Sioni mwelekeo wa dhati huko Mashariki ya Kati: Serry

Kusikiliza /

Robert Serry

Mratibu maalum wa Umoja wa Taifa katika mchakato wa amani huko Mashariki ya Kati, Robert Serry ameeleza wasiwasi wake juu ya kukosekana kwa mwelekeo wa dhati na bayana wa mchakato wa amani mashariki ya kati baina ya Israeli na Palestina.

Bwana Serry ambaye pia ni mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu amesema hayo katika taarifa yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataiaf kuhusu hali ilivyo Mashariki ya Kati na suala la Palestina.

Amesema licha ya kwamba kuna jitihada za kimataifa za kusongesha mchakato huo, bado kunakosekana ushiriki wa dhati wa pande husika.

Bwana Serry, amesema kumekuwepo kwa viashiria ukosefu wa kuaminiana kati ya Israeli na Palestina pamoja na vitendo vinavyokwamisha juhudi za kimataifa.

"Hakuna jitihada za kimataifa pekee zinazoweza kufanikisha bila ya ushiriki wa pande husika. Iwapo wanataka wao na wengine kutoa fursa ya kurejea katika mwelekeo wa mchakato husika basi wakati huu siyo wakati wa vitendo vya kuondoa imani baina yao. Punde baada ya Palestina kupewa hadhi ya uanachama bila uwezo wa kupiga kura ndani ya Baraza kuu, tumeshuhudia vitendo kama vile kuongezeka taarifa za ujenzi wa makazi ya walowezi wa kiyahudi ikiwemo kwenye eneo muhimu la E-1."

Bwana Serry amesema m chakato wa amani au maridhiano siyo suala la kuchagua moja na kuacha lingine bali yote yanakwenda pamoja na ametaka Hamas kueleza bayana wana msimamo gani juu ya suala la msingi kwenye mchakato huo.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031