Upanzi wa miti waokoa wakulima Kenya: UNEP

Kusikiliza /

maji nchini Kenya

Mradi wa Umoja wa Mataifa wa upanzi wa miti kwenye miteremko ya Mlima Kenya umekuwa wa manufaa kwa wakulima waliokuwa wanategemea msimu wa mvua kwenye shughuli zao za kilimo huku pia ukichaangia katika kupunguza umaskini.

Kupitia mradi huo unaohusu upanzi wa miche kwenye sehemu za vyanzo vya maji umewanufaisha wakulima hasa sehemu na mashariki mwa mlima Kenya ambao hutumia maji kunyunyizia mimea yao kando na ilivyokuwa hapo awali.

Christine Mugure Munene ni mmoja wa wakulima walionufaika na mradi huo.

(SAUTI YA CHRISTINE MUGURE)

"Ninaweza kufanya chochote kwa saabu maji yanatiririka wakati wote kwa hivyo hakuna shida ya maji"

Paul Njuguna ambaye ni afisa kwenye mfuko wa Umoja wa Mataifa wa maendelo ya kilimo, IFAD unaofadhili mradi huo anasema kuwa zaidi ya miche milioni Tatu imepandwa kwenye miteremko ya mlima Kenya.

(SAUTI YA PAUL NJUGUNA)

"Kukiwa na miti kwenye vianzo vya maji inahakiisha kwamba wakati mvua inaponyesha maji hutwama kwenye udongo na baadaye hutiririka taratibu na kuhakikisha kuwepo kwa maji kwenye mito kila wakati"

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Machi 2017
T N T K J M P
« feb    
 12345
6789101112
13141516171819
20212223242526
2728293031