Zerrougui asikitishwa na mauaji ya watoto yaliyofanywa na AMISOM

Kusikiliza /

Kikosi cha AMISOM

Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto na migogoro ya kivita Leila Zerrougui amesema anasikitishwa sana na taarifa kuwa jeshi la kulinda amani la Umoja wa Afrika nchini Somalia, AMISOM limeua watoto kadhaa wakati wa operesheni zake huko Shabelle siku ya Jumanne.

Ameeleza masikitiko yake wakati huu ambapo Kaimu Mkuu wa AMISOM Meja Jenerali Salvatore Harushimana, ameshatangaza kuwa atachunguza tukio hilo na mazingira yaliyosababisha kutokea.

Bi.  Zerrougui amesifu kitendo cha AMISOM kukiri kisa hicho na kuridhia kuchunguza ndani ya wakati na amesema ni matumaini yake uchunguzi huo utaibuka na matokeo thabiti ya kuepusha kutokea tena kaw kitendo hicho.

Halikadhalika ametaka walinda amani wa Umoja wa Afrika kutambua kuwa ulinzi wa watoto ni jambo muhimu katika operesheni zao zote ikiwemo Mali na maeneo yaliyoathiriwa na kikundi cha waasi cha Lord's Resistance Army.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Mei 2016
T N T K J M P
« apr    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031