia hiyo. Akizungumza katika mahojiano maalum na Radio ya Umoja wa Mataifa, Dkt. Babatunde ametaja changamoto hiyo kuwa ni ajira mbadala kwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatari ya watoto wa kike kukeketwa yapungua, Kenya yatajwa kuwa mfano: Ripoti UM

Watoto wa kike

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo, siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji wa wanawake na watoto wa kike, imesema kuwa hatari ya watoto wa kike kukeketwa imepungua ikilinganishwa na ilivyokuwa zamani. Ripoti hiyo ya mashirika ya Umoja wa mataifa ya UNICEF linalohusika na watoto na UNFPA la idadi watu, imesema katika nchi 29 [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Huduma za afya zaongezeka kutokana na kuwepo usalama nchini Somalia

Somalia health

Baada ya kuimarika kwa usalama baada ya wanamgambo wa Al-Shabab kuikimbia miji ya kusini na kati kati mwa Somalia mashirika ya kutoa misaada sasa yameongeza huduma za kiafya na huduma zingine za dharura katika maeneo ambayo awali ilikuwa vigumu kuyafikia. Mratibu wa masuala ya dharura kwenye shirika la afya duniani WHO nchini Somalia Omar Saleh [...]

06/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Ban na Jim wajadili malengo ya maendeleo ya milenia

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon na Rais wa Benki ya Dunia Jim Yong Kim

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekuwa na mazungumzo na Rais wa Benki ya dunia Jim Yong Kim ambapo wameangalia upya fursa za kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili hizo hususan kwenye maeneo ya nchi za Maziwa Makuu barani Afrika. Taarifa iliyotolewa na ofisi ya msemaji wa Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa Bwana [...]

06/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ushirikishaji jamii dhidi ya ukeketaji ndio siri ya mafanikio: Babatounde

Baadhi ya vifaa vinavyotumiwa na mangariba wa jamii ya Bondo nchini Sierra Leone

Wakati leo ni siku ya kimataifa ya kutokomeza ukeketaji, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la idadi ya watu duniani, UNFPA, Dkt. Babatunde Osotimehin amesema siri ya mafanikio ya vita dhidi ya ukeketaji wanawake na watoto wa kike ni ushirikishaji wa dhati wa jamii husika. Dkt. Osotimehin ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa katika mahojiano maalum kuwa [...]

06/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa CAR, Ban asifu

Wananchi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati

Taarifa za kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati zimepokelewa kwa pongezi na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Upande wa serikali na wale wa upinzani wamefikai hatua hiyo kufuatia makubaliano yaliyotiwa saini huko Libreville, Gabon tarehe 11 mwezi uliopita ambapo Bwana Ban amesema hatua hiyo ya [...]

05/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Ban akerwa na hukumu za Mogadishu dhidi ya mwanamke na mwandishi habari

Ban Ki-Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, ameelezewa kukerwa na hukumu ya kifungo cha mwaka mmoja, ambayo imetolewa mjini Mogadishu, Somalia dhidi ya mwanamke mmoja na mwandishi wa habari. Mwanamke huyo anadaiwa kubakwa na wanaume wenye silaha na ambao walivalia sare za vikosi vya serikali, wakati akiishi katika kambi ya wakimbizi wa ndani. Umoja [...]

05/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNDP na ILO zataja sababu za vuguvugu katika nchi za kiarabu

Vijana wakipambana na askari

Vuguvugu linaloendelea katika nchi za kiarabu limeweka bayana mazingira duni na ukosefu wa haki za kijamii kwenye nchi hizo katika kipindi cha miongo kadhaa ya utekelezaji mbovu wa uchumi huria. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi karibuni zaidi iliyoandaliwa kwa pamoja na shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP na [...]

05/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mashauriano ya dhati kati ya Palestina na Israeli ndiyo suluhu pekee: Ban

Katibu Mkuu wa UM Ban Ki-Moon katika kikao kuhusu haki za msingi za Palestina

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amefungua kikao cha kamati ya haki za kimsingi za wananchi wa Palestina na kusema kuwa ujenzi wa makazi wa walowezi unaofanywa na Israel kwenye Ukingo wa magharibi wa mto Jordan na Yerusalem Mashariki ni batili. Amesema ujenzi huo siyo tu ni kinyume na sheria ya kimataifa bali [...]

