UNAMID yasambaza misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa Darfur

Kusikiliza /

UNAMID yasambaza misaada Darfur

Ujumbe wa pamoja wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Darfur nchini Sudan, UNAMID umesambaza misaada ya dharura kwa mamia ya raia wanaoteseka katika eneo la Kaskazini mwa Darfur na maeneo mengine ya jirani.

Katika awamu yake ya kwanza, UNAMID ambayo imetumia njia ya anga na barabara, imesambaza kiasi cha kilo 44,000 za sukari kwa wananchi wa vijijji vya Saraf Omra, Kabkabya, El Sereif na Abu Gamra pamoja na vifaa vya kusafishia maji, nguo, magodoro ya kulalia na mablanketi.

Kaimu Mkuu wa UNAMID Aichatou Mindaoudou amesema ofisi yake pia imeshiriki kulinda misafara ya wafanyakazi wa usamaria mwema ambao wakati mwingine hukabiliwa na vitisho vya kushambuliwa toka kwa makundi korofi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2017
T N T K J M P
« dis    
 1
2345678
9101112131415
16171819202122
23242526272829
3031