Zimbabwe yalaumiwa kwa kukandamiza haki za binadamu

Kusikiliza /

wakimbizi wa Zimbabwe

Umoja wa Mataifa umelaani hatua ya serikali ya Zimbabwe ya kuyaandama mashirika yasiyo ya kiserikali na mengine ikiyafungua katika wakati taifa hilo likielekea kwenye uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Ofisi ya Haki za binadamu ya umoja huo imemtaka Rais Robert Mugabe na utawala wake kuondosha vitisho dhidi ya mashirika hayo ya kiraia na kumtaka kuheshimu haki za binadamu

Taarifa ya ofisi hiyo imekariri tukio la hivi la karibuni la kutiwa mbaroni na maafisa wa polisi Mkurugenzi Mkuu wa chama cha haki za banadmu nchini humo Okay Machisa aliyedaiwa kutoa taarifa za uongo na uchochezi kwa serikali na baada ya kujisalimisha polisi mwenyewe bado yuko rumande.

Pia mwishoni mwa mwaka jana maafisa wengine wawili wa mashirika ya kutetea haki za binadamu walikamatwa na polisi na bado hawajaachiwa.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2017
T N T K J M P
« jul    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031