05/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Iran iache kukamata waandishi wa habari: Wataalamu UM

Ramani ya Iran

Kundi la wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaohusika na masuala ya haki za binadamu wametoa wito kwa serikali ya Iran kusitisha hatua yake ya kuwakamata waandishi wa habari na kuwaachilia wale ambao bado wanazuiliwa. Wito huo unajiri baada ya tukio la juma lililopita ambapo maafisa wa usalama walivamia afisi za magazeti matano na kuwakamata takriban [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Sera mpya zahitajika kuboresha kilimo cha miti na mimea ya kilimo:FAO

Mfano wa kilimo cha mazao na miti

Mamilioni ya watu wanaweza kujikomboa kutoka kwenye umaskini, njaa na kuharibika kwa mazingira ikiwa mataifa yatafanya juhudi zaidi katika mbinu za  kujumuisha kilimo cha miti na mimea ya chakula au na kilimo  cha mifugo. Hii ni kwa mujibu wa Shirika la kilimo na mazao la Umoja wa Mataifa FAO, ambalo limesema kuwa sekta ya kilimo [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Matibabu ya uraibu wa heroin yanapunguza viwango vya UKIMWI Uhispania: WHO

WHO

Ripoti mpya ya Shirika la Afya duniani, WHO, imesema kuwa nchi ya Uhispania imepiga hatua kubwa katika kupunguza maambukizi na viwango vya virusi vya HIV miongoni mwa watu wanaotumia madawa ya kulevya aina ya heroin, kwa kutoa matibabu dhidi ya uraibu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo ilochapishwa katika jarida la WHO, ufanisi huu umefikiwa kwa [...]

05/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yaanza kutoa huduma za maji na usafi katika kambi ya Doro Sudan Kusini

IOM yasaidia wakimbizi wa kambi ya Doro

  Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeanzisha shughuli za kuimarisha hali ya maji na usafi katika kambi ya Doro iliopo Jimbo ya Upper Nile Sudan Kusini ili kukabiliana na mlipuko wa ujonjwa wa ini wa aina ya Hepatitis E. Wizara ya afya ilitanzaga kuzuka kwa ugonjwa huu katika kambi tatu Sudan Kusini mnamo mwezi [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

UNEP na wadau kujadili uchafuzi wa mazingira Ongoniland

Ogoniland, Nigeria

Wawakilishi wa Shirika la Mpango wa Mazingira katika Umoja wa Mataifa, UNEP, wakiongozwa na Mwakilishi maalum, Erik Solheim, watakutana na viongozi wa ngazi ya juu nchini Nigeria na wadau wengine wiki hii mijini Abuja na Port Harcourt kujadili jinsi ya kutekeleza mapendekezo ya ripoti ya uchunguzi wa UNEP kuhusu uhifadhi wa mazingira katika Ongoniland. Ripoti [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

WFP yaendelea kusambaza vyakula Syria na Mali

Wanawake wakiandaa mlo nchini Mali

Shirika la mpango wa chakula la Umoja wa Mataifa WFP limesema lina mpango wa kuwa limefikisha misaada kwa watu Milioni Mbili na Nusu nchini Syria ifikapo mwezi Aprili mwaka huu. WFP imesema msaada wa chakula unajumuisha bidhaa nane ikiwemo  mchele, sukari, chumvi na kwamba tayari wamepata kibali cha kuingiza nchini humo mafuta kwa ajili ya [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

OCHA yaonya kuhusu kuendelea kwa mzozo wa Syria

Wananchi wa Syria wakisubiri misaada

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA limeonya kuwa kadri mzozo wa Syria unavyoendelea wakati huu ukiingia takribani mwaka wa pili mahitaji ya kibindamu yanaongezeka na hivyo ni vyema mgogoro huo ukapatiwa ufumbuzi. OCHA imesema kwa sasa kuna zaidi ya watu Milioni Nne wanahitaji msaada wa dharura na wengine zaidi ya [...]

05/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Jiunge na Umoja wa Mataifa

radio-spot

Umoja wa Mataifa, kimbilio la ulimwengu wakati wa matatizo magumu duniani kote: Kuanzia kumaliza migogoro, kuondoa umaskini, kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, na utetezi wa haki za binadamu. Masuala ndani ya ajenda za Umoja wa Mataifa ni mengi na tofauti kama vile ilivyo kwa fursa za ajira zinazotolewa na umoja huo. Miongoni mwa wafanyakazi [...]

