UNICEF yaungana na mataifa kadha kupunguza vifo vya watoto

Kusikiliza /

watoto

Mawaziri wa Afya kutoka nchi za Afrika wanakutana Addis Ababa Ethiopita kuanzia leo kwa lengo la kuweka mikakati mipya ya kudhibiti vifo vya watoto.

Ripoti zinasema kuwa idadi ya watoto wanaokufa kwenye nchi za AFrika zilizo kusini mwa jangwa la sahara ilipungua kwa asilimia 39 tangu mwaka 1990. Mataifa mengi ya bara la Afrika kwa sasa yako kwenye mkondo ya kuafikia lengo la maendeleo ya milenia la kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano kwa thulethi mbili ifikapo mwaka 2015.

Kwenye nchi hizo mmoja kati ya watoto wanane huwa anakufa kabla ya kutimiza umri wa miaka mitano. Katika jitihaza za kukabiliana na tatizo hilo serikali za Ethiopia, India na Amerika pamoja na Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF walizindua wito wenye lengo la kuzuia vifo vya watoto mwezi Juni mwaka uliopita mjini Washington ambapo zaidi ya mataifa 160 yalitia sahihi makubaliano ya kuzuia vifo vya watoto kwa miongo miwili inayokuja.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Aprili 2017
T N T K J M P
« mac    
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930