Udhibiti wa ajali za barabarani huokoa maisha na fedha: WHO

Kusikiliza /

barabara

Utafiti mmoja uliochapishwa na jarida la shirika la afya ulimwenguni WHO, umesema nchi ambazo huchukua njia rahisi kudhibiti ajali za barabarani hunufaika na mambo mengi ikiwemo yale yenye taswira ya kiuchumi.

Utafiti huo uliochapishwa kwenye jarida la mwezi huu umesema kuwa pamoja na kwamba nchi hizo zinakubalika kwa kufaulu kuokoa maisha ya watu, lakini kwa kiwango kikubwa zipo kwenye mkondo unaokubalika kiuchumi.

Miongoni mwa mambo yaliyoangaziwa na utafiti huo ni pamoja na juhudi zilizochukuliwa na mamlaka katika eneo la Catalonia nchini Hispania ambalo liliongeza juhudi za kudhibiti ajali katika kipindi cha mwaka 2010.

Ripoti hiyo imepongeza kuwepo kwa mifumo kama vyombo vya sheria na mabaraza ya utoaji maamuzi. Imesisitiza kuwa maeneo hayo ni muhimu kuwepo kwani yanatoa mchango mkubwa wa kudhibiti ajali za bara barani.

 

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031