04/02/2013 | Jamii: Jiunge na Umoja wa Mataifa | Kusoma Zaidi »

UM walaani mauwaji ya kwenye makao makuu ya polisi Kirkuk

Kobler

Mwakilishi maalum wa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq amelaani vikali shambulizi la kupangwa lililolenga makao makuu ya jeshi la polisi, katika mji wa Kirkuk ulioko kaskazini mwa nchi hiyo na kuua watu kadhaa na wengine kujeruhiwa. Martin Kobler ambaye pia anaongoza ofisi ya ujumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Nchi za Asia zajadiliana kuhusu njia za kupunguzwa kwa vichafuzi kwa hewa

pollutants Asia

Wawakilishi wa serikali kutoka mataifa 19 ya Asia wameanza mikutano mjini Bangkok hii leo inayoandalaiwa na maafisa wa mazingira kutoka nchini Bangladesh na Japan kutafuta mbuni za kupunguza athari za muda mfupi za uchafuzi wa mazingira katika eneo la Asia. Vichafuzi vya mazingira vikiwemo carbon na Methane vinachangia katika kupanda kwa joto duniani hivi sasa [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Thuluthi mbili za visa vya saratani vyaweza kuepukika: WHO

Mgonjwa wa saratani Tanzania

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema zaidi ya asilimia sabini ya visa vya ugonjwa wa saratani vinaweza kuzuiliwa. Kwenye ujumbe wake wa siku ya saratani duniani ambayo ni leo tarehe nne Februari, WHO imesema hili linawezekana ikiwa nchi zitaongeza uwezo wao wa kudhibiti saratani. Shirika hilo limesema na kwamba nusu ya nchi kote duniani hazina [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkuu wa UNESCO aanza ziara Tanzania

Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi wa Tanzania Dkt. Shukuru Kawambwa

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Irina Bokova yuko nchiniTanzaniakwa ziara rasmi ya siku tatu ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi mbali mbali. Taarifa kutoka tovuti ya UNESCO inasema viongozi hao ni pamoja na mawaziri wa Mawasiliano, Sayanasi na Teknolojia, Elimu na Mafunzo ya Ufundi, pamoja na [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Marathoni kuinua hadhi ya Nairobi kama mji mkuu wa mazingira wa dunia.

Nick Nuttal nwa UNEP akiwa na baadhi ya wanariadha mashuhuri wa Kenya

Baadhi ya wanariadha mashuhuri wa Kenya wa marathoni na wale wanaoibukia watashiriki katika mbio maalum zilizoandaliwa na Shirika la mazingira la Umoja wa Mataifa, UNEP mjini Nairobi kwa lengo la kuinua zaidi hadhi ya mji huo kama mji mkuu wa uhifadhi wa mazingira wa dunia. UNEP inasema mbio hizo za kilometa 21 zitakazofanyika tarehe 24 [...]

04/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

UNICEF yaanza kusambaza dawa za kutakasa maji kwa Wasyria

Mgao wa maji kwa wananchi wa Syria

  Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeanza operesheni ya aina yake ya kuhakikisha wasyria walioko katika mzozo wanapata majisafina salama kwa kusambaza dawa za kutakasa maji. Matenki yaliyojazwa maji ambayo yamewekewa dawa maalumu za kutakasa maji yamesafirishwa kupitia mpaka waJordanhadi katika miji yaHoms,Aleppo,Hamana Idlepo ambako kiasi cha watu zaidi ya milioni [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Watoto DRC watumia sanaa kuelezea madhila yao

Mchoro wa askari akimshambulia mtoto

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na washirika wake wamewezesha watoto huko Mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia yaCongo, DRC ambao walikumbwa na athari za kisaikolojia kutokana na mapigano kati ya majeshi ya serikali na waasi, kuweza kuelezea fikra na madhila yaliyowakumba kupitia sanaa na uchoraji. UNICEF imetenga eneo maalum la watoto [...]

04/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Feltman apongeza mchango wa Burundi nchini Somalia

Ramani ya Burundi

Msimamizi Mkuu wa masuala ya kisiasa ndani ya Umoja wa Mataifa Jeffrey Feltman amehitimisha ziara yake nchini Burundi na kupongeza mchango wa nchi hiyo katika ujenzi wa amani na utulivu nchini Somalia. Feltman amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari mjini Gitega nchini Burundi baada ya mazungumzo yake na Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunziza. [...]

