UNICEF yaimarisha usaidizi wake kwa watoto huko CAR

Kusikiliza /

Watoto Jamhuri ya Afrika ya Kati

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF linaimarisha operesheni zake huko Jamhuri ya Afrika ya Kati ili kusaidia maelfu ya watoto wanaohitaji misaada ya dharura baada ya kujikuta katikati ya mzozo unaoendelea hivi sasa nchini humo.

Mwakilishi wa UNICEF nchini huko Souleyman Diabate amesema wamebaini maeneo ambako watoto wameathirika zaidi ni pamoja na N'dele, Bria, Bombari, and Kaga ambako watoto wanaishi katika mazingira magumu kupindukia.

Katika taarifa amekaririwa akisema kuwa ni vyema sana kuwafikia watoto hao hivi sasa na kuwapatia misaada lakini wametaka pande zote husika kuweka ustawi wa kudumu wa watoto hao kama kipaumbele na muhimu sana katika kupatia suluhu mgogoro huo.

UNICEF inasema mzozo wa sasa huko Jamhuri ya Afrika ya Kati umeathiri watu karibu Milioni Moja nukta Nane ambapo Laki nane wanahitaji misaada ya dharura.

Misaada ya haraka inayohitajika ni pamoja na chakula, dawa, maji safi na salama, elimu na ulinzi na kwamba dola Milioni Mbili nukta Moja zahitajika mara moja kusaidia shughuli hiyo..

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031