Misaada yasambazwa kwa wakimbizi DRC: UNICEF

Kusikiliza /

msaada kutoka UNICEF kwa wakimbizi wa DRC

Utulivu siku za hivi karibuni umechangia kuwepo usambazaji wa misaada ni bidhaa zingine muhimu zikiwemo blanketi na nguo kwenye meeneo waliko wakimbizi wa ndani kwenye mkoa wa Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo DRC.

Hii ndiyo oparesheni kubwa zaidi ya ugavi wa bidhaa za nyumbani kufanyika siku za hivi karibuni mkoani Kivu Kaskazini. Watu wanazidi kukimbia makwao kunapoendelea kushuhudiwa ghasia huku zaidi ya watu 130,000 wakiripotiwa kuhama makwao.

Ulrich Wagner ni mtaalamu wa masuala ya dharura kwenye Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

(SAUTI YA WAGNER)

Tuko kwenye kipindi cha mvua, vile unavyoona sasa kuna mawingu mengi, kwa hivyo imenyesha leo itanyesha usiku watu wanahitaji makao hasa watoto ambao wanaweza kupata maambukizi.

Febe Bushu mwenye umri wa miaka 64 anaishi eneo hilo na mabinti wake wawili. Wote hawa walitembea kwa muda wa majuma mawili hivi kabla ya kuwasili mjini Goma.

(Swahili Clip)

Hata hivyo changamoto kubwa kwa wakimbizi wa ndani inabaki kuwa usalama hasa usiku wakati kunaposhuhudiwa visa vingi.

Kipindi Kamili
Kipindi Kamili
Loading the player ...

 

Julai 2014
T N T K J M P
« jun    
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
28293031