Umoja wa Mataifa wazungumzia ghasia zinazoshuhudiwa nchini Kenya

Kusikiliza /

Umoja wa Mataifa umetuma rambi rambi zake kwa serikali ya Kenya pamoja na kwa familia za watu waliothiriwa na ghasia zinazoshuhudiwa kwenye eneo la Mto Tana na sehemu zeningine za nchi. Kupitia taarifa iliyotolewa na ofisi ya masuala ya kibinadamu nchini Kenya, Umoja wa Mataifa umelaani kile unachokitaja kuwa vitendo viofu ambavyo tangu mwanzo wa mwaka uliopita vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 450 wakiwemo watoto na akina mama na pia kuwalazimu karibu watu 112,000 kuhama makwao.

Umoja wa Mataifa unasema kuwa unatambua jitihada zinazofanywa na msaada unaotolewa kwa jamii zilizoathirika na kuongeza kuwa uko tayari kutoa msaada kwa serikali ya Kenya na watoa wengine wa huduma za kibinadamu. Huku Kenya ikielekea kwenye uchaguzi mkuu mwezi Machi mwaka huu Umoja wa Mataifa umewataka wakenya kupiga kura kwa njia ya amani na kwa hemisha.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Januari 2018
T N T K J M P
« dis    
1234567
891011121314
15161718192021
22232425262728
293031