AU yazungumzia Madagascar na Mali

Kusikiliza /

mapigano nchini Mali

Umoja wa Afrika umekaribisha hatua ya rais wa Madagascar Andry Rajolina ya kutangaza kutogombea kwenye uchaguzi mkuu wa urais uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu, ikiwa ni sehemu kukubali sharti lililkotoewa na Jumuiya ya Maendeleo Kusin mwa Afrika SADC, iliyotaka kuwepo kwa maelewano ya kisasa ili kuondosha hali ya uhamasama iliyoliandama taifa hilo kwa miaka kadhaa. HAlikadhalika Umoja wa Afrika umezungumzia operaioni za kijeshi zinzoendelea huko mali dhidi ya vikundi vyenye silaha chini Mali.

Kutoka DSM, George Njogopa anaarifu zaidi

Mwenyekiti wa Umoja huo wa afrika ambaye pia ni rais wa Benin Boni Yayi ametoa pongezi hizo jijini Dar es salama wakati alipokutana na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete kujadilia pamoja na mambo mengine migogoro inayoendelea kulikumba bara la afrika na namna ya kusaka ufumbuzi wake.

Kiongozi huyo wa madagasca ametangaza kwamba hatawania kwenye kinyang'anyiro hicho ikiwa ni siku chache tu baada ya kuwa na majadiliano na viongozi wa sadc waliokutana jijini Dsm kwa ajili ya kusaka suluhu kuhusiana na mzozo wa madaraka uliolikumba taifa hilo tangu mwaka 2009.

Kwa upande wake Rais Jakaya Kikwete ambaye ndiye aliyoongoza majadiliano ya kupatikana suluhu ya kudumu, amesema kuwa nchi za sadc zimepokea taarifa hiyo kwa furaha kubwa, na akahaidi uungwaji mkono kwa wananchi wa madagasca

Pamoja na kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na rais Andry Rajolina, kwa upande mwingine Mwenyekiti wa Umoja huo wa Afrika umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuunga mkono juhudi za kuwafurusha wanamgambo walioliteka eneo la Kaskazini mwa Mali.

Amesema msimamo mkali unaochukuliwa na kundi hilo la wanamgambo ambalo linatajwa kuwa na mafungamano ya karibu ya kundi la alqaida, ni kitisho kwa eneo nzima la afrika magharibi hivyo juhudi za pamoja zinapaswa kuchukuliwa sasa ili kuwadhibiti waasi hao.

Zingatio hilo linakuja katika wakati ambapo vikosi vya serikali chini ya msaada wa vikosi vya Ufaransa vikifaulu kuwafurusha wanamgambo hao katika baadhi ya ngome walizokalia, na tayari nchi I wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Afrika Magharibi ECOWAS zimearifu utayari wao wa kuunga mkono operesheni ya kijeshi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kip-moon amepongeza hatua ya uendeshwaji wa opereshni hiyo na ametaka mashirikiano zaidi ili kuwafurusha wanamgambo hao.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Agosti 2014
T N T K J M P
« jul    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031