Serikali ya DRC na waasi wa M23 wakubaliana ajenda ya mazungumzo

Kusikiliza /

Serikali ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, DRC na waasi wa kikundi cha M23 wanaokutana nchini Uganda wamekubaliana juu ya ajenda ya mazungumzo kati yao yaliyoanza tarehe 10 Desemba mwaka 2012 mjini Kampala.

Ajenda ya mazungumzo ilizua vuta nikuvute baina ya pande mbili hizo na kukwamisha mazungumzo kwa siku tano.

Taarifa ya pamoja iliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Uganda Crispus Kiyonga anayeratibu mazungumzo hayo imesema sasa pande hizo zimekubaliana kuanza mazungumzo juu ya ajenda muhimu.

Ajenda hizo ni mapitio ya makubaliano ya tarehe 23 Machi 2009, masuala ya usalama, kijamii, kisiasa na kiuchumi na mpango wa utekelezaji.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Disemba 2017
T N T K J M P
« nov    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031