Nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi: UM

Kusikiliza /

Balozi Masood Khan, Rais wa sasa wa Baraza la Usalama

Baada ya mjadala wa siku nzima kuhusu vita dhidi ya ugaidi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kamwe nguvu za kijeshi haziwezi kutokomeza ugaidi.

Badala yale limesema mkakati wa kina na endelevu ndio njia pekee ya kukabiliana na ugaidi ambapo mkakati huo ushughulikie mazingira yanayochochea vitendo hivyo vya kihalifu.

Baraza hilo limekaririwa kupitia taarifa iliyotolewa na Rais wake Balozi Masood Khan wa Pakistani limetaja mazingira hayo kama vile migogoro na ukiukwaji wa haki za binadamu ambavyo limesema hutunisha na kueneza ugaidi.

Halikadhalika wamesisitiza kuwa hakuna sababu yoyote ile inayoweza kuhalalisha ugaidi kwani kitendo hicho ni uhalifu.

Zaidi ya wajumbe 50 walitoa maoni yao kwenye mjadala huo wa wazi ambapo Baraza limetambua kwa dhati kuwa ugaidi unaendelea kuwa tishio la ulinzi na usalama duniani.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2016
T N T K J M P
« jun    
 123
45678910
11121314151617
18192021222324
25262728293031