02/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Baraza la Usalama lalaani shambulio kwenye Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki

Kikao cha Baraza la Usalama

Kufuatia shambulio dhidi ya Ubalozi wa Marekani nchini Uturuki siku ya Ijumaa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo hicho na kusema kuwa ni cha kinyama huku wajumbe wake wakituma rambirambi kwa wafiwa. Taarifa iliyotolewa na baraza hilo imesema linasikitishwa na shambulio hilo mjini Ankara  ambalo limesababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi.. [...]

02/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

UNESCO yaanza harakati za ukarabati na uhifadhi wa maeneo ya urithi wa kiasili Mali

Mkurungenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova na Rais wa Ufaransa François Hollande wakipatiwa maelezo katika moja ya maeneo waliyotembelea

"Tunataka hatua za haraka za kulinda na kujenga upya maeneo ya kipekee ya urithi wa kiutamaduni nchini Mali". Hiyo ni kauli ya Mkurugenzi Mkuu wa  Shirika la Umoja wa Matiaifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Irina Bokova, aliyoitoa Jumamosi baada ya kuwasili nchini Mali, ikiwa ni sehemu ya harakati za shirika hilo za kusaidia [...]

02/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Waliotumia madawa ya kulevya na harakati za kujikomboa

UNODC_DRUGS

Madawa ya kulevya yameendelea kuwa tishio siyo tu kwa uchumi wa nchi kwa kuwa vijana wanatumbukia katika lindi hilo na kushindwa kufanya kazi, bali pia kijamii kwa kuwa waathirika wa madawa hayo wanashindwa kufanya kazi na hata kuleta mizozo ya kijamii ndani ya familia na jamii zao. Umoja wa Mataifa kupitia ofisi yake ya kupambana [...]

01/02/2013 | Jamii: Makala za wiki | Kusoma Zaidi »

Mkakati mpana wahitajika kudhibiti kauli za chuki: Dieng

Adama Dieng, Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuzuia mauaji ya kimbari.

Harakati zozote za kudhibiti kauli chochezi na za chuki zinazoweza kusababisha migogoro zinahitaji mpango mpana unaojumuisha pande nyingi. Hiyo ni kauli ya Adama Dieng, Mshauri maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu jinsi ya kuzuia mauaji ya kimbari, kauli ambayo ameitoa wakati wa mkutano wa kujadili suala hilo mjini New York, Marekani. Dieng amesema hilo ni [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Kila 1 kati ya nchi 2 duniani hazipo tayari kuzuia na kutibu saratani: WHO

2cancer_jpeg

Zaidi ya nusu ya nchi kote duniani hazina uwezo wa kuzuia na kutoa matibabu dhidi ya saratani, kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Afya Duniani, WHO. Shirika hilo limesema nyingi ya nchi hizi hazina mpango tekelezi wa kudhibiti kansa, ambao unajumuisha kuzuia, kugundua mapema, kutibu na huduma za uuguzi. WHO inasema kuna haja [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Uendeshaji wa kesi ya ubakaji Somalia inatia wasiwasi: UNPOS

somalia-map1

Kuhusu maswala ya haki nchini Somalia, Afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya kisiasa nchini Somalia (UNPOS), imeelezea wasiwasi wake kuhusu jinsi kesi inayohusu madai ya ubakaji dhidi ya mwanamke mmoja wa Kisomali inavyoendeshwa. Watu watano wameshtakiwa katika kesi hiyo iliyofunguliwa na polisi ikisema kuwa habari zilizochapishwa kuhusu madai ya ubakaji huo, zilikuwa za [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

IOM na UNDP washirikiana kuwasaidia wahamiaji wa Chad

Safari ya kutoka Ufaransa kurejea Chad

Shirika la wahamiaji duniani  IOM na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa wametia saini mkataba wa kutekeleza programu ya kusaidia wahamiaji wa Chad walio Ufaransa, na ambao wana kiasi kikubwa cha ujuzi na maarifa,  kurudi nyumbani ili kuchangia katika maendeleo ya nchi yao. Msemaji wa IOM Jumbe Omari Jumbe amezungumza na Radio ya Umoja [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Bunge la Urusi litupilie mbali muswada wa propaganda za ushoga.

homophobia1

Kundi la wataalamu huru wa masuala ya haki za kibinadamu la Umoja wa Mataifa limetoa wito kwa bunge la Urusi kutupilia mswada  ambao utaidhinisha kutolewa kwa adabu kwa propaganda zozote zinazohusu ushoga kwa watoto. Wataalamu hao wanaonya kuwa mswada huo utakandamiza haki za binadamu nchini Urusi na kuwalenga zaidi walio mashoga , wasagaji na wale [...]

