Mjumbe maalum wa UM kuhusu ubaguzi wa rangi azuru Uhispania
Kusikiliza /Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ubaguzi wa rangi Mutuma Ruteere ameanza ziara ya juma moja nchini Uhispania ambapo anatarajiwa kukutana na waakilishi wa serikali , wabunge , mahakama, Ombudsman, mashirika yasiyokuwa ya serikali pamoja na makundi yanayofanya kazi kwneye nyanja za ubaguzi wa tangi. Ruteere tayari ashakutana na Waziri wa masuala ya kigeni Gonzalo Benito.
