Wafanyakazi wa majumbani waendelea kunyanyasika: ILO

Kusikiliza /

mfanyakazi wa nyumbani

Ripoti mpya ya shirika la Kazi duniani, ILO kuhusu hali ya wafanyakazi wa majumbani imeonyesha kupanuka kwa sekta hiyo huku mazingira ya kazi yakiendelea kuwa duni hususan katika nchi zinazoendelea.

Mathalani ripoti hiyo imesema kuwa wafanyakazi hao wanaendelea kunyanyaswa ikiwemo kufanya kazi saa nyingi kupindukia kwa ujira mdogo, kufanya kazi kwa saa nyingi ikitolea mfano Tanzania ambako ambako wastani wa saa za kazi kwa wafanyakazi wa majumbani kwa wiki ni saa 63 huku Austria ikiwa ni saa 15 kwa wiki, ilhali wastani unatakiwa uwe kati ya saa 40 na 48 kwa wiki.

Akizindua ripoti hiyo mjini Geneva, Uswisi leo, Naibu Mkurugenzi wa ILO Sandra Polaski amesema wafanyakazi hao wanatarajiwa kufanya kazi kwa saa nyingi kuliko wafanyakazi wengine na katika nchi nyingi hawana haki sawa za mapumziko ya wiki.

(SAUTI ya SANDRA)

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2015
T N T K J M P
« nov    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031