01/02/2013 | Jamii: Taarifa maalumu | Kusoma Zaidi »

Mwakilishi wa UM yuko Burundi kwa ziara ya siku mbili

Jeffrey Feltman

Msaidizi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya kisiasa, Jeffrey Feltman  amewasili nchini Burundi kwa ziara ya siku mbili. Afisa huyo Mkuu wa Umoja wa Mataifa anatarajiwa kukutana kwa mazungumzo na Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na wawakilishi wa vyama vya kisiasa. Tayari Bwana Feltman amekuwa na mazungumzo hii  leo  na [...]

01/02/2013 | Jamii: | Kusoma Zaidi »

Watoto 210,000 mjini Homs wanahitaji msaada wa kibinadamu: UNICEF

Watoto wa Syria

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwenye mji wa Homs nchini Syria umegundua kuwa jumla ya watu 420,000 nusu yao wakiwa ni watoto wanahitaji msaada wa dharura. Shughuli hiyo ya mwezi mzima ambayo tayari imekamilika iligundua kuwa  karibu watu 700,000 kwenye mji huo waliathiriwa na mzozo ulishuhuhudiwa wakiwemo watu 635,000 waliolazimika kuhama makwao. Watoto ndio walioathirika [...]

01/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

IOM yahofia usalama wa wafilipino waliobakia Syria

Baadhi ya wafilipino waliorejea nyumbani kutoka Syria

Usalama wa raia wa Ufilipino ambao bado wamebakia Syria baada ya wenzao kuanza kurejea makwao unatia hofu shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na uhamiaji IOM. Mratibu wa IOM nchini Syria Othman Belbesi amesema kuwa idadi kubwa ya raia hao wameshindwa kuondoka kutokana  na kutojua namna watavyoondoka. Baadhi yao wanadaiwa kukwama katika maeneo ambayo siyo [...]

01/02/2013 | Jamii: Hapa na pale | Kusoma Zaidi »

Hali ya kibinadamu nchini Somalia yaimarika

Stefano Porretti

Kaimu mratibu wa Umoja wa Mataifa juu ya shughuli za misaada ya kibinadamu nchini Somalia Stefano Porretti, amepongeza maendeleo makubwa yaliyofikiwa nchini humo na kusifia kitendo cha kuwakwamua wananchi waliotumbukia kwenye mzozo ambao sasa wamepungua hadi kufikia milioni 1.05. Hata hivyo afisa huyo ameonya kuwa mafanikio hayo yanaweza kuporomoka kama kutakosekana mipango endelevu. Amesema tangazo la [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Hatimaye msafara wa UNHCR waingia kaskazini mwa Syria

Watoto wakipokea misaada eneo la Azza

Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na wakimbizi UNHCR, kwa mara ya kwanza limefaulu kusambaza vifaa kwa ajili ya kukabiliana na hali ya baridi kwa wakimbizi wa ndani wa Syria waliotawanyika katika eneo la Kaskazini mwa nchi hiyo. Vifaa hivyo ni pamoja na mahema, mablanketi ambapo usambazaji wa huduma hizo ulifanyika kwa ufanisi mkubwa na [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Mgogoro unaoendelea Syria waibua ugonjwa wa ngozi

Taka zikiwa zimesambaa eneo moja nchini Syria

Shirika la Afya duniani WHO limesema mzozo unaoendelea nchini Syria unaendelea kusababisha uhaba wa dawa muhimu kama vile vile nusu kaputi na dawa za kuondoa maambukizi mwilini pamoja na kuibuka kwa magonjwa ya ngozi. WHO inasema maduka ya dawa nchini Syria yanazidi kukosa uwezo wa kutoa dawa za msingi kama vile zile za kutuliza maumivu [...]

01/02/2013 | Jamii: Habari za wiki | Kusoma Zaidi »

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Novemba 2017
T N T K J M P
« okt    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